Spika Ndugai: Gwajima akirudia tutamuita Waziri wa Mambo ya Ndani na kumhoji

Spika Ndugai: Gwajima akirudia tutamuita Waziri wa Mambo ya Ndani na kumhoji

Spika Job Ndugai amesema vyombo vingine vya serikali na chama vinapaswa kumuwajibisha Josephat Gwajima kutokana na kauli zake

Amesema kama hatowajibiswa na akarudia makosa aliyokutwa nayo kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge watalazimika kuitwa wao

Amesema Waziri wa Mambo ya Ndani atapaswa kuhojiwa na Kamati ya Maadili endapo makosa hayo yatajirudia
Yeye atahojiwa na nani kwa kukandamiza haki za wananchi kuona bunge Live?
 
Wataalam wa maswala ya kibunge na taratibu zake hebu toeni ufafanuzi.

Kwamba Askofu akirudia kosa Waziri ataitwa kwenye kamati ahojiwe Kwa msingi upi? Kosa la Gwajima ila anaehojiwa ni waziri? Hii imekaa vipi wadau!?

Sent from my BLA-L29 using JamiiForums mobile app
Waziri ndio ana mapolisi (IGP) wanajua kuna jinai wamekaa kimya!!!... Waziri wa Afya katoa taarifa Mchungaji akamatwe ahojiwe (Waziri na polisi wake kimya Hadi Bunge limeamua kuchukua hatua)
 
Spika Job Ndugai amesema vyombo vingine vya serikali na chama vinapaswa kumuwajibisha Josephat Gwajima kutokana na kauli zake

Amesema kama hatowajibiswa na akarudia makosa aliyokutwa nayo kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge watalazimika kuitwa wao

Amesema Waziri wa Mambo ya Ndani atapaswa kuhojiwa na Kamati ya Maadili endapo makosa hayo yatajirudia
Imetoka iyo.. Wamemshindwa....!

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
 
Yani leo nimepata hasira,,katika mambo yote yanayosumbua wananchi ,mmepata mda wa kumjadiili Gwajima🤨.
WTH!
Bunge la hovyo kabisa hili. Matatizo yooooooooooooooooooooooooooote ya watanzania with regard to Bunge wameona la Gwajima ndilo pressing. Stpid!
 
ktk mawaziri ambao wamekuwa wapole kupita maelezo ni Waziri wa mambo ya ndani.
Waziri amekuwa mpole sana, amekuwa mzito sana kutoa makemeo na makaripio.
kuna kauli nyingi sana zinatolewa ambazo zinaashiria uvunjifu wa amani na kauli hizo zinatolewa na baadhi ya viongozi tena wa dini!!!
Waziri wa Mambo ya ndani afahamu kuwa amebeba dhamana ya Amani na Usalama wa Wananchi wote wa Tz, hayupo hapo kuwachekea wavunjifu wa amani.
Tunamtaka Waziri wetu abadilike.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenda kule, embu orodhesha hizo kauli unazotaka jeshi likamate watu?? Au unamaanisha kauli za Hamza?!
 
Kwenda kule, embu orodhesha hizo kauli unazotaka jeshi likamate watu?? Au unamaanisha kauli za Hamza?!
CHADEMA ni kichaka cha wahalifu wa aina zote;
magaidi, majambazi, wauza madawa, wote wamejificha ktk chama cha chadema.
 
Kidogo na mi nashangazwa, kuna waziri alisema IGP amkamate Gwaji. IGP akasema hakuna jinai hapo.
Sasa Spika nae ameagiza ashughulikiwe, vinginevyo Waziri husika ataitwa!
Kuna ka-element ka kulindana, mbona posho hata TL walimnyima alikuwa na kosa gani? Na aliitwa lini bungeni kujitetea kabla ya hukumu, kama walivyofanyiwa Gwaji na Jeri?

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Only God knows what would happen huyu Gwajiboy angekuwa mpinzani
 
Spika ndungai na wajumb wa kamati husika ni CCM tupu.

Hakuna CHADEMA kwenye hayo maamuzi yaliyofanyika kwa huyo kibwetere wenu.

Hili mtamalizana nyie mataga pori wenyewe kwa wenyewe huko Lumumba na Bungeni, msiwahamishie CHADEMA matatizo yenu.
CHADEMA wanatamani Gwajima afukuzwe wapate mgombea maana kwa Sasa hoi kabisa.
 
Spika ndungai na wajumbe wa kamati husika ni CCM tupu.

Hakuna CHADEMA kwenye hayo maamuzi yaliyofanyika kwa huyo kibwetere wenu.

Hili mtamalizana nyie mataga pori wenyewe kwa wenyewe huko Lumumba na Bungeni, msiwahamishie CHADEMA matatizo yenu.
Nyinyi ni Chadema jina,fikra na matendo yenu yote ni kama Fisiemu.

Tena awamu hii ndo mmedhihirisha kabisa nyi ni CCM-B so msitumie nguvu kubishana na watu ambao wameamua kutofungamana na huo ulaghai wenu wa vyama vya siasa
 
Wewe wasema lkn sisi tunafahamiana humu kulingana na misimamo yetu. Kama wewe ni sukuma gang au sijui gwajiboy hayo ni yako.
 
Back
Top Bottom