Spika Ndugai: Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, wakikaa na simu wanaperuzi tu

Spika Ndugai: Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, wakikaa na simu wanaperuzi tu

Kutoka Dodoma.

"Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, ambao wakikaa na simu wanaperuzi mitandaoni tu"...
Spika hajui kwamba Kodi kubwa ni chanzo cha nambari wani cha vijana kukosa ajira

Ngumu kuanza biashara Kwa muundo wa Kodi wa sasa

Na adhabu wanazotoa ni Kali sana
 
Kutoka Dodoma.

"Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, ambao wakikaa na simu wanaperuzi mitandaoni tu"...
Ndugai yuko bungeni zaidi ya miaka 15, kwanini asiwaachie wasio na mitaji nao wapate ili yeye akafungue kiwanda atoe ajira? Anaingia bungeni kwa kunajisi uchaguzi, kama kazi ni nyingi kwanini atumie mbinu haramu kuendelea kuwa mbunge?
 
Watu wengi wanaofanikiwa wanatokea kwenye mazingira haya haya miaka nenda rudi wengine wanalalamika maisha magumu Vijana wengi wa kitanzania ni wavivu kuna Makundi mengi ni tegemezi hawataki kujishughulisha mfano hawa vijana wanywaji wa pombe za kienyeji ,watumiaji wa Instagram,vijana wa kubeti nk

Kwaio unataka tusibet au??
 
Ndugai alifanikiwa kwa kufanya kazi gani zaidi ya kupiga porojo huko bungeni? Atuambie ni wapi watoto wake wamejiajiri zaidi ya kuchomekwa serekalini ili tuone uhalisia wa anachosema.
 
Mh. usingepata hiyo kazi hapo ulipo nawe ungezurura tuu mitaani. Watu wanapenda kazi tatizo zikowapi? Viwanda vikowapi? kilimo mmekiwezeshaje? Maslahi vipi?

Huwa hamuoni nafasi zakazi zikitoka watu hujazana? Au mnakuwaga nchi za nje?? Wapeni vijana ajira msiwabeze,kavp achieni ajira zenu tuingie nasisi
 
Waongeze kodi!!? Hivi hawa huwa hawasomi historia? Hiyo kauli inatofauti gani na Malkia wa Ufaransa ambaye baada ya watu kulia kuwa hawana mikate akawaambia kama hawana mikate wale keki!!?.

Mtu hana ajira halafu unamuongezea kodi?!
 
Kutoka Dodoma.

"Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, ambao wakikaa na simu wanaperuzi mitandaoni tu".

"Nafikiri labda tuongeze kodi labda itapunguza hata sijui, hivi tufanye kitu gani ili tuhakikishe kila mtu anafanya kazi, maafisa maendeleo ya jamii hawafanyi kazi" -Job Ndugai.

Nini maoni yako mdau?
Kama ni kweli Mzee Ndugai amesema maneno haya, basi nimesikitishwa sana na kauli hii. Kuna wavivu wasiopenda kufanya kazi vile vile kuna wanaopenda kufanya kazi ila hawana hizo kazi.

Maisha ya mtaani sasa ni changamoto kwa vijana wooote pasipo kujali itikadi zao za vyama.
 
dah Hawa viongozi wetu bana ,Vijana tusichoke kusali utawala huu umalize muda wake tu wapumzike ,maybe utawala ujao utaweka sera nzuri za vijana na vipaombele vyakufuta umasikini ,Yaan wabunge kupiga meza tu na hoja mfu mnajikuta mnafanya Sana kazi !
Mnatusikitisha Sana lakin
 
Yaani kwa kuwa Vijana hawana ajira basi waongezewe kodi?.

Yaleyale ya Malkia aliyesema kama Watu hawana Mkate wale keki.
 
Ukomo wa ubunge unapaswa uwepo. Mbunge akitumikia miaka 10 au awamu 2 inatosha kabisa. Wapishe wengine wenye experience za mtaani kama wanao-comment.

Hii mtu anakua mbunge miaka 15 hadi 20 si sawa kabisa. Kwanza analipwa hela nyingi huku akitoa mchango wa kipuuzi kama huu wa Ndugai. Pili anabweteka yan it’s like liwalo na liwe while wanaoteseka ni raia wa chini kabisa
Siyo ukomo wa ubunge tu sekita zote ziwe na ukomo Kama ilivyo kwenye uraisi kuanzia ubunge, uwaziri, ukuu wa wilaya, mkoa maana ni sekita za kuleta amsha amsha alafu watoke waingie wengine. Na serikali kuu na taasisi hivyo hivyo zile zinazozidisha miaka sitini ziangaliwe upya Ili vijana wakatumike.
 
Watu wengi wanaofanikiwa wanatokea kwenye mazingira haya haya miaka nenda rudi wengine wanalalamika maisha magumu Vijana wengi wa kitanzania ni wavivu kuna Makundi mengi ni tegemezi hawataki kujishughulisha mfano hawa vijana wanywaji wa pombe za kienyeji ,watumiaji wa Instagram,vijana wa kubeti nk
Nenda zako na Ndugai wako.
 
Taratibu tunarudishwa miaka ya 80 sasa hivi utasikia "Operation Nguvu Kazi" inarudi

Gwala Tena mpaka tutie akili shubaaaamit!!!
 
Back
Top Bottom