Spika Tulia: Tusichanganye Maadili ya Mtanzania na Imani za kidini. Lipi kosa la walimu waliosimamishwa kazi Kwa kucheza muziki? Warudisheni kazini

Spika Tulia: Tusichanganye Maadili ya Mtanzania na Imani za kidini. Lipi kosa la walimu waliosimamishwa kazi Kwa kucheza muziki? Warudisheni kazini

Amesema hayo akihoji kuhus Njia iliyotumika Kuwasimamisha walimu hao,Bila ya kufuata utaratibu wa kinidhamu wa kiutumishi,Hata hivyo ameongeza na kusema kuwa lisionewe kundi fulani tu kwani hata baadhi ya wabunge pia nao wanacheza miziki hiyo..

"Wapo mawaziri humu ndani na sisi wabunge huwa tunacheza mziki na hao wanafunzi, Tufafanuliwe hapa ili watu wajue nini cha kufanya la sivyo tutaendelea kucheza huo mziki na watoto wakiwepo shuleni alafu tutawapomza wale ambao watatakiwa kuchukuliwa hatua ,kwahiyo ni muhimu muwe na hatua zaidi ya hapa ili watu wote wawe na uelewa ni miziki gani inachezwa na ipi haichezwi itasaidia sana,Lakini tusiingize Huko hisia za kidini tusichanganye Imani ya dini na maadili ya mtanzania tusivichanganye" amesema Dkt tulia Ackson spika wa bunge la Muungano leo bungeni

hata hivyo aliendelea kumhoji waziri Njia iliyotumika kuwasimamisha walimu wao kazi na akasema kuwa njia hiyo haikuwa na usawa hivyo ameomba warudishwe makazini na njia sahihi zifuatwe

View attachment 2806039

View attachment 2805928
Walimu ni kundi la watumishi linaloonewa na kukandamizwa sana na wanasiasa maamuma.
 
Hata bila Spika kuhoji,yeye Kwa akili yake anaona ni sawa kuimba wimbo huo Shuleni?

Mdau kasema hapo tuwe na versio mbili za public na parental
Yeah mkuu kwa sababu BASATA Hawana mfumo huo hapo wa kwanza kiwajibika angekuwa BASATA na wizara ya Michezo kwa ujumla kwa sababu wameshindwa kufanya Censorship ya nyimbo ambazo hazina maasili kama sio kuzifungia kabisa au kuna double standard kwenye kufungia nyimbo zinaangaliwa zinazopinga serikali tu?
 
Ni kweli Kuna viongozi hawatofaitishi kati Imani au maadili ya kidini na maadili ya jumla ya Mtanzania
Na hapo ndio changamoto...
Linatakiwa Somo lianze kufundishwa kuhusu hasa ni IPI MILA/MAADILI YA MTANZANIA ili watu watofautishe na Tamaduni za kidini...
Kwa mfano kuwa na wake wengi hiyo ni mila ya mtanzania ila kidini hasa ukristo hairuhusu kwahyo mtu akioa watu watamwona kaenda kinyume na maadili..

Kwahyo inabidi uchorwe mstari kuhusu maadili ni yapi na Ipi ni tamaduni za kidini
 
Kidomodomo sana. Ukiacha madawa ya kisafa na kinyakyusa anayotegemea hana jipya. Integrity ya nchi imeshuka na kuonekana ya kike kike kila kona. Tangu aingie uspika bungeni, hakuna mjadala na mswada wa maana uliopitishwa. Bunge limekosa hata meno kuwWajibisha wezi wa fedha za umma, It is a shame. PhD holder unadandia vistory vya vijiweni vya kina Zuchu,hopelesss.
Lilikuwa ni swali la Mbunge aliuliza kwahyo na yeye akaamua kuchagiza..angalia atached video utaelewa..hata ya CAG pia amegongelea msumali na kasema kuna pesa kweli zimeibiwa
 
Walimu ni kundi la watumishi linaloonewa na kukandamizwa sana na wanasiasa maamuma.
Huu ni ukweli sana unakuta eti mpaka mwenyekiti wa mtaa na kitongoji anawakoromea walimu na anajifanya boss wake tukiamua kuwatetea kuna watu wanakuja juu wanataka walimu waendelee kuonewa hii sio sawa...

Wanafnya kazi kwwny mazingira magumu hebu tuwape motisha sio kuwakandamiza..
Kitu hicho hicho akifanya mkuu wa mkoa,Mbunge ,mkurugenzi na watumishi wengine haikiitwi kuvunja maadili ila akifanya yeye anavunja maadili hebu tuae na huruma...
 
Nje ya mada kidogo

Hivi suala la Mdundo wa Taifa limefikia wapi pamoja na vazi la Taifa
 
Amesema hayo akihoji kuhus Njia iliyotumika Kuwasimamisha walimu hao,Bila ya kufuata utaratibu wa kinidhamu wa kiutumishi,Hata hivyo ameongeza na kusema kuwa lisionewe kundi fulani tu kwani hata baadhi ya wabunge pia nao wanacheza miziki hiyo..

"Wapo mawaziri humu ndani na sisi wabunge huwa tunacheza mziki na hao wanafunzi, Tufafanuliwe hapa ili watu wajue nini cha kufanya la sivyo tutaendelea kucheza huo mziki na watoto wakiwepo shuleni alafu tutawapomza wale ambao watatakiwa kuchukuliwa hatua ,kwahiyo ni muhimu muwe na hatua zaidi ya hapa ili watu wote wawe na uelewa ni miziki gani inachezwa na ipi haichezwi itasaidia sana,Lakini tusiingize Huko hisia za kidini tusichanganye Imani ya dini na maadili ya mtanzania tusivichanganye" amesema Dkt tulia Ackson spika wa bunge la Muungano leo bungeni

hata hivyo aliendelea kumhoji waziri Njia iliyotumika kuwasimamisha walimu wao kazi na akasema kuwa njia hiyo haikuwa na usawa hivyo ameomba warudishwe makazini na njia sahihi zifuatwe

View attachment 2806039

View attachment 2805928
Spika yupo sahihi wanaopasa kutimuliwa ni wale waliouruhusu huo wimbo uendelee kuwepo Nchini bila kuufungia !!
 
Jamani,huyo hana tofauti na yule naesikia anavunja nyumba za watu jijini kisa wakazi. Mwalimu mkuu,hajatunga wimbo,hajausambaza. Mwalimu,siyo DJ. Labda kama aliomba upigwe,hapo ntaunga mkono wa kumshusha cheo na kuchukuliwa hatua za kinidhamu ingekuwa poa. Lakini, maadili mnayolilia siku hizi yako wapi? Bungeni kwenyewe wanatoleana maneno ya aibu,mtu mzima anaetazama hilo bunge anajifunza nini? Siku hizi,walimu hao ni vitoto vidogo vya umri sawa na wa wanafunzi. Kumbukeni,ni wa hiki kizazi kisicho na maadili. Kwanza,hiyo BASATA ina kazi gani? Kama taarifa gazetini kwanza inahaliliwa,kwa nini hata hiyo BASATA isingekuwa na kamati ya kuelekeza wasanii na kuwakosoa!! Kizazi cha kihuni,kinapenda maneno ya kihuni. Ili msanii auze,lazima atumie maneno hayo hayo. Bahati mbaya hawa watu wenye vipato cyao,hakika watoto wao hawachezi. Lakini angeingia mitaa ya kiswahili aangalie huo wimbo unavyochezwa na vitoto vidogo,unajiuliza haka kakifikisha miaka 10 itakuwaje! Vigodolo vimeanzia miaka 3 na kuendelea sasa
Spika yuko sahihi, kama wimbo huo hauna maadili kwanini BASATA wameupitisha upigwe kwenye jamii? Hao walimu walikuwa wameonewa , pia ikumbukwe hapo shuleni kulikwa na hafla ndo mziki huo ukapigwa je walimu wangezuia watoto wasicheze? Darasa la 7 Huwa wana graduation zao na huwa wanacheza miziki hiyo hiyo na wanafanyia shuleni.
 
Siyo kila nyimbo inapigwa kila mahali, watoto wanapaswa kufundishwa maadili mema, Maudhui ya ile nyimbo yanafaa watu walioko kwenye ma-bar na magenge mengine ya wahuni
Ndiyo maana kasema warudishwe kazini HALAFU NJIA SAHIHI ZIFUATWE..!! Wale walimu wakishitaki kuhusu utaratibu itakuwaje..!!?? Sababu kama hizi ndo zinatufanya hadi leo tunalimwa mafaini kisa kuna mtu mmoja hakufuata taratibu kwenye kuvunja mikataba iliyopo kisheria.
 
Wanavyofanya wenzetu ambao wametutangulia katika mambo haya ni hivi.

Wasanii wanarekodi nyimbo zenye versions tofauti, version moja inakuwa ni ya "explicit lyrics" wanaweza kununua wanaopenda. Hii inakuwa na maneno makali yote. Ni kwa ajili ya wakubwa, haitakiwi kupigwa redioni wala sehemu yoyote public kwenye watoto.

Hata ukinunua CD utakuta imeandikwa "Parental Advisory. Explicit Lyrics".

Version nyingine inakuwa "radio version", hii inakuwa imeondolewa maneno makali. Inaweza kupigwa redioni au sehemu zenye watoto.

Hapo msanii hajaondolewa uhuru wake wa kisanii, na jamii haijalazimishwa kusikia maneno makali pale pasipostahili.

Tatizo, huko Tanzania, kwenye nyimbo zenye maneno makali, hatuna kitu kinaitwa "radio version". Kila wimbo ni "explicit lyrics" version inapigwa sehemu zote, kuanzia redioni mpaka shuleni.
Mimi kama 'DJ' hapa nimekuelewa zaidi
 
Back
Top Bottom