Spika Ndugai aomba radhi Wakristo kwa kauli yake kuhusu Yesu

Spika Ndugai aomba radhi Wakristo kwa kauli yake kuhusu Yesu

Nilisema humu kuwa wakikusanya hotuba zake zote hachomoki.
Wakati anaanza alijifanya haogopi kitu, baada ya kusikia mikwara akaanza kulegeza kauri. Zile hotuba zake za mwanzo ndizo wamembana nazo hadi akapatikana na hatia.

Ashauriwe.
 
Kumbe anasoma mitandao ya kijamii mbona hajirekebishi mapungufu yake.
Mfano.....kumkumbatia mzee Halima and co.
Kutomlipa Lisu stahiki zake.
Kumfukuza Lissu bungeni wakati Kuna yule mbunge tajiri wa Kanda maalum ambaye hakuhudhuria bungeni kwa zaidi ya miaka mitatu.
Kumuogopa Mbowe wakati Mbowe Ni mtu wa kawaida sana.
Kutokua na confidence.
 
unasubiri itokee kama mumeo askofu Rashidi alivyosema watu watakua mazombi?
Na wewe kama umedunga J&J kuwa makini kila siku ukiamka asubuhi kajiangalie kwenye kioo jinsi unavyoanza kuwa na sura ya zombi kidogo kidogo!😀😀😀
 
Acheni kutafuta ujiko kirahisi rahisi. Akuombe msamaha kwani amekukosea nini? Kukosea ni jambo la kawaida. Isitoshe, kisheria, anaypaswa kuomba msamaha ni Yesu kama atakuwa ameudhika. Pia, fahamu. Yesu alipoondoka alicha wanafunzi na si wakristo jina ambalo liliundwa na maadui zake kwa kejeli wakimaanisha wale walioanza kufuata mafundisho yake sawa na walutheran na luther au wahutterite na Jacob Hutter wamennonite na Menno Simmons etc.
Sema tu ni kwa kuwa wakristo huwa hawapendi kukuza mambo na pia dini huwa inasisitiza sana upendo na kusamehe. Lakini kama angekuwa amesema jambo linalokwenda kinyume kwa kiongozi wa ule upande mwingine (Muddy) ungeona reaction za kila aina na pengine angejitokeza HAMZA mwingine huko bungeni.
 
Uko
Nimeona taarifa ya Bunge kuwa Ndugai anatuomba radhi Wakristo. Kusema Yesu ana mke hayo ni maneno ya Mpinga Kristo kwa mujibu wa imani yangu.

Kwanini Ndugai atume mtu aniombe radhi wakati amemdhalilisha Bwana wangu Yesu Kristo na kumnenea uongo?

Ndugai ameshindwa nini kuja kwenye vyombo vya habari yeye mwenyewe au kutumia njia ilele aliyonikwaza kuniomba radhi?

Mimi naona amenidharau na dini yangu na Bwana wangu. Sijamsamehe
Umesema sawasawa kabisa
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amewaomba radhi wakristu kwa kauli aliyotoa leo bungeni alipokuwa akielezea alivyotembelea Israel

Katika maelezo yake alisema "Yesu alitembea na mke wake kutoka Nazareti kwenda Yerusalemu kuhesabiwa" ambapo amesema alimaanisha Yusufu alitembea na mke wake sio Yesu kama alivyotamka

Amesema kilichotokea ni kosa la kibinadamu. Alivyokuwa anaeleza kuwa anaufahamu ukristo vizuri na kuwa amewahi kuhiji maeneo matakatifu

View attachment 1918431
View attachment 1918433
Aombe radhi tena maana walitoka Nazareth kwenda Bethlehem na sio kwenda Jerusalem!
 
  • Kicheko
Reactions: Ame
Kukosea ni kawaida tu.
Ujue wanapingana na Mungu, Mungu wetu hataki watanzania tuangamie, na huyo huyo ndugai kipindi cha Magufuli alishabikia chanjo mbaya leo unajadili na kusema eti kusema chanjo ni mbaya ni makosa??? Na bado, adhabu ya Mungu yaja, maana Yesu ni Mungu, huwezi kutoa kauli kama hiyo kama bila kudhamiria, ni kafanya makusudi. Luckily Yesu huwa anajitetea, ila ingekuwa Mohammed nadhani fatwa zingekuwa zimetangazwa
 
Sema tu ni kwa kuwa wakristo huwa hawapendi kukuza mambo na pia dini huwa inasisitiza sana upendo na kusamehe. Lakini kama angekuwa amesema jambo linalokwenda kinyume kwa kiongozi wa ule upande mwingine (Muddy) ungeona reaction za kila aina na pengine angejitokeza HAMZA mwingine huko bungeni.
Nakubaliana nawe. Upande wa pili una malezi mabaya yaliyojengwa kwenye jazba badala ya fikra, visasi badala ya msamaha. Ila mie huwa sijali upande. Hata ilipotokea kashfa ya Rushdie, ingekuwa leo, ningewashauri wamwache aliyetukanwa alalamike ila si wao. Mwanangu nakubaliana nawe. Mtu anatukanwa baba au mama yake halalamiki. Ila akitukaniwa mtume eti yuko tayari kuua wakati jamaa mwenyewe wala hakumuona. Hii akili au uchizi?
 
Naaam
Ila bado kakosea...kiimani Yosefu hakuwa mume wa Bikira Maria...
Alikuwa mchumba wake...
Kwahiyo Kuna Radhi nyingine tunaisubiria🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️
Kachemsha tena...hakuna popote kwenye maandiko waliyosema Yosefu alikuwa mume wa Maria.
 
Aombe radhi tena maana walitoka Nazareth kwenda Bethlehem na sio kwenda Jerusalem!
Sasa naanza kupata picha kwa nini akiendesha vikao vya bunge huwa na vitabu lukuki pale mezani kwake. MEMORY LOW!
 
Nimeona taarifa ya Bunge kuwa Ndugai anatuomba radhi Wakristo. Kusema Yesu ana mke hayo ni maneno ya Mpinga Kristo kwa mujibu wa imani yangu.

Kwanini Ndugai atume mtu aniombe radhi wakati amemdhalilisha Bwana wangu Yesu Kristo na kumnenea uongo?

Ndugai ameshindwa nini kuja kwenye vyombo vya habari yeye mwenyewe au kutumia njia ilele aliyonikwaza kuniomba radhi?

Mimi naona amenidharau na dini yangu na Bwana wangu. Sijamsamehe

Mathayo 5 : 44 Lkn mimi nawaambia wapendeni adui zenu waombeeni wanaowaudhi
 
Sentesi ya mwisho imeharibu kila kitu. Nadhani kuna haja ya kujifunza kuandika. Huwezi kumuomba radhi mtu wakati huohuo unamkumbusha kuwa naye ana makosa, ni kitu cha kawaida[emoji24]. Halafu Carperinaum siyo Kijiji cha Yesu. Chake ni Nazareth
 
Huyo Job Nadhani Anayatafuta Yaliyompata Anania Na Safira
 
Hata asingeomba msamaha hii spika mbovu inakinga hata ingekuwaje.
Ila kule mkoka kongwa kunajamaa anaitwa yesu ndio alikuwa anamzungumzia.
 
Sasa naanza kupata picha kwa nini akiendesha vikao vya bunge huwa na vitabu lukuki pale mezani kwake. MEMORY LOW!
Kuna sheria hupitishwa akiwa kitini lakini amelala, akiamka anaanza kushangaa ilipitaje na yeye alikuwepo?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom