Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Hapo kawafundisha nini wabunge kama spika tu ndio hivyo wabunge wake itakuwa wanasikitisha sana
 
Ni wazi kauli yake imeleta uharibifu na mkanganyiko Mkubwa sana. Kwanini alikawia kuomba radhi? Tena badala ya kufafanua akadai anasemwa kwasababu yeye ni Mgogo!

Ndugai angeweza hata kutoa press release kama kweli alikuwa anaumwa kama anavyodai lakini aliamua kukaa kimya mpaka leo Je alikuwa anapima nini?

Je radhi yake ni ya kweli? Au ni namna ya kuwakabili wabunge kwenye kamati zinazotarajiwa kuanza?

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
Kaambiwa kamkosea Mungu. Samia ndiyo Mingu huku Tanganyika. Matunda ya Mwungano. Upuuzi mtupu
 
"Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana"

Tangu kuzaliwa kwangu sijawahi mwungamia binadamu mwenzangu.
Tumbooo na madaraka ni hatari Sanaa mkuu... Kwani unadhani ni kwa nini Polepole anahangaika Sana?
 
Hivi kaomba radhi kwa “kosa” gani haswa?

Kakosoa mwenendo wa Rais wa JMT, jemedari mkuu na mwenyekiti wa CCM. Ni kosa kubwa sana huko CCM.

Ingekuwa enzi za JPM, hiyo ni fatal mistake. Saa hizi asingekuwa bado akiuza sura ndani ya jengo na kuendelea kusemasema ovyo. Angeshachukua likizo bila malipo kutizamia afya yake.
 
Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3

Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko

Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote

Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali

NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa

Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika

Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma

NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE

Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake

Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa

Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
View attachment 2066990
View attachment 2067070
Pia soma;
Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni
Aitwe kwenye kamati ya maadili na ahojiwe na afungiwe kama anavyofanya kwa wenzake...Huu MTINDO WAKE WA KUTENDA MAKOSA MAKUSUDI NA KUOMBA RADHI SASA UMEKUWA SUGU KWA NDUNGAI...NYIE MCHEKEENI TU....ANA AKILI ZA KIJINGAJINGA SANA HUYU...MARA ACHAPE WATU FIMBO...KWA UMRI WAKE NA MATENDO YAKE NDANI NA NJE YA BUNGE NI YA OVYO OVYO SANA....ANA HILA HILA SANA HUYU, MARA HALIMA MDEE NA WENZAKE 19....SIJUI PUNGUANI
 
Yaani ile tuu plaizi za kuminya mananiliu zinaandaliwa jamaa akaona isiwe kesi.
 
Mtemi kakutana na watemi wenzake...ungeacha kupiga magoti ili ushuhudie unavyonyolewa..wewe si uliangia Prof Asad aletwe kwako kwa pingu...sasa ungeacha wewe ungekwenda kwa machela
 
Cha ajabu hata wananchi wengi wa kawaida wanaamini Ndugai kamkosea mama inabidi aombe msamaha, tuna safari ndefu sana watanzania
 
I have a family to feed not a community to impress....ametekenywa akatakenyaka akakumbushwa kuwa bado yy ni MGOGO
 
Mi naona ndugai kaleta changamoto nzuri kwa uongozi wala hakukosea kitu.
Watu wanakuja tu na mapesa yao kuwakopesha kwa mguvu ili mnunue matakataka au bidhaa au huduma toka makampuni yao halafu nchi inakopa ttu

Wanapata faida tupu mara mbili. Kwanza kuwakopesha mnalipa riba pilinanunua toka kampuni za kwao tena bei kubws tu. Sisi ni hasara tupu. Kwanza kidaikolojia wanakufanyeni tegemezi na wajinga. Pili mnachokopea hakina maana tena hela za mkopo zinaliwa na wao kushirikiana na wenyeji. Unakuta hakuna impact yoyote kwa mchi.

Alichosema ndugai tuwe na mikopo ya kuamua wenyewe kufuatana na mipango yetu sio kusukumiziwa mikopo ya kilaghai na kinyonyaji.
Wewe utalii ha Mungu wa Tanzania. Huyo mama ni Kama Mungu sasa hivi, kila kitu yeye tu. It is a very sad situation. Historians will tell us in the future. Alisema ukweli, why? Hakumegewa $$$$$,
 
Siasa za chama kimoja amnacho ni dominant bado Rais ana nguvu sana. Ndugai hawezi akamvimbia Rais kwa kuwa u-spika wake ni kwa hisani ya CCM ambayo Mwenyekiti wake ndiye Rais wa Tanzania.
 
Wakuu
Hii press ya Job leo unaichambuaje?

Je, Ndugai & The Gang walikuwa wanaupima upepo?

Je, wananchi ama wanaharakati wangeonesha kumuunga mkono angefanya hii submission press ya leo?

Thinkers wa JF, mnaiangaliaje hii move ya Ndugai kuomba radhi hadharani leo akiwa kama mkuu wa Mhimili huru wa Bunge? Jambo hili limekaaje
Kisiasa
Kiusalama
Kidemokrasia

Pascal Mayalla
Mshana Jr
figganigga
Mzito Kabwela
Mchambuzi87
Japo sijaalikwa kuchangia ngoja nimwage kapumba kangu kiduchu...

Bwana Job hakuwa na nia ya kuomba msamaha. Angekuwa na nia hiyo asingechukua muda mrefu hivyo. Siamini pia kama ni ushauri wa maswahiba zake wala presha ya maadui zake....

Naamini kapigiwa simu moja kutoka mamlaka za juu (labda za ulinzi na usalama) na kumshauri afanye hivyo au aachie ngazi

CDF akimpigia simu na kumwambia sijafurahi namna unavyolumbana na bosi wangu... Amiri Jeshi Mkuu wangu.... sidhani kama Job angekuwa na namna tena.

Maana ukubwa bado anautaka na kuupenda.

Hii kwa mama imemjenga sana kisiasa. Hivi sasa anasubiria awe hai 2025 achapishiwe form yake pekee ajaze akagombee muhula wa pili.

Hamna wa kumzuia tena
 
Mtemi kakutana na watemi wenzake...ungeacha kupiga magoti ili ushuhudie unavyonyolewa..wewe si uliangia Prof Asad aletwe kwako kwa pingu...sasa ungeacha wewe ungekwenda kwa machela [emoji38] [emoji1787] [emoji1]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom