Jamani,huyo hana tofauti na yule naesikia anavunja nyumba za watu jijini kisa wakazi. Mwalimu mkuu,hajatunga wimbo,hajausambaza. Mwalimu,siyo DJ. Labda kama aliomba upigwe,hapo ntaunga mkono wa kumshusha cheo na kuchukuliwa hatua za kinidhamu ingekuwa poa. Lakini, maadili mnayolilia siku hizi yako wapi? Bungeni kwenyewe wanatoleana maneno ya aibu,mtu mzima anaetazama hilo bunge anajifunza nini? Siku hizi,walimu hao ni vitoto vidogo vya umri sawa na wa wanafunzi. Kumbukeni,ni wa hiki kizazi kisicho na maadili. Kwanza,hiyo BASATA ina kazi gani? Kama taarifa gazetini kwanza inahaliliwa,kwa nini hata hiyo BASATA isingekuwa na kamati ya kuelekeza wasanii na kuwakosoa!! Kizazi cha kihuni,kinapenda maneno ya kihuni. Ili msanii auze,lazima atumie maneno hayo hayo. Bahati mbaya hawa watu wenye vipato cyao,hakika watoto wao hawachezi. Lakini angeingia mitaa ya kiswahili aangalie huo wimbo unavyochezwa na vitoto vidogo,unajiuliza haka kakifikisha miaka 10 itakuwaje! Vigodolo vimeanzia miaka 3 na kuendelea sasa