Spika Ndugai: Asiyetaka tozo ya kizalendo atupe njia mbadala ya kupata fedha



Huyo atakuwa hajitambui kidogo!!, sasa atuambie baada ya 2025, kodi hiyo itasitishwa??!!---- yaani Bunge litapelekewa Muswada wa kufuta hiyo kodi???
 
Huo mjadala unaosema haumhusu Ndugai na majibu yake ya shombo? Yaani watanzania wanaolalamika anawaona wajinga ila yeye na genge lake wanaolishwa bure kwa kodi zetu. Yeye analipa nini huyo Pimbi zaidi ya kula na kuvishwa majoho bure? Kodi inakatwa kwa anayetuma tuseme ana uwezo sawa, inakatwa kwa anayetumiwa maskini yuko kijijini Msoga halafu anajitokeza pimbi asiyejua fedha inapatikanaje anajibu watu utumbo?
 
Huyu wimbi hili litaondoka nae, kavimbiwa pesa zetu
 
Hizo za mikononi, Magufuri aliwambia angalau walipe elfu 20 mkaanza kubeza kuwa Magufuri mwizi,kisa kawambia machinga kulipa elfu 20,acha watukomeshe maana Watanzania atujui tunaitaji kuongozwa na Mtu yupi
 
Tozo ya miamala ni sahihi
Ila ongezea
Parking fee ya Toyo na bajaji
Hawa jamaa wamejaza Parking mjini na ndio wanufaika wa awamu hizi za 5 na 6
Wamachinga vitambulisho vyao viwe 50000
Kila mtu aliyeko mjini anatafuta pesa achangie kitu kwenye kukuza uchumi
 
Huyu anaweza kuwa alichaguliwa kutimiza diversity quota ya watu 'wafupi' bungeni kama ilivokuwa kwa viti maalum...Huwezi kutoa kauli kama hii...


Mniwie radhi ndugu zangu wenye 'low center of gravity' kama nimewakwaza.
 
Huduma za fedha kwa njia ya mitandao ya simu badala ya kuboreshwa ili serikali izidi kupata mapata makubwa kwa kushawishi wananchi wengi zaidi kuitumia kwani kodi yake haina chenga, wana-discourage huduma hii kwa maksudi! Kwa kiwango cha tuzo anayotetea mbunge huyu, watu watarudi kwenye mifumo ya awali (cash itashika hatamu) watakosa hata kodi ilokuwa ikipatikana kabla ya tozo mpya.

Wakati umefika hawa watunga sheria, n.k. nao walipe kodi zote pasiwe na double standard. Ukitaka wananchi kuwa na uzalendo, viongozi wanapaswa kuonesha mfano wa kile wanachokihubiri.

Nchi hii inautajiri mkubwa sana, madini, ardhi, maji, n.k. Mfano kupitia kilimo; tumezungukwa na vyanzo vikubwa vya maji lakini tunalima kwa kutegemea mvua ya mwenyenzi badala ya umwagiliaji. Utawakuta viongozi (watu wazima, wasomi, n.k)wamekalia kuwazuia wakulima kuuza mazao yao nje ya nchi kwa kisingizio eti watapata njaa badala ya kuitumia hii kama fursa ya wanachi walowengi kupata ajira na nchi kujipatia fedha za kigeni kwa kuwaboreshea miundo mbinu, n.k.
 
Wao huko serikalini wanaishi maisha mazuri ya kifahari wao na familia zao, kila kuzuri kuzuri wanalala wao, kutibiwa kuzuri wanatibiwa wao, kula kuzuri wanakula wao, shule nzuri kwa watoto wao Wana soma wao, hata maziko mazuri wanapata wao,!

Sisi ndio tumekua watwana wao, kutafuta tufute sisi wao ndio watumie, wao ndio watupangie.

Mimi nawatakia yote, ila mwenyezi Mungu siku zote humkumbuka Alie mnyonge na humwokoa katika Shari zote, iwapo Kuna maisha baada ya haya Basi ni watakie hao wanaotupangia yote yalio mema!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazo jemaa KABISA kuchangia nchi yangu na maendeleo yake
wakati muafaka Kama wananchi tusikomae tu iondoelewr

TUTOE ushauri nn kifanyike seerikali iendelee kupata pesa za KUFANYA maendeleo ya NCHI yetu

nimeona dini zilizoea Kupitisha.mizigo bila Kodi leohii zinalipa...

Hili la wabunge kulipa.kodi.nalo n wazo jemaa pia na ikiwezekana kuwe na punguzo ktk posho wanazopata KUSAIDIA kuendeleza maendeleo ya NCHI yetu

kingine serkl ingekaa wakubaliane kiasi KIDOGo kaama n 200 ama 500 kilamhamala si mbaya huku kampuni zikiendelea kulipa kodizao kama kawaida....mwananchi atajisikia amechangia nchi yake..

kuwe na costant amount ushauri 200-500 KIla.mhamala SI.mbaya isiangalie kiasi anachotuma mtu...

nawatakia mjadala mwema nikisubiri wabunge nao wapewe hiihoja kujadili MBADALA wa hii tozo

kulipa mtalipa nchi iendee tuombee majadiliano mema

Mungu ibariki Tanzania

#VAAABARAKOA
#NAWAMIKONO
#COVID
#INAUA
 
Wab hamna mbadala na ndio mnapitisha sheria

wananchi wanatoa Wapi wanze wao kuonyesha uzalendo kwa waliowatuma
 
Magari ya serikali kuwe na ukomo wa bei,mwisho iwe 150 hili ndilo gari atumie kiongozi wa juu.

Wengine watumie hata hardtop na Prado.Tunaishi kwa anasa huku tunategemea tozo kwenye simu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…