Spika Tulia: Tusichanganye Maadili ya Mtanzania na Imani za kidini. Lipi kosa la walimu waliosimamishwa kazi Kwa kucheza muziki? Warudisheni kazini

Wanavyofanya wenzetu ambao wametutangulia katika mambo haya ni hivi.

Wasanii wanarekodi nyimbo zenye versions tofauti, version moja inakuwa ni ya "explicit lyrics" wanaweza kununua wanaopenda. Hii inakuwa na maneno makali yote. Ni kwa ajili ya wakubwa, haitakiwi kupigwa redioni wala sehemu yoyote public kwenye watoto.

Hata ukinunua CD utakuta imeandikwa "Parental Advisory. Explicit Lyrics".

Version nyingine inakuwa "radio version", hii inakuwa imeondolewa maneno makali. Inaweza kupigwa redioni au sehemu zenye watoto.

Hapo msanii hajaondolewa uhuru wake wa kisanii, na jamii haijalazimishwa kusikia maneno makali pale pasipostahili.

Tatizo, huko Tanzania, kwenye nyimbo zenye maneno makali, hatuna kitu kinaitwa "radio version". Kila wimbo ni "explicit lyrics" version inapigwa sehemu zote, kuanzia redioni mpaka shuleni.
 
Na hii ndo alichokigundua Spika kwamba Proff mkenda anajaribu kuficha maovu ya wizara ya michezo kwa kutoa walimu kafara wakati kosa liko wizara ya michezo
Jamani,huyo hana tofauti na yule naesikia anavunja nyumba za watu jijini kisa wakazi. Mwalimu mkuu,hajatunga wimbo,hajausambaza. Mwalimu,siyo DJ. Labda kama aliomba upigwe,hapo ntaunga mkono wa kumshusha cheo na kuchukuliwa hatua za kinidhamu ingekuwa poa. Lakini, maadili mnayolilia siku hizi yako wapi? Bungeni kwenyewe wanatoleana maneno ya aibu,mtu mzima anaetazama hilo bunge anajifunza nini? Siku hizi,walimu hao ni vitoto vidogo vya umri sawa na wa wanafunzi. Kumbukeni,ni wa hiki kizazi kisicho na maadili. Kwanza,hiyo BASATA ina kazi gani? Kama taarifa gazetini kwanza inahaliliwa,kwa nini hata hiyo BASATA isingekuwa na kamati ya kuelekeza wasanii na kuwakosoa!! Kizazi cha kihuni,kinapenda maneno ya kihuni. Ili msanii auze,lazima atumie maneno hayo hayo. Bahati mbaya hawa watu wenye vipato cyao,hakika watoto wao hawachezi. Lakini angeingia mitaa ya kiswahili aangalie huo wimbo unavyochezwa na vitoto vidogo,unajiuliza haka kakifikisha miaka 10 itakuwaje! Vigodolo vimeanzia miaka 3 na kuendelea sasa
 
Ahsante Spika Tulia PhD

Nilisema hapa JF mbona kwenye mikutano ya CCM tunachezaga huwo Wimbo wa Honey tukiwa tumechanganyikana na wanafunzi wa Chekechea, Primary na secondary?!!
 
Akhsante Spika Tulia.

Mhe. Waziri alifanyamaamuzi yaharaka bila kuzingatia taratibu na kanuni.

Warudishwe kazini
 
Siyo kila nyimbo inapigwa kila mahali, watoto wanapaswa kufundishwa maadili mema, Maudhui ya ile nyimbo yanafaa watu walioko kwenye ma-bar na magenge mengine ya wahuni
Tulia hajakosea chochote. Kama huo mziki umeruhusiwa kupigwa na kuchezwa hadharani kwanini hao watoto na walimu waadhibiwe? Kwani hawa si sehemu ya jamii? Tunaposema maadili tusibane upande mmoja, kwanini tusianze na kumuadhibu yule aliyeutunga? Naungana na Tulia, tukitaka kuchanganya miiko ya kidini ktk taasisi za umma kwa kisingizio cha maadili lazima tutakwama. Shule za umma si sehemu ya seminary, hivyo tusichanganye mambo ya dini kwenye taasisi zetu za umma.
 
Hapaswi kuingilia majukumu ya serikali kwanza waziri amesema wamesimamishwa hii maana yake uchunguzi unafanyika na hatua stahiki zitachukuliwa uchunguzi utakapokamilika ,hivyo aache kiherehere na kutafuta sifa za kijinga.
 
Siyo kila nyimbo inapigwa kila mahali, watoto wanapaswa kufundishwa maadili mema, Maudhui ya ile nyimbo yanafaa watu walioko kwenye ma-bar na magenge mengine ya wahuni
Hilo kosa la basata Kama wimbo hauna maadili,watoto hawakutakiwa kuujua
 
Waziri wa Michezo na Utamaduni anatakiwa kuwajibika yye pamoja na BASATA kwa kosa hili na sio waalimu
 
Hapaswi kuingilia majukumu ya serikali kwanza waziri amesema wamesimamishwa hii maana yake uchunguzi unafanyika na hatua stahiki zitachukuliwa uchunguzi utakapokamilika ,hivyo aache kiherehere na kutafuta sifa za kijinga.
Ameyasema hayo akiwa amekalia kiti cha mamlaka ambayo Waziri anakuwa chinj yake!
Ila hata hivyo tukiachana na hayo ...

Kitumishi sio sawa kumsimamisha mtumishi bila kusikiliza utetezi wake unatakiwa upate maelezo ya pande mbili pande inayohukumu na pande inayojitetea ndo utoe maamuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…