Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

View attachment 2071031
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo Januari 06, 2022 ikiwa ni siku chache tangu kusambaa kwa video ambayo alinukuliwa akisema ipo siku Nchi itauzwa kutokana na madeni

Amesema ameandika Barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM na uamuzi huo ni binafsi na hiari, na ameuchukua kwa kuzingatia maslahi mapana ya Nchi, Serikali na Chama

#JamiiForums

Mbunge wa Kongwa (CCM), Job Ndugai tarehe 10 Novemba 2020, alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 12 baada ya kupata kura 344 kati ya kura 345 zilizopigwa sawa na asilimia 99.7. Kura moja ilimkataa. Ndugai alikuwa spika katika Bunge la 11 la 2015 - 2020.

Hapo awali akizungumza Desemba 28 katika mkutano mkuu wa pili wa wanakikundi cha Mikalile Ye Wanyusi uliofanyika jijini Dodoma, Ndugai alitetea uamuzi wa Bunge kuanzisha tozo za miamala ya simu, kuliko kuendelea kukopa kwani ipo Siku Nchi itapigwa Mnada

“Juzi mama ameenda kukopa 1.3 trilioni. hivi ipi bora. Sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni au tubanane banane hapa hapa, tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa haya yasiyoeleweka. Ni lini sisi tutafanya wenyewe ‘and how’ (na kwa vipi),” alisema Spika Ndugai.

Job Ndugai alihoji wanaofurahia nchi kukopa na kwamba deni limefika Sh70 trilioni.


RAIS SAMIA ASHANGAZWA NA SPIKA NDUGAI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alieleza kushangazwa na kauli za Spika wa Bunge Job Ndugai kusimama hadharani na kukosoa mkopo wa Shilingi Trilioni 1.3 kutoka shirika la Fedha Duniani (IMF) wenye lengo la kuchochea mapambano dhidi ya UVIKO -19 wakati taarifa mbalimbali zinapitia kwenye bunge lake.

Akizungumza Jumanne Januari 4,2022 Jijini Dar es salaama wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ikiwemo elimu, afya,maji na miundombinu, Rais Samia alionyesha kukerwa na kile alichokisema Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu Serikali kukopakopa badala ya kujiendesha kwa pesa za ndani.

“Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025. Inashangaza kuona mtu mwenye uelewa, anasema kuna fedha ya tozo lakini kaenda kukopa, ya nini? Au kwa nini tunaendelea kutoa tozo wakati fedha ya mkopo ipo. Mawaziri tupeni hizo takwimu sasa hivi.

"Mtu na akili yake anasimama na anahoji kuhusu mikopo na tozo, sio lolote ni homa ya 2025, kwa mtu ambaye nilimtegemea kushirikiana naye kwenye maendeleo, sikutegemea kama angesimama na kusema maneno hayo. Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025", amesema Rais Samia.

Soma:
Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Kwa mujibu wa taarifa yake kwa umma, Ndugai amesema kuwa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kujiuuzulu nafasi hiyo ikibainisha kuwa uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari.

“Naomba kutoa taarifa kwa uma wa watanzania kuwa leo Tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa wa Tanzania” imesema sehemu ya taarifa hiyo nakuongeza

“Pia nakala yangu hiyo ya kujiuzulu nimewasilisha kwa katibu wa Bunge
View attachment 2070821

======

WASIFU

========

Job Yustino Ndugai (58) ni mwanasiasa kutoka Tanzania ambaye anahudumu kama Spika wa Bunge tangu mwaka 2015. Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2010.

Alizaliwa Januari 21, 1963 alipata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1991-1997. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.

Amesoma Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka kuanzia mwaka 1986-1988, kisha Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989-1993).

Amesoma Post Graduate kutoka Chuo cha Kilimo nchini Norway kuanzia 1994-1995 na kusoma Shahada ya Umahiri kutoka chuo hicho (1995-1996).

Safari yake ya elimu iliishia Eastern and Southern African Management Institute ambapo alisoma Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (2005-2008)

Amekuwa mbunge wa Kongwa kwa miaka 21 sasa (tangu mwaka 2000) na ameshika nafasi mbalimbali ndani ya kamati za bunge.

Alichaguliwa kuwa spika wa bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika.

Mbali na ubunge, amefanya kazi sehemu nyinginezo ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pori la Akiba Selous na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Januari 6, 2022 amejiuzulu nafasi ya Uspika kutokana na sababu binafsi na kwa hiari yake.

Ndugai ni mume wa Fatuma Mganga.
Ndugai sijawahi kumfagilia hajawahi kuwa na msimamo thabiti amekuwa na lugha za kejeli kwa wabunge, wananchi na hatimaye rais wa nchi. Wapinzani wake wa kisiasa amewacharaza bakora. Amehusika katika kutunga sheria kandamizi ambazo leo hii zitatumika kumuhukumu yeye.

Ndugai alikeji maneno matakatifu. "Mitaa ya Galilaya anaifamu sana huko alishatembelea sana kumuona mke wa masihi". Kishekesho kweli! Tunawashukuru malaika wa Mungu hawalali masaa 24 wako macho. Muda wote wako kazini wote. Mchimba kaburi huingia yeye mwenyewe.

Kwa wapinzani wa CCM tulieni kama Daudi vitani, hawana wa kupigana nao ingekuwa ni nyie lakini wamewafanyia hila. Wakikosa wakusozana naye watafanyiana hila wao kwa wao. "Nyamazeni kumia" tunajenga uchumi. Uchumi umeanza kujengwa bungeni kwa kuondoa wasema hovyo!

Mtikisiko upo! mafuriko yapo! Joto lipo juu! Tena lipo juu sana! Msitu bado haujashika moto lakini umekauka, majani yamekauka, miti yote imeshadondosha majani. Kaaeni kimya hivi vita siyo vya kwenu! Hivi vita ni vya kwao! Nyamazeni kimya.

Kwa mara ya kwanza ndiyo nimeona Rais muwazi mkweli! Muwazi kwa kuwa ametueleza ukweli kuhusu fedha zote alizokopa. Pia na matumizi yake amekuwa muwazi. Uwazi ni nguzo ya utawala bora. Nimeona madarasa mengi na bora yamejengwa kuliko wakati wowote katika historia ya nchi hii. Januari ya 2022 hakuna kushikana mashati kwa kuhusu kujenga madarasa bali unahitajika kufanya ukaguzi maalum kubaini waliocheza na fedha zetu. Kazi iendelee.

Mama yetu asiependa makuu mkimya na anyetumia kalamu yake vyema tunakuomba safisha kila chafu! Wale wabunge 19 feki wa Ndugai waondolewe bungeni. Hii itakujengea wewe na serikali unayoingoza heshima kubwa. Hakika hii ndiyo dhana halisi ya "Kazi Iendelee". Kichafu chochote kile kisihusishwe na serikali yako. Waache wao wafanye vitu vya aibu. Kina mama siku zote ni smart. Kazi iendelee!

Safisha sehemu zote chafu. Kesi zote za kutungwa muelekeze DPP azifute.

Mama ukikosa wapinzani nje ya CCM watotokea ndani ya CCM. Hao ni wabaya kuliko Lema na Msigwa. Wakipata watu wakuwachachafya watakimbilia majimboni mwao kusimamia maendeleo ya watu. Si unajua tena mtu akikosa kazi ya kufanya anabweteka na kuanza matusi kama ya Ndugai ya nchi kupigwa mnada!

Ruhusu mikutano ya siasa wote watatulia tuli na kukimbilia majimboni mwao kupambana na upinzani na siyo serikali. Sasa hivi wameshiba wanapambana na CCM.

Tunyamaze kimya vita hivi siyo vya kwetu. Siyo vya CCM wala CHADEMA ni vya Bwana. Mshindi wa vita hivi ni yule atakaye simama upande wa haki!

Kazi iendelee!
 
Mimi binafsi Mzanzibar asingeweza kunishinikiza alafu nijiuzuru. Ukizinngatia kazi yenyewe nimeipata kwa shida, baada ya kumdunda mtu kwa li-fimbo. Kingine huko Zanzibar kwao haturuhusiwi kudaka kazi, alafu eti aje atie maji kwenye kazi yangu huku bara!!!!
 
Lile grupu la G70 lililokuwa linadai serikali ya Tanganyika lilikuwa ni la wabunge wa CCM, na wala hawakutishwa hata na watoto wadogo wanaoitwa Vijana wa CCM kama ilivyotokea kwa Ndugai; jamaa wale walifanya hivyo wakati Nyerere akiwa hai. Jambo alilofanya Nyerere nikushawishi kuwa wazo lao halikuwa sahihi, lakini hawakutishiwa kwa namna yoyote ile kuwa watavuliwa uanachama au kuvuliwa nyadhifa zao.
Lakini mkuu usisahau group la G 55 ndilo lililomuondoa madarakani Katibu Mkuu wa CCM Horace Kolimba na Waziri Mkuu John Malecela.
Kolimba aliambiwa ameshindwa kutumia nguvu za chama alizokuwa nazo kuwadhibiti wabunge wale.
Na Malecela kama mkuu wa shughuli za serikali bungeni ameshindwa kutumia ushawishi kuvunja tishio lile la kuigawa nchi.
Nyerere alisema Muungano wa serikali mbili ni Sera ya CCM, asiyeutaka kwanza ajiondoe kwenye chama hicho.
Kwahiyo kwa mujibu wa Nyerere chama hakikutumika ipasavyo kuwadhibiti G55.

Hivyo basi, utaona namna chama kilivyo na uwezo mkubwa wa kuvuruga maguvu ya muhimili huu muhimu.
 
Ule mwingine kwani hamuoni unavyofanya madudu na matapu tapu kwa ile kesi maarufu
Hata huu unaonekana ni rahisi mno kutikiswa, tatizo ni katiba au viongozi wakuu wa hii mihimili wameshindwa kusimamia vyema katiba?

Ndugai alikuwa mlinzi wa katiba ya 1977 sasa ni mhanga kwasababu haikumlinda kama kiongozi wa mhimili. Aliishi kwa mazoea na ubabe, good riddance
Kaacha joho kaondoka mtupu ! bila heshima yoyote
Wakati wa awamu ya 5 huu muhimili ulilaumiwa sana kwa kujipendekeza kwa serikali.........huenda Job alitaka kuivunja hii ndoa haramu kati ya bunge na serikali (japo alishiriki kuiasisi) sema wana Ccm wenzake na baadhi ya wapinzani hawakumuelewa badala yake wameangalia rekodi yake ya nyuma bila kujua hata saa mbovu kuna muda inasema ukweli.

Kwa wadau wa demokrasia hili tukio ni hatari kwa ustawi wa nchi yetu.
 
Jamaa muoga sana. Angeendelea kupambana tu.

Lakini sio mbaya maana ana kinga tayar.
 
Uzuri wa Tanzania ni pamoja na maajabu ya Historia inayotengenezwa/kutokea kila iitwapo leo.
Ingawa kuna wakati Historia hizo uambatana na majonzi kwa watu na pengine misiba.
Ninawapa pole wale wote waliopoteza ndugu, jamaa na rafiki kwenye ajali ya Boti kisiwani Pemba na ile ajali ya watu kugongwa na Loli Newala Mtwara.
Mwenyezi Mungu azilaze Mahala pema roho zao
Amina.
 
Nampongeza Ndugai kwa kujiuzulu.Rais Mwinyi aliwahi kujiuzulu na baadae akawa Rais.
Hoja ni kuwa wale wahuni na Chawa kamwe wasipewe nafasi.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Tunaendelea kufukiza kuni mbichi kwenye pango!!!
 
IMG_0216.jpg
 
Nampongeza Ndugai kwa kujiuzulu.Rais Mwinyi aliwahi kujiuzulu na baadae akawa Rais.
Hoja ni kuwa wale wahuni na Chawa kamwe wasipewe nafasi.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
Kwahiyo supika naye atakuwa rais blaza?
 
Back
Top Bottom