Spika Ndugai: Nitawalinda wabunge wa Viti Maalumu CHADEMA kwa nguvu zote, Mnyika akajifunze kwa Dkt. Bashiru kazi za Katibu Mkuu

Spika Ndugai: Nitawalinda wabunge wa Viti Maalumu CHADEMA kwa nguvu zote, Mnyika akajifunze kwa Dkt. Bashiru kazi za Katibu Mkuu

Nacho zote omba omba duniani zine mtindo wa siasa unao fanana.
Hapa ndo utajua law nini ni maskini na tegemezi. Tanzania,Uganda,Congo, C.A.R, BUKINAFASO,BAGLADESH,IV COAST,Zimbabwe,Burundi...sudan.... zote zinafanana kisiasa
Ulipoamrishwa kuandamana kushinikiza marudio ya Uchaguzi ulijitokeza? Wacha wenye chama wakiokoe chama chao(ruzuku),kwa njia itakayowapendeza.Nafasi yako uliokuwa nayo ni kuandamana, na haukufanya hivuo.

👉Kwahiyo acha kujifanya una uchungu Sana, kelele zako nyuma ya keyboard hazina mashiko yoyote.
 
Haahaa halima ameanza kuwa mbunge wake Jana? Mkuu tuache unafiki
Saisa sio nyepesi kihivyo mkuu, siku niliyowakuta Mdee na Gwajiboy wakinywa soda pamoja ndo niliamini hivyo. Kwahiyo kwa akili zako Mdee na Halima wameanza kulink up jana eeh? Haya mkuu[emoji23]
 
Kama Mungu yupo ,hakika atabaki kuwa Mungu!!!. Kwani hafananishwi na awaye yote hasa uwezo wake wa kuvumulia hata upuuzi na unafiki wetu.

Ningekua mm ndiye God ...Kuna ujinga flani nisingeuvumilia. Unautenda nakuhaibisha on the spot uli upate adabu na ukiungama nakusamehe maisha yanaendelea.

Ila kwa situation hii ... tutaendelea kuchezeana sana
 
Spika Ndugai amesema kanuni za bunge zinamtaka kuwalinda wabunge walio wachache na maslahi yao naye atafanya hivyo kwa nguvu zake zote.

Ndugai amesema wabunge 19 wa CHADEMA wameteuliwa kihalali na kama CHADEMA wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu na kuwafokea kupitia vyombo vya habari.

Spika Ndugai amesisitiza kuwa Mnyika bado hajakomaa kisiasa hivyo amemshauri aende kwa Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru akafundishwe namna Katibu mkuu anavyopaswa kutenda kazi zake kwa ufanisi.

Chanzo: TBC Aridhio

Maendeleo hayana vyama!

NOTE: Ilishadokezwa tangu juzi kuwa Ndugai ana mkakati huo > Ofisi ya Spika ‘kuwalinda’ wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA - Imevuja!

Tatizo naliona tz kwa macho ya kiroho zaidi,
Kila mtu kutaka ugangwe, kwa nafasi aliyonayo, na ndo shida kubwa kwa Sasa tz inaota mizizi
Let me be clear, ukatae au ukubali,tz hakuna aliejuu ya TAIFA iwe leo ,kesho au kesho kutwa,tuwe hai ,au tusiwe hai,
Mzee wa upako ,niliwai ona clip yake akionya,kwamba akiwambia watu msifanye hivi,mtaleta tabu katika TAIFA ikiwa ni pamoja na machafuko,mnasema amekunywa konyagi,na alipenda mbali zahidi, akisema hacheni kuzarau kazi za watu,hivi kote zinapouzwa konyagi natengeneza Mimi,??
Hatutaki sikia,tunakua wazito kipokea USHAURI wa watu tofauti, na kuwabeza, tutalia wote,tutaumia wote bila kujali,we una nafasi gani, cheo gani, TENGENEZA TZ KWA VITUKUU NA VITUKUU ,JAMANI TZ NI KUBWA NA ZAHIDI YA MATAKWA YETU
 
Anaharishaa tuu huyo ndugai.wote tunajua mchakato wa kuwapata hao vitu maalum haujapitia kwenye chama rasmi.anataka kuhalalisha haramu kwa maslahi ya ccm na tumbo lake.akwendee zake huko.
 
Yani CHADEMA nilikuwa nakiamini na kukipigania,but sasa ni chama cha hovyo kabisa.Nitakaa tu bila ufuasi wowote ule
 
Wivu huo .Shetani ni wewe
Wivu wa nini/kipi?
Labda wewe unaewatendio shetani mwenzao.
Umeisoma hiyo barua kutoka BAWACHA?
Mnyika ajiandae kujiuzuru ukatibu mkuu kesho. Akajiunge na Tundu Lissu huko Ubeligiji kuendelea na uanaharakati. Siasa hawaziwezi. Wanaweza uanaharakati tu kama wa akina Maria Sarungi, Fatuma Karume, Tundu Lissu, Jenerali Ulimwengu na kadhalika.
Nimeisoma vizuri sana.
Sioni kitu humo zaidi ya mbinu zilezile za kihuni za kujihami kwa kuokoteza vijisababu vya kukumbatia usaliti.
Kama Kamati kuu itaungana na wasaliti waliovuruga katiba na taratibu za uteuzi za chama na nchi, Mnyika yuko tayari kujiuzulu sio tu wadhifa bali hata chama ili kuukataa na kujitenga na huo usaliti.
 
Hahaha kwani Ndugai naye sasa kawa mwenyeketi mwenza wa chadema?!

Chadema iwafukuze uanachama hao covid-19 na kama serikali wataifuta chadema na iwe hivyo.

Waliiua CUF ili kupave utawala wa Sheni Zanzibar na wataiua chadema bara ku pave utawala wa Magufuli Tanganyika.

Waiue chadema na iwe hivyo.

CCM waunde chama chao cha mfukoni, ila siyo chadema. Wakiiua chadema wameua vyama vingi Tanganyika na hawatapata chama mbadala tena.
 
Usiwaamini sana Chadema bwashee!
Nakubaliana na wewe. Nakumbuka ule wakati walifoji sahihi za wajumbe ili kumkataa Meya Muita. Na wakati ule walipofoji barua ya kumnyang'anya umeya ndugu Jacob na hata pale ambapo chama chake kilipowasilisha barua ya kuikana ile barua wakawaambia waende polisi. Bila shaka unakumbuka kisa kilichotokea Ubungo ambapo msimamizi aliwastukia walipowasilisha barua ya kufoji ya kujifanya ni wagombea wa chama chetu. Kweli hawafai kabisa. Sio watu wa kuwaamini.

Amandla...
 
Umeisoma hiyo barua kutoka BAWACHA?
Mnyika ajiandae kujiuzuru ukatibu mkuu kesho. Akajiunge na Tundu Lissu huko Ubeligiji kuendelea na uanaharakati. Siasa haziwezi. Anaweza uanaharakati tu kama wa akina Maria Sarungi, Fatuma Karume, Tundu Lissu, Jenerali Ulimwengu na kadhalika.
Nimeona Grace Kiwelu yuko upande wa Mnyika..... Ngoma inogile!
 
Huyu spika ameyumba mpaka sasa anagaragara chini.,
 
Walisema awataki wapinzani bungeni kulikoni. Yote ni uroho wa pesa ya mabeberu
 
Toka lini dungai akamtetea halima.
Huu ndo upunguani wake
Spika wa bunge Job Ndugai amemtaka katibu mkuu wa CHADEMA akajifunze namna ya kuwa katibu mkuu kwa Bashiru Ally ambaye ni Katibu Mkuu wa CCM.

Ndugai amesema kitendo cha Mnyika kuwasema hadharani, kuwahukumu na kuwashutumu wabunge wa viti maalum kwenye vyombo vya habari inaonesha wazi Mnyika hafai kuwa Katibu Mkuu.

Ndugai ameshauri mambo kama hayo huongelewa kwenye vikao vya ndani na kisha katibu mkuu hutoka na taarifa za kikao na kuwaambia wananchi sio kupayuka hadharani.

Sambamba na hilo Ndugai amesema kwamba yeye majina hayo kumi na Tisa(19) ya viti maalumu ya CHADEMA amepewa na Tume ya uchaguzi yeye kazi yake ni kuwaapisha tu Wabunge hao na ameshafanya hivyo. Na ameapa kuwalinda Wabunge hao hivyo amewataka wawe na imani kabisa.

Source: TBC ARIDHIO.
 
Spika wa bunge Job Ndugai amemtaka katibu mkuu wa CHADEMA akajifunze namna ya kuwa katibu mkuu kwa Bashiru Ally ambaye ni Katibu Mkuu wa CCM.

Ndugai amesema kitendo cha Mnyika kuwasema hadharani, kuwahukumu na kuwashutumu wabunge wa viti maalum kwenye vyombo vya habari inaonesha wazi Mnyika hafai kuwa Katibu Mkuu.

Ndugai ameshauri mambo kama hayo huongelewa kwenye vikao vya ndani na kisha katibu mkuu hutoka na taarifa za kikao na kuwaambia wananchi sio kupayuka hadharani.

Sambamba na hilo Ndugai amesema kwamba yeye majina hayo kumi na Tisa(19) ya viti maalumu ya CHADEMA amepewa na Tume ya uchaguzi yeye kazi yake ni kuwaapisha tu Wabunge hao na ameshafanya hivyo. Na ameapa kuwalinda Wabunge hao hivyo amewataka wawe na imani kabisa.

Source: TBC ARIDHIO.
Mnyika hakutoa hukumu. Alirudia mara mbili mbili kuwa kamati kuu ndio itakayoamua.

Mnyika hakumfokea mtu, alirudia mara nne nne kufafanua taratibu za mbunge VM kuchaguliwa.

Mnyika hana sababu ya kujifunza kwa Bashiru kwa sababu zilizo wazi

Nilitegemea Spika kwa uzoefu wake wa kibunge angefafanua sakata la Nusrat, na tarehe zinazotajwa kuleta utata hiyo ya tarehe 20 Novemba aliyoitaja yeye Spika na tarehe 23 aliyetolewa Nusrat Gerezani Usiku.

Angejibu hoja za Mnyika kwa kumtaja ni nani ndani ya Chadema aliyesaini tamko la Katibu mkuu kwenye form no 8D.


Angetamka uhalali wa kisheria wa akina Mdee katika kipindi ambacho chama kupitia kwa KM kinakana kushiriki kwenye chochote cha kupitisha VM.

Kinyume na hapo, ANAPIGA SIASA ZA KIZAMANI
 
Back
Top Bottom