Spika Ndugai: Serikali wapeni watu nafasi ya kufanya mambo yao, msiwe front sana

Alikuwa mateka
Ni kweli mkuu hadi unacheka ni huyu huyu Ndugai au mwingine we fikiri tu anaongea hivyo ghafla milango inafunguka na mwenda zake huyo anaingia 🤣 🤣 🤣 atatokea dirishani,naona akili alizokuwa kazishikilia Bwana yule zinaanza kurudi.
 
Aisee. Hata Yohana Mbatizaji kapata wokovu 😅
 
Ila Magufuli aliwafanya viongozi wa chini kuwa kama mtaahira,hebu eti fikiria walitakiwa kuchagua kati ya kuvaa barakoa na kazi
 
Huyu "Igandu" mbona kipindi hiki anajifanya kuwatetea sana watu, anajisogeza sana kwa wananchi kuliko kawaida yake! Halafu anajitahidi kuikaba koo serikali kuna nini?? Nadhani huyu mtu ameanza mapemaaa kuandaa mazingira ya 2025 au hata 2030 kwenye kinyang'anyiro cha urais!! Sidhani kama ni hivi hivi tu!!
 
Historia yake itamuandama, atafeli vibaya mno 2025
 
Anachoongea Ndugai ni kwenye. Kuna kitu kinaitwa citizenship freedom. Serikali ni mwezeshaji tu na siyo tightly controller wa watu. yaani unaitisha uchaguzi wa balozi pale kijijini napo serikali na mabunduki mgongoni, uchaguzi wa kitongoji tu mapolisi yamejaa, hapana.

Lazima kuwe na semi-autonomous ya raia. hata mzazi hutakiwi kuwa mgongoni pa mtoto wako kila mahali. Mpe muda wa ku-exercise maturity and independence. Hata Mwalimu kuna wakati anatakiwa kumpa nafasi mwanafunzi kufikiri na kutenda kwa kujitegemea na siyo tightly supervision.

Ila najiuliza, kumbe Ndugai anayajua haya mambo ila alikuwa anafanya makusudi?
 
mgonjwa wetu kapona sasa msimpe uji tena mpatieni ugali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…