Spika Ndugai: Miradi yote aliyoacha Rais Magufuli iko salama

Spika Ndugai: Miradi yote aliyoacha Rais Magufuli iko salama

Mitano tena ......hakuna kutuvusha !!! Tuliambiwa vitabu vitakatifu amtegemeaye binadamu......
 
Aongezewe muda
Aongezewe muda
Wewe panga, Mungu hupangua
 
Leo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai wakati akitoa salamu za pole kufutia kifo cha Rais Magufuli, amewataka watanzania kuwa watulivu na kusema ilani ya CCM ya 2020 - 2025 na miradi yote ya maendeleo aliyoacha Rais Magufuli itatekelezwa kwani fedha zote za miradi hiyo zilikuwa zinapitishwa na Bunge.

Amewataka wabunge ambao kupitia kamati mbalimbali sasa hivi wako wanatembelea miradi hiyo kuwa watulivu.

=======

SPIKA NDUGAI: Ikumbukwe kwamba mheshimiwa Rais kwa nafasi yake ni sehemu ya pili ya Mhimili wa Bunge kwahiyo ni mdau wetu muhimu sana katika uendeshaji wa Bunge na shughuli za Bunge kwa ujumla wake kwahiyo tumepata pigo kubwa sana.

Natoa pole nyingi kwa mheshimiwa makamu wa Rais, mama Samia Suluhu, viongozi wa serikali, kipekee tunatoa pole nyingi sana kwa mama Janeth Magufuli, familia ya mheshimiwa Rais wetu lakini kikubwa zaidi kwa watanzania wote popote pale walipo.

Kama mnavyofahamu ndugu waandishi, waheshimiwa wabunge walikuwa katika ziara za kukagua miradi ya maendeleo kutokana na utekelezaji wa bajeti inayoendelea ambayo inaishia tarehe 30 June mwaka huu.

Imebidi tutoe wito na maelekezo kwamba, sasa wabunge wote waliokuwa katika waliokuwa katika ziara hizo za ukaguzi wa maendeleo warudi Dodoma haraka sana.

Kwahiyo wabunge wako njiani kutoka sehemu mbalimbali za nchi kurudi hapa Dodoma.

Kama tunavyojua, mheshimiwa Magugufuli ana mambo ambayo alijipambanua mapema, ni mengi sana lakini kwa kifupi alikuwa ndio Rais mjenga nchi hasa katika eneo la miundombinu. Miundombinu ya barabara, reli, bandari, shirika letu la ndege, ujenzi wa viwanja vya ndege, miradi mikubwa mikubwa ya maji, miundombinu ya elimu, eneo la afya. Sijui ni eneo gani utaweza kusema kwamba mheshimiwa Rais ameweka kumbukumbu ya aina yake.

Kwahiyo tunayo kazi kuwa sana sisi Watanzania ya kuhakikisha kwamba tunaendeleza nngwe ambayo amekwisha kuiweka ili kuhakikisha kwamba kazi zote alizokuwa akizisimamia ikiwemo ya utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-25 na kwa mambo mbalimbali ambayo aliyaainisha kupitia hotuba ambazo alizitoa hapa bungeni yeye mwenyewe tunaendelea kuzisimamia kwa faida kubwa zaidi ya Mtanzania.
Bajeti kupitishwa na bunge ni kitu tofauti na upatikanaji wa pesa na utashi wa kisiasa kuendelea miradi yote hiyo kwa wakati mmoja, ndugai asipotoshe umma

Sent from my itel A32F using JamiiForums mobile app
 
Hili bunge la kuteuliwa livunjwe tu tuanze upya
Mama Samia ili afanikiwe afuate ya Tshikedi Kongo na ubia wa Kabila

Atumie mbinu ya kuondoa vinasaba viovu kwa kudeel na Supika Ndugei kama Kongo
Hapo ataweza kuendesha nchi atambue kuna nileteeni Gwajimaaa!!? Ukweli atamsumbua sana Mh Raisi
Jingine sasa mtaona usumbufu wa Mashehe kwa muislamu mwenzao
 
Mbona tuliambiwa tumuongezee na muda kwamba bila yeye hakuna wa kutuvusha ?
Mungu amelipigania taifa, na kuonesha kila mtu anaweza kutuvusha. Na Taifa Lina hazina ya viongozi kibao, tuachane na wachumia tumbo ambao walitaka aongezewe mda kwa sababu ya kujijengea vitambi. Tuendelee kuomba ili wachumia tumbo waendelee kupigwa mapigo Kama ya farao
 
Katika kumuenzi Rais wetu kipenzi Marehemu Dr John Pombe Magufuli ni vyema kuweka mpango wa haraka wa kukamilisha miradi iliyoanzishwa katika awamu hii.
Ieleweke vyema kuwa mama Samia Suluhu alikuwa ni Mgombea mwenza wa Magufuli hivyo ahadi yake kwa wananchi ipo pale pale.
utekelezaji wa Ilani ni lazima.

1-Mradi wa umeme wa mwalimu nyerere

2- Mradi wa reli ya SGR

3- Miradi ya madarasa na vituo vya afya

4. Ujenzi wa Ikulu ya Dodoma

5-........Orodha itaendelea
 
Yan hapo cha mhimu ni madarasa na vituo vya Afya pamoja na bwawa la umeme , na madaraja ya kuvuka maji... labda pia na miradi ya barabara mengine ni nonsense Kwa sasa may be yaende Kwa awamu sana
 
Back
Top Bottom