Spika Ndugai: Nampa onyo kali Jenerali Ulimwengu kuchunga ulimi wake, haipendezi mtu wa umri wake kuwa anaongea ovyo ovyo

Spika Ndugai: Nampa onyo kali Jenerali Ulimwengu kuchunga ulimi wake, haipendezi mtu wa umri wake kuwa anaongea ovyo ovyo

Bunge lenyewe linajidharaulisha! Wabunge wenyewe wanalidharau... Serikali inalidharau...
Wananchi wanalidharau...!!
 
Aache upupu basi, ukweli ndo hawautaki hawa jamaa ni watu wa ajabu sana
 
Ametoa onyo hilo leo Mjini Dodoma na amemtaka Ulimwengu kuacha mara moja kutoa lugha za dharau dhidi ya Mhimili wa bunge .

Bali hakusema ni hatua gani atachukua ikiwa Jenerali Ulimwengu atakaidi onyo hilo , ila anasema watapambana naye ndani na nje .
Hivi huyo mtu anajiona kama nani haswa hapa dodoma?

Huyo rais wa nchi tu hawatishi wananchi.
 
Wananchi wangapi au wewe na nani lete takwimu,acha mara moja hili jina la Imhotep

Yule alikuwa genius,siyo
Huyo Spika anahusika katika kuwarubuni na kuwatisha Wabunge wa Upinzani wakubali rushwa ili wahamie CCM, huyo Spika anayekwenda kinyume na Sheria na Katiba kwa kuruhusu Wabunge wasiokuwa na Vyama wakae Bungeni.

Hilo Bunge litaheshimiwa na nani?
 
Ila bunge linadharaulika sana

Hebu tuliheshimu bunge wazee

Ova
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai amempa onyo kali Mwanazuoni Jenerali Ulimwengu kutokana na alichokiita tabia yake ya kukashifu Watu mitandaoni.

Akizungumza katikati ya mjadala wa marekebisho ya Sheria mbalimbali uliowasilishwa Bungeni, Spika Ndugai amesema Ulimwengu ambaye ni Mwandishi wa Habari Nguli amekuwa akilikashfu Bunge na Spika apendavyo.

"Jenerali amekuwa akilivunjia heshima Bunge na Spika pia, napenda kumpa onyo kali kuchunga ulimi wake, haipendezi Mtu wa umri wake kuwa anaongea ovyoovyo, akiendelea na sisi tutaacha ukimya itabidi Watu washughulike nae ndani na nje yaani Mahakamani, habari imfikie uvumilivu wetu umefika mwisho, sisi sio kama anavyodhani" ——— Spika Ndugai
Hana ajuwalo msameheni huyo maradhi yanamsumbua
 
Ndugai ana chukia kuambiwa ukweli kuwa bunge ni dhaifu na hakuna cha maana wafanyacho zaidi ya kuridhia kila kiletwacho na serikali.
Jenerali ametonesha donda la Prof Assad.
Kapiga melemle kwenye mshono
 
Back
Top Bottom