Fund man
JF-Expert Member
- Feb 24, 2021
- 3,629
- 4,831
Wataisoma namba.Hapo ndipo utajua ccm ni kubwa yaani barua ya kujiuzulu kaandikiwa Katibu Mkuu wa Chama.
Safi Sana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wataisoma namba.Hapo ndipo utajua ccm ni kubwa yaani barua ya kujiuzulu kaandikiwa Katibu Mkuu wa Chama.
Safi Sana.
Ndugai sijawahi kumfagilia hajawahi kuwa na msimamo thabiti amekuwa na lugha za kejeli kwa wabunge, wananchi na hatimaye rais wa nchi. Wapinzani wake wa kisiasa amewacharaza bakora. Amehusika katika kutunga sheria kandamizi ambazo leo hii zitatumika kumuhukumu yeye.View attachment 2071031
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo Januari 06, 2022 ikiwa ni siku chache tangu kusambaa kwa video ambayo alinukuliwa akisema ipo siku Nchi itauzwa kutokana na madeni
Amesema ameandika Barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM na uamuzi huo ni binafsi na hiari, na ameuchukua kwa kuzingatia maslahi mapana ya Nchi, Serikali na Chama
#JamiiForums
Mbunge wa Kongwa (CCM), Job Ndugai tarehe 10 Novemba 2020, alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 12 baada ya kupata kura 344 kati ya kura 345 zilizopigwa sawa na asilimia 99.7. Kura moja ilimkataa. Ndugai alikuwa spika katika Bunge la 11 la 2015 - 2020.
Hapo awali akizungumza Desemba 28 katika mkutano mkuu wa pili wa wanakikundi cha Mikalile Ye Wanyusi uliofanyika jijini Dodoma, Ndugai alitetea uamuzi wa Bunge kuanzisha tozo za miamala ya simu, kuliko kuendelea kukopa kwani ipo Siku Nchi itapigwa Mnada
“Juzi mama ameenda kukopa 1.3 trilioni. hivi ipi bora. Sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni au tubanane banane hapa hapa, tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa haya yasiyoeleweka. Ni lini sisi tutafanya wenyewe ‘and how’ (na kwa vipi),” alisema Spika Ndugai.
Job Ndugai alihoji wanaofurahia nchi kukopa na kwamba deni limefika Sh70 trilioni.
Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni
Spika wa bunge la jamhuri ya muungano JOB NDUGAI amedai kuwa kulingana na mwenendo wa deni la taifa kufikia trilion 70 ipo siku nchi ya Tanzania itapigwa mnada amenena maneno hayo baada ya kusema kwamba tozo zote zamiamala ya simu zilizopitishwa na bunge zilipitishwa kwa lazima kwani wananchi...www.jamiiforums.com
RAIS SAMIA ASHANGAZWA NA SPIKA NDUGAI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alieleza kushangazwa na kauli za Spika wa Bunge Job Ndugai kusimama hadharani na kukosoa mkopo wa Shilingi Trilioni 1.3 kutoka shirika la Fedha Duniani (IMF) wenye lengo la kuchochea mapambano dhidi ya UVIKO -19 wakati taarifa mbalimbali zinapitia kwenye bunge lake.
Akizungumza Jumanne Januari 4,2022 Jijini Dar es salaama wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ikiwemo elimu, afya,maji na miundombinu, Rais Samia alionyesha kukerwa na kile alichokisema Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu Serikali kukopakopa badala ya kujiendesha kwa pesa za ndani.
“Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025. Inashangaza kuona mtu mwenye uelewa, anasema kuna fedha ya tozo lakini kaenda kukopa, ya nini? Au kwa nini tunaendelea kutoa tozo wakati fedha ya mkopo ipo. Mawaziri tupeni hizo takwimu sasa hivi.
"Mtu na akili yake anasimama na anahoji kuhusu mikopo na tozo, sio lolote ni homa ya 2025, kwa mtu ambaye nilimtegemea kushirikiana naye kwenye maendeleo, sikutegemea kama angesimama na kusema maneno hayo. Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025", amesema Rais Samia.
Soma:
Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"
Kwa mujibu wa taarifa yake kwa umma, Ndugai amesema kuwa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kujiuuzulu nafasi hiyo ikibainisha kuwa uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari.
“Naomba kutoa taarifa kwa uma wa watanzania kuwa leo Tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa wa Tanzania” imesema sehemu ya taarifa hiyo nakuongeza
“Pia nakala yangu hiyo ya kujiuzulu nimewasilisha kwa katibu wa Bunge
View attachment 2070821
======
WASIFU
========
Job Yustino Ndugai (58) ni mwanasiasa kutoka Tanzania ambaye anahudumu kama Spika wa Bunge tangu mwaka 2015. Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2010.
Alizaliwa Januari 21, 1963 alipata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1991-1997. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.
Amesoma Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka kuanzia mwaka 1986-1988, kisha Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989-1993).
Amesoma Post Graduate kutoka Chuo cha Kilimo nchini Norway kuanzia 1994-1995 na kusoma Shahada ya Umahiri kutoka chuo hicho (1995-1996).
Safari yake ya elimu iliishia Eastern and Southern African Management Institute ambapo alisoma Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (2005-2008)
Amekuwa mbunge wa Kongwa kwa miaka 21 sasa (tangu mwaka 2000) na ameshika nafasi mbalimbali ndani ya kamati za bunge.
Alichaguliwa kuwa spika wa bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika.
Mbali na ubunge, amefanya kazi sehemu nyinginezo ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pori la Akiba Selous na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).
Januari 6, 2022 amejiuzulu nafasi ya Uspika kutokana na sababu binafsi na kwa hiari yake.
Ndugai ni mume wa Fatuma Mganga.
Lakini mkuu usisahau group la G 55 ndilo lililomuondoa madarakani Katibu Mkuu wa CCM Horace Kolimba na Waziri Mkuu John Malecela.Lile grupu la G70 lililokuwa linadai serikali ya Tanganyika lilikuwa ni la wabunge wa CCM, na wala hawakutishwa hata na watoto wadogo wanaoitwa Vijana wa CCM kama ilivyotokea kwa Ndugai; jamaa wale walifanya hivyo wakati Nyerere akiwa hai. Jambo alilofanya Nyerere nikushawishi kuwa wazo lao halikuwa sahihi, lakini hawakutishiwa kwa namna yoyote ile kuwa watavuliwa uanachama au kuvuliwa nyadhifa zao.
Hata huu unaonekana ni rahisi mno kutikiswa, tatizo ni katiba au viongozi wakuu wa hii mihimili wameshindwa kusimamia vyema katiba?Ule mwingine kwani hamuoni unavyofanya madudu na matapu tapu kwa ile kesi maarufu
Wakati wa awamu ya 5 huu muhimili ulilaumiwa sana kwa kujipendekeza kwa serikali.........huenda Job alitaka kuivunja hii ndoa haramu kati ya bunge na serikali (japo alishiriki kuiasisi) sema wana Ccm wenzake na baadhi ya wapinzani hawakumuelewa badala yake wameangalia rekodi yake ya nyuma bila kujua hata saa mbovu kuna muda inasema ukweli.Ndugai alikuwa mlinzi wa katiba ya 1977 sasa ni mhanga kwasababu haikumlinda kama kiongozi wa mhimili. Aliishi kwa mazoea na ubabe, good riddance
Kaacha joho kaondoka mtupu ! bila heshima yoyote
Eti ndiye alikuwa spika huyoo! Job kweli kweliDuh, Kaichapa kwa herufi kubwa kuonyesha hasira🐒
Bado unasema fakeHii fake.
Na nani?"ikikubaliwa"
... alikoipeleka.Na nani?
Kwahiyo supika naye atakuwa rais blaza?Nampongeza Ndugai kwa kujiuzulu.Rais Mwinyi aliwahi kujiuzulu na baadae akawa Rais.
Hoja ni kuwa wale wahuni na Chawa kamwe wasipewe nafasi.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!