Spika Ndugai: Lissu kwa miaka 10 ya Ubunge hakuna 'legacy' yoyote aliyoacha Jimboni kwake

Spika Ndugai: Lissu kwa miaka 10 ya Ubunge hakuna 'legacy' yoyote aliyoacha Jimboni kwake

Nchi hii utadhani hawajui nini, kilichokuwa kinaendelea na mambo ambayo yamekuwa yakifanywa kwa makusudi na chama tawala kwa miaka nenda miaka rudi. Majimbo ya wapinzani yalikuwa yakinyimwa kwa makusudi maendeleo ili waonekane hawafai kwa wapiga kura wao. Miaka ya nyuma hujuma hizi ambazo ninaweza kusema ni za kijinga zilikuwa zinafanyika kimya kimya, ila Rais (Hayati Magufuli) alishindwa kufanya hivyo kwa kificho.

Ni nani ambaye hakusikia chama tawala kupitia mgombe wao yaani Rais Magufuli, kikisema kuwa maendeleo kwenye majimbo ya wapinzani yapo nyuma kwa kuwa wamekosea kuchagua, hivyo serikali haiwezi kupeleka maendeleo sehemu ambayo imekikataa chama tawala. kauli kama hizo zilikuwa zikijirudia na zitaendelea kujirudia maana tuna tabaka kubwa ambalo hawewezi kuhoji na pengine hawana utambuzi wa majukumu ya serikali na yale ya mbuge. kusema Mbuge hajafanya lolote wakati alikuwa akiomba mara kwa mara kupewa miradi ya maendeleo bila mafanikio huo ni ujuha wa hali ya juu.

Siasa hizi za kipuuzi ndio zinazoturudisha nyuma kimaendeleo na kwa miaka mingi tutazidi kuwaona mataifa mengine yakipiga hatua kubwa za maendeleo huku sisi tukitopea kwenye siasa za kijinga jinga zisizokuwa na tija yoyote. Vyama vya upinzani visichukuliwe kama maadui, japo navyo vinamapungufu yake ila vina mengi mazuri yeneye kuweza kuleta mchango mkubwa wa kimaendeleo.
Tukiendelea na siasa hizi za kijuha tunajiletea madhara juu yetu na vizazi vyetu tutakosa jambo jema la kuwaachia.
 
Hapo kwa Spika wa bunge, debe buku.
Sijui ni nani spika
Screenshot_20210511-110253.jpg
 
Wakaxi wa Jimbo la KONDWA Mkoani Dodoma wakichota maji kwenye Bomba la kisasa lililozinduliwa naMbunge wao Ndugai ,hivyo kuunga mkono uchumi wa kati.

FB_IMG_1620883433830.jpg
 
Hivi ni Lissu anapeleka Maji au serikali? Kwa sababu Lissu kazi yake ilikua kusemea hilo swala kwahio walitaka Lissu atoe hela zake apeleke maji kule ..Ndugai Jinga kweli
 
Hivi huyu mtu huwa anajiuliza yeye amecha legacy gani ktk;
Bunge
Jimbo lake
familia yake?
namshauri kufunga na kuomba hekima na busara kwani uelekeo alio nao ni mbovu sana.
Ana bahati kwamba nafasi ya uSPika inampa hadhi ya kujadiliwa. Vinginevyo, huyu ni kielelezo cha aibu iliyoletwa na mwendazake katika taasisi muhimu za taifa hili. Watu aliowapa nyadhfa za kuongoza taasisi kuu za taifa wengi ni fyatu na wasio na haya kudhihirisha ujinga wao hadharani. Hata wanaohangaika kuitetea "legacy" nao ni hivyo hivyo. Hawana mantiki kabisa. Ni propaganda uchwara tu. Lissu apeleke maji kijijini? Utter stupidity.

Mwendazake alitumia nguvu za dola kufuta upinzani bungeni, bila kujua kuwa watu aliowajaza bungeni ni wale waliozoea kupata ujiko kwa kuwapayukia na kuwanyanyasa wabunge wa upinzani. Sasa wanahangaika kufuatilia twitter, youtube, facebook, n.k. kusikiliza wapinzani huko nje wanasemaje na kuifanya sehemu kubwa na muhimu ya mijadala ya bunge! Mbunge anaongea kidogo kuhusu hoja ya wizara iliyoko mezani halafu anatumia muda mwingi kwenye kumkashifu Mbowe, Lissu au Lema huku akichagizwa na mipasho ya Spika. Very desperate and pathetic!
 
Leo kwenye mjadala wa kupitisha bajeti ya wizara ya maji, spika Ndugai amesema kwa masikitiko makubwa kuwa licha ya Tundu Lissu kuwa mbunge wa Ikungi kwa miaka 10 lakini hakuna alichofanya cha kukumbukwa na wananchi!

Ndugai amesema hata kijiji anachotoka Lisu hakuweza kuwapelekea maji kwa miaka kumi!



My take
Nguvu aliyoitumia Lissu mzee wa MIGA kutetea Acacia angeielekeza kutetea wananchi wa jimbo lake wangefika mbali sana kwa miaka 10.

Inasikitisha sana wananchi hawana maji alafu yeye anatetea wezi wa madini !!!
Kaangalie Kongwa alafu kulinganisha
 
Mbona mbowe,Sugu, msigwa, mdee walipelekea maji majimbo yao?
Sikatai kuwa kuna maeneo ambayo wapinzani walifanya vizuri, ila nimejaribu kuonyesha kuwa kukosekana maendeleo kwenye majimbo mengi ya wapinzani, kumetokana na juhudi za makusudi za serikali kupitia chama tawala ili kuwakomoa wabunge wa upinzani. ukikataa hoja hii basi pengine umekuwa si mfuatialiji mzuri wa siasa za Nchi hii au kwa makusudi umeamua kukataa tu.

Swali kwanini Mbowe, Sugu, Mdee walipeleka maji naweza kulifananisha na swali kwanini mkoloni alijenga reli Dar es Salaam, tabora hadi kigoma na sio kwingine, jibu ni kwa sababu alikuwa na maslahi binafsi, mfano jimboni kwa Mdee ndipo bomba kubwa la maji kutoka Ruvu upita kwa mantiki hiyo jimbo la Kawe lingekosa vipi maji? maji lazima yalikuwa yapite hapo kwenda majimbo mengine huu ni mfano mdogo tu kuonyesha kwanini wengine walipata na wengine walikosa, nimetumia jimbo la kawe kwa kuwa naijua geografia yake kidogo.

Tulikosea, kukosea sio kosa kama tutatumia makosa yetu kujifunza na kuhakikisha njia tutakayochagua ni njema isiyo na maigizo, vibweka visivyo na maana. Nimalizie kwa kusema Siasa za vyama vingi sio ugomvi, pia jitihada zetu ziwe za kujenga Nchi imara na sio kukwamishana, ukimkwamisha Mbuge wa upinzani kwa makusudi haumkomoi yeye bali wakina sie na Nchi kwa ujumla.
 
Spika jirekebishe binafsi. Hao watu unao wasimanga kila siku, mbowe na lissu lazima ukubari kuwa Wana wafuasi wengi, kwa hiyo kila siku utaishia kutukanwa na kudhalilishwa bila sababu. Waache
 
Leo kwenye mjadala wa kupitisha bajeti ya wizara ya maji, spika Ndugai amesema kwa masikitiko makubwa kuwa licha ya Tundu Lissu kuwa mbunge wa Ikungi kwa miaka 10 lakini hakuna alichofanya cha kukumbukwa na wananchi!

Ndugai amesema hata kijiji anachotoka Lisu hakuweza kuwapelekea maji kwa miaka kumi!



My take
Nguvu aliyoitumia Lissu mzee wa MIGA kutetea Acacia angeielekeza kutetea wananchi wa jimbo lake wangefika mbali sana kwa miaka 10.

Inasikitisha sana wananchi hawana maji alafu yeye anatetea wezi wa madini !!!
Inasikitisha sana hii
 
Jamaa kashadata!! Mnara hausomi... Kuna muda dawa hizi huwa zinaanza kugoma sasa ukishaona hivi basi safari ya mavumbini huwa i mbioni..ni muda wa maombi yetu kwake ili aongezewe siku hamna namna nyingine kwa kweli
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom