Spika Tulia: Tusichanganye Maadili ya Mtanzania na Imani za kidini. Lipi kosa la walimu waliosimamishwa kazi Kwa kucheza muziki? Warudisheni kazini

Spika Tulia: Tusichanganye Maadili ya Mtanzania na Imani za kidini. Lipi kosa la walimu waliosimamishwa kazi Kwa kucheza muziki? Warudisheni kazini

Amesema hayo akihoji kuhus Njia iliyotumika Kuwasimamisha walimu hao,Bila ya kufuata utaratibu wa kinidhamu wa kiutumishi,Hata hivyo ameongeza na kusema kuwa lisionewe kundi fulani tu kwani hata baadhi ya wabunge pia nao wanacheza miziki hiyo..

"Wapo mawaziri humu ndani na sisi wabunge huwa tunacheza mziki na hao wanafunzi, Tufafanuliwe hapa ili watu wajue nini cha kufanya la sivyo tutaendelea kucheza huo mziki na watoto wakiwepo shuleni alafu tutawapomza wale ambao watatakiwa kuchukuliwa hatua ,kwahiyo ni muhimu muwe na hatua zaidi ya hapa ili watu wote wawe na uelewa ni miziki gani inachezwa na ipi haichezwi itasaidia sana,Lakini tusiingize Huko hisia za kidini tusichanganye Imani ya dini na maadili ya mtanzania tusivichanganye" amesema Dkt tulia Ackson spika wa bunge la Muungano leo bungeni

hata hivyo aliendelea kumhoji waziri Njia iliyotumika kuwasimamisha walimu wao kazi na akasema kuwa njia hiyo haikuwa na usawa hivyo ameomba warudishwe makazini na njia sahihi zifuatwe

View attachment 2805936

View attachment 2805928
Mbwa wehu hata akiwa anabweka kukuamsha unahisi anakubwekea wewe akung'ate
 
Na ndo maana Spika ameomba apewe utaratibu wa nyimbo zinazoruhusiwa wapi na sehsmu gani
Hata kama hawana, hata common sense nazo haziruhusiwi? Kama ameona haina maadili angeipongeza serikali na kuitaka itengeneza guidelines
 
Hapaswi kuingilia majukumu ya serikali kwanza waziri amesema wamesimamishwa hii maana yake uchunguzi unafanyika na hatua stahiki zitachukuliwa uchunguzi utakapokamilika ,hivyo aache kiherehere na kutafuta sifa za kijinga.
Kosa la kucheza mziki linaitaji uchunguzi gani? Tuache kushabikia vitu vya hovyo. Kazi ya mbunge ni kuishauri na kuisimamia serikali, Tulia kakosea nini kama mbunge na spika au wewe ndiye unaetafuta sifa kwa waziri.
 
Kosa la basata haliwezi kuwa kibali.
Mkuu kwa mfano Umenunua bidhaa supermaket ukaileta nyumbani ukamkabidhi mkeo akaandaa mkala..
Baada ya muda mkapata Food poison..

Chakula kikapimwa kikagundulika kilikuwa chini ya ubora..
Utampa Talaka mkeo kukuandalia chakula Kibovu au utaenda kuwafata Supermarket kuwawajibisha?
Na ikiwezekana hasa kampuni iliyotengeneza?

Sasa utamwajibishaje Dobi kutakasa kaniki?
 
Amesema hayo akihoji kuhus Njia iliyotumika Kuwasimamisha walimu hao,Bila ya kufuata utaratibu wa kinidhamu wa kiutumishi,Hata hivyo ameongeza na kusema kuwa lisionewe kundi fulani tu kwani hata baadhi ya wabunge pia nao wanacheza miziki hiyo..

"Wapo mawaziri humu ndani na sisi wabunge huwa tunacheza mziki na hao wanafunzi, Tufafanuliwe hapa ili watu wajue nini cha kufanya la sivyo tutaendelea kucheza huo mziki na watoto wakiwepo shuleni alafu tutawapomza wale ambao watatakiwa kuchukuliwa hatua ,kwahiyo ni muhimu muwe na hatua zaidi ya hapa ili watu wote wawe na uelewa ni miziki gani inachezwa na ipi haichezwi itasaidia sana,Lakini tusiingize Huko hisia za kidini tusichanganye Imani ya dini na maadili ya mtanzania tusivichanganye" amesema Dkt tulia Ackson spika wa bunge la Muungano leo bungeni

hata hivyo aliendelea kumhoji waziri Njia iliyotumika kuwasimamisha walimu wao kazi na akasema kuwa njia hiyo haikuwa na usawa hivyo ameomba warudishwe makazini na njia sahihi zifuatwe

View attachment 2805936

View attachment 2805928
Spika yupo sawa. Wizara inayohusika itoe waraka kwa shule kuhusu utaratibu wa wanafunzi kuburudika na miziki. Pia waraka wa wafadhili wanaoenda shuleni moja Kwa Moja.
 
Kwa kosa la kupiga wimbo usio na maadili na wenye kuhamasisha ngono. Ni mjinga pekee anaweza kupiga wimbo wowote mahali popote. Mkuu wewe unaweza kupiga wimbo "Zagamua" mbele ya wanao?
Kwann huo wimbo usifungiwe kama hauna maadili. Au unataka kusema kila sehemu unakopigwa watoto hawausikilizi? Ukipigwa kwenye baa karibu na nyumbani kwako utahama kisa una watoto nyumbani?
 
Watoto wenu wanachezeshwa nyimbo za ajabu za watu waliopotea kumaadili huko shuleni, watoto wao wanasoma kwa bidii na kufuata taratibu za miongozo ya shule zao za mamilioni ya pesa.

Mko hapa mnaita Waziri mjinga na kupambania walimu wakuu wazembe walioshindwa kusimamia shule.

Watawatawala wao na wakizeeka mtatawaliwa na watoto wao na wajukuu, endeleeni kushabikia uzembe na ujinga ujinga.
 
Ameyasema hayo akiwa amekalia kiti cha mamlaka ambayo Waziri anakuwa chinj yake!
Ila hata hivyo tukiachana na hayo ...

Kitumishi sio sawa kumsimamisha mtumishi bila kusikiliza utetezi wake unatakiwa upate maelezo ya pande mbili pande inayohukumu na pande inayojitetea ndo utoe maamuzi
Serikali imekuwa ikifanya hivi mara kwa mara na hata imeshatokea mara kadhaa kwa wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali na maofisa wengine wa serikali kusimamishwa kazi inapotokea kiongozi au mtumishi ametuhumiwa kwa kosa fulani na lengo hasa ni kumzuia mtu huyo asiingilie uchunguzi utakaokuwa ukifanywa juu ya tuhuma dhidi yake na uchunguzi utakapokamilika ndipo hatua stahiki zinachukuliwa na pale inapobainika mtumishi hakuwa na makosa basi urudishwa kazini na kulipwa stahiki zake zote.
Na ni pale uchunguzi unapofanyika ndipo mtuhumiwa uhojiwa na kupata fursa ya kujitetea.
 
Watoto wenu wanachezeshwa nyimbo za ajabu za watu waliopotea kumaadili huko shuleni, watoto wao wanasoma kwa bidii na kufuata taratibu za miongozo ya shule zao za mamilioni ya pesa.

Mko hapa mnaita Waziri mjinga na kupambania walimu wakuu wazembe walioshindwa kusimamia shule.

Watawatawala wao na wakizeeka mtatawaliwa na watoto wao na wajukuu, endeleeni kushabikia uzembe na ujinga ujinga.
Sasa unazuiaje Shuleni wakati nyumbani wanasikiliza?
Mkuu umeiona clip?

Pengine hata walimu walikuwa hawajui nyimbo ile imaimbwaje ila watoto wale waliimba nyimbo kuanzia mwanzo mpaka mwisho..
hiyo ingetosha kutoa picha kwamba mwenye kosa sio mwalimu aliyecheza nyimbo hiyo ila mwenye kosa ni BASATA kuachia nyimbo kupigwa ikiwa haina maadiki
 
Back
Top Bottom