Spika Ndugai: Nyani wanashangilia kifo cha mkulima wa mahindi wanasahau mwakani hawana pa kula

Spika Ndugai: Nyani wanashangilia kifo cha mkulima wa mahindi wanasahau mwakani hawana pa kula

Hii kauli ya Spika wa bunge mh Ndugai inafikirisha sana.

Hao nyani wanaofurahia kifo cha hayati Magufuli ni akina nani?

Je, ni Ufipa?

Na kwanini mwakani watakosa chakula?

Hata hivyo Ndugai amesema wanaoshangilia wanajidanganya Tanzania haitarejea kuwa shamba la bibi kamwe.

Maendeleo hayana vyama!
Tazama kwa jicho lililo kwenye paji la uso
 
Kauli za kijinga toka kwa wajinga...
Nyani wana akili sana... Hawategemeii mahindi pekee.
Uzuri mwingine ni kuwa hata kabla ya mkulima wa mahindi nyani walikuwepo...

Lakini nahisi atakuwa anawasema manyani walozoea vya kubebwa bebwa (kupewa pewa) kama yeye... Na hasa wabunge na mawaziri manyani...
That's a phrase you fool, yaani hii sentensi mmeitafsiri neno kwa neno na wala hamjahangaisha bongo zenu au yawezekana ndio uwezo wenu umefika mwisho...chekecha akili wewe mtu mzima, acha kuaibisha utu uzima...
 
Wapi nimesema ndugai ndio kaanzisha huo msemo? Wewe ni kubwa jinga mkuu.
Unataka kuniambia mpaka huo msemo ndugai kausema tu hajaanisha kitu hata kwa mawqzo yake?
pia unathibitisha ulivyo mpvmbavu maana umetafsiri hayo maneno literally....poor you!
Wenye akili wanakuona unavyojiingiza kwenye kundi lao kwa nguvu. Nimekuuliza hao uliowataja walipata nini kwa Magufuli ili mwakani wajute baada ya kifo chake? Jibu hilo ili watu waijue akili yako. Au wewe ndo Ndugai?
 
Kkoo mabakora yanatembea now[emoji848][emoji848]
 
Spika Ndugai: Nyani wanashangilia kifo cha mkulima wa mahindi wanasahau mwakani hawana pa kula!

Hii kauli ya Spika wa bunge mh Ndugai inafikirisha sana.
Haifikirishi kabisa. Maana yake ni kwamba mkulima aliyerithi shamba hawezi kuzalisha mazao, nyani watakosa pa kula lakini pia watoto wa mkulima huyu mrithi watakosa pa kula
 
Chama la wana!
Tabia za fisi kulana wao kwa wao!
Waliopo madarakani kwenye kila muhimili ni wao wenyewe. Sasa kina nyani ni kina nani??? 😅 😅
Mgonjwa ghali haijapata kutokea kuliko wagonjwa wote awamu zote za serikali. Anajisahau naye ni nyani!

Everyday is Saturday................................😎
 
Hivi Ndungai pamoja na changamoto zote za kiafya,bado havai barakoa tu?
 
Nina uhakika wanaoshangilia kifo cha Jiwe,wengi wao ni maCCM yenyewe yaliyotemwa kwenye teuzi mbalimbali na walioisoma namba!
 
Anatuita nyani sawa

Ni kwa sababu kashiba

Mwenzake pia alitutukana Sana .

Kama sisi Ni nyani yeye ni Nina?
 
Hii kauli ya Spika wa bunge mh Ndugai inafikirisha sana.

Hao nyani wanaofurahia kifo cha hayati Magufuli ni akina nani?

Je, ni Ufipa?

Na kwanini mwakani watakosa chakula?

Hata hivyo Ndugai amesema wanaoshangilia wanajidanganya Tanzania haitarejea kuwa shamba la bibi kamwe.

Maendeleo hayana vyama!

========================

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amewashukia watu wanaofurahia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli (61), kilichotokea Jumatano ya tarehe 17 Machi 2021.

Kiongozi huyo wa mhimili wa bunge, amewashukia watu hao leo Jumatatu tarehe 22 Machi 2021, wakati mwili wa Hayati Rais Magufuli ukiagwa na wabunge kwenye viwanja vya bunge jijini Dodoma.

Hayati Magufuli amefariki dunia katika Hospitali ya Mzena, mkoani Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu ya matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo.

Akizungumzia kifo hicho, Spika Ndugai amewafananisha watu hao na nyani waliofurahia kifo cha mwenye shamba la mahindi, ambaye alikuwa anawazuia kula mahindi yake.

“Sasa iko hadithi ya wale nyani walioshambulia shamba la mkulima kwenye mahindi, wakifurahi sana mahindi yanapokuwa yanaiva wanavuna wanakula, walipopata habari mwenye shamba amefariki wale nyani walifurahi sana.”

“Naamini katika nchi yetu manyani wa namna hii hawakosekani, lakini wakasahau mwaka uliofika wakati mahindi kuiva wakarudi shambani kula mahindi wakasahau mwenye shamba alifariki mwaka jana wakawa wanasikitika,” amesimulia Spika Ndugai.

Spika Ndugai ameshauri Watanzania, wasiwe kama ngedere hao kwa kutofanya mambo mabaya ambayo hayati Rais Magufuli aliyakat
Ushauri wa bure kwa ndugai,watu hawakupendi hata ccm wenzako kaa kimya kua mpole,huna hakika anayefata ni nani...
 
Bakhresa tajiri mkubwa Tanzania ndani ya kipindi cha Magufuli investment portfolio zake zimeongezeka

Mo Dowji kajitanua zaidi kwa kuongeza hisa za umiliki wa Simba na kawa dollar billionaire ndani ya Magufuli

Makampuni ya simu yameongeza network zao ndani ya Tanzania maana yake biashara ni nzuri.

Vijana wadogo kama akina Majjizo na Diamond utajiri wao umekuwa maradufu kipindi cha Magufuli.

Wapiga deal wenye kuelewa PEST analysis mazingira ya nje yanapobadilika na wewe inabidi ubadilike the likes of Rostam Aziz (wamerudisha media za CCM kwa wenyewe) na GSM JK alipotoka walibadili biashara na kujikita kwenye consumer market badala ya serikali wapo poa.

Kasheshe kwa wamatumbi ambao wamekariri lazima biashara wafanye na serikali tuu, hawa ndio wanaoshangalia kifo na wakosoaji wakubwa.

Kosa kubwa atakalofanya mama Samia ni kurudi nyuma hilo kundi la wamatumbi lazima wabadili attitude kuna opportunity nyingi sana za food processing industries ili kuongeza thamani ya mazao.

Kama wamatumbi ni wafanyabiashara kweli waende huko, lakini kurudi nyuma kufanya nao biashara ni kuwalemaza. Hizo shida watazoea tu baada ya muda uwezi kuanzisha biashara kwa malengo ya contract za serikali tu that is just pathetic.
 
Wenye akili wanakuona unavyojiingiza kwenye kundi lao kwa nguvu. Nimekuuliza hao uliowataja walipata nini kwa Magufuli ili mwakani wajute baada ya kifo chake? Jibu hilo ili watu waijue akili yako. Au wewe ndo Ndugai?
Sijibu swali la kijinga toka kwa mjinga. Wewe jifikirishe, tafsiri yako ninkuwa walipewa hela au kunufaika moja kwa moja?
 
Mjinga tu huyo.. alikuwa anategemea amuongezee jamaa yake muda wa kutawala Mungu akamfyekelea mbali. Sasa kwa ubaya aliomtendea Tundu Lissu kumfukuza kama mbwa na kumyima stahiki zake.. Karma inamfata yeye, sasa zamu yake na yeye..
Huyo Jamaa lazima karma imchape maana ule unyama kwa lissu alihusika kwa kiasi kikubwa sana
 
Back
Top Bottom