Spika Tulia: Tusichanganye Maadili ya Mtanzania na Imani za kidini. Lipi kosa la walimu waliosimamishwa kazi Kwa kucheza muziki? Warudisheni kazini

Wanawalea kwa nidhamu ili waje kuwaongoza watoto wanaokata viuno shuleni kwenye vumbi. Watoto wa darasa la nne tayari akili ipo kingonongono, Waziri akisimama kulinda maadili wanamuita mjinga.
Ndicho kinachofanyika

Wanawabomoa watoto wa wenzao

Wakati wa kwao wanalelewa kwenye mstari,ili waje na wazidi kukutawala

Anyway Acha kila mzazi abebe msalaba wake asiyesikia Acha aendelee,mitoto ikiharibika who cares

Ova
 
Kuna sehemu umeona nimeandika kufukuzwa kazi mkuu Au wewe ndo umekuja na perception zako kichwani..
Taarifa ni kwamba wamevuliwa vyeo wakati huo huo wamesimamishwa kupisha uchunguzi
Sawa basi,nyie endeleeni kuwasikilisha watoto miziki hyo
Sijui honey,ameyatimba,kuzaguama

Ova
 
Sawa basi,nyie endeleeni kuwasikilisha watoto miziki hyo
Sijui honey,ameyatimba,kuzaguama

Ova
Wanangu me wote watu wazma wana maamuzi yao wakiamua kusikiliza shaur yao watajua wao..
Sasa toto lina miaka 20 naanza kuliambia usimsikilize zuchu si ntakuwa sina akili
 
Huo wimbo hauna maadil kwa watoto. Haufai kusikilizwa au kuchezwa nashuleni. Hao walimu hawajui miongozo na taratibu za shule kuhusu maadili? Walipaswa kumwambia DJ aweke wimbo mwingine wenye maadili na siyo huo wa namkatia viuno viuno. Ukosefu wa maadili ndiyo unapelekea mwisho wake watoto wanafanya vitendo vya ubakaji na ulawiti. Mwenye hasara siyo mama Gwajima wala Profesa Mkenda. Acha inyeshe tuone panapovuja.
 
Role ya mwalimu ni kulea pia, so jamii inategemea vitu vikubwa zaidi ya kuwachezesha watoto nyimbo za kipumbavu
Mbona hujataka wanasiasa waliochezesha hizo nyimbo mbele ya wanafunzi nao wafutwe vyeo vyao?
Mwalimu analea kwa kutumia vigezo, kwahiyo siku nyingine CWT wapige marufuku vyakula vya watoto visivyo na ubora kwa sababu "wanalea"? Kazi ya TBS na TFDA ni nini.

Kipimo cha mziki kinatolewa na BASATA. Lini ulisikia huo wimbo umekatazwa kuchezwa under 18 au mashuleni? Kwanini BASATA wasiwajibike badala yake wawajibike walimu.
 
Na hii ndo point nayosema na kama Basata Haitawajibika Basi wizara ya Michezo iwajibike
 
Huyu Tulia kuna Wakati hua nampenda sana anapoacha kuchanganya maslahi Binafsi na taaluma yake.

Yuko Sawa kabisa.
Ule mziki haujafungiwa popote Kwa kukiuka madili ya Mtanzania ,hivyo ni halali kuchezwa popote na watu kuburudika bila vikwazo.

Kama Huo mziki ungekua umekiuka maadili ya Mtanzania basi ulipaswa kufungiwa na maD.J wasingeuweka kwanye Tafrija.

Hao walimu warejeshwa haraka sana kwenye nafasi zao na wapongezwe Kwa kuonyesha Uzalendo mkubwa Kwa kuifurahia KAZI Yao pamoja na mazingira magumu na maslahi Duni.
 
Spika ni Jembe[emoji91][emoji91][emoji91]
Ameongea ukweli
 
Video nzima Ya maelezo hapo juu hii hapaaa
Your browser is not able to display this video.
 
Dr Tulia yuko sahihi, jamii yenyewe imeshajiharibikia. Tatizo viongozi wetu muda wote wako kwenye magari full tinted na wanaishi ushuani. Wangekuwa na wasaa wa kuzunguka uswahilini maeneo kama Mbagala, Tandale, Buguruni, Manzese na kwingineko ndo wangejua jamii tuliyonayo sasa imeharibika kiasi gani, vitoto vinajua nyimbo zote hasa zenye maneno ya matusi, wazazi wanacheza vigodoro uchi wa mnyama na watoto wanashuhudia. Kwa kifupi kwenye maadili nchii hii tumeshafeli na hii yote inatokana na ubinafsi wa viongozi wetu. Walimu warudishwe kazini bhana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…