Sports Arena ya Wasafi FM ni moja ya kipindi cha hovyo cha michezo Bongo

Sports Arena ya Wasafi FM ni moja ya kipindi cha hovyo cha michezo Bongo

Mimi kile kipindi huwa nakisikiliza kwa sababu ya George Ambangile, ila naona kama hapewi dakika za kutosha za mimi kusikia madini yake.

Nimeacha kwa muda kuwasikiliza.
Sahihi kabisa mkuu,utakuta George anachambua kiufundi ghafla anatokea Momo anaingiza maneno mpaka jamaa anasahau alikuwa anazungumzia nini...hawampi muda kabisa
 
Redio ziko nyingi,sio lazima uwasikilize
 
Sahihi kabisa mkuu,utakuta George anachambua kiufundi ghafla anatokea Momo anaingiza maneno mpaka jamaa anasahau alikuwa anazungumzia nini...hawampi muda kabisa

Kwangu George ni mchambuzi pekee ninayeweza kumsikiliza muda wowote akichambua soka Tanzania.

Jamaa anajua.
 
Na wewe unayeweka nukta kwanza alafu ndio unashangaa? 🙂 sawasawa,punguza ujuaji ilhali na wewe hujui,khaaaaaa
Nikurudishe darasani?
unapoweka alama ya koma acha nafasi ndio uandike neno jingine sawa eeeh?
 
Wengine wote pale wanajua kusimulia kilichotokea uwanjani,ila George anachambua soka na anajua

Kwa kweli jamaa anajua, mara ya kwanza kumsikia akiwa Magic nilijikuta napenda kusikiliza kipindi chao kabla hata sijamfahamu jina.

Baadae nikaona topic humu ya kumhusu, ndo kujua kumbe kuna wana kibao wanamwelewa.
 
Wewe kweli ni mtu wa hovyo kuwahi kutokea yaani unanilazimisha kuuliza!!kama lengo langu lilikuwa kushangaa je?khaaaaa
Rekebisha hapo nilipo bold kwa red kama hutagundua makosa yako niambie I'm hia hia tu tichi yu!
 
Nikurudishe darasani?
unapoweka alama ya koma acha nafasi ndio uandike neno jingine sawa eeeh?
lugha ni art, na kila mtu ana swaga zake za kiundashi, usiishi kwa kukrem, don't take everything serious, life is very simple, kama mimi uandishi wake unanipa attention ya kusoma na tukaelewana, hilo ndiyo dhumuni la lugha, hayo ma grammar yako peleka kwa wanafunzi wako shuleni, humu watu wamesoma tena huyo unayemkosoa si ajabu akawa profesa wa kilimo somewhere, acha ujuaji.
 
Labda niweke wazi kuwa sina chuki hata chembe na hiki kituo cha redio na wala sina utimu mimi....ila ukweli lazima usemwe ili ikiwezekana mabadiliko yafanyike.

Awali kipindi hiki kilipoanzishwa niliahidi kuwa mdau mkubwa wa kipindi hiki cha michezo lakini kadri siku zinavyozidi kwenda nilianza kuwa mvivu kusikiliza kipindi hiki.

Nadhani nilivutiwa na majina yaliyosajiliwa kina Eddo, Kitenge, Kawambwa, Mkule, Abdallah n.k nikawa na matarajio makubwa sana lakini sasa nimegundua kuwa hiki kipindi hakina tofauti na timu ya taifa ya Argentina ambayo ina ma-pro wakutosha lakini mafanikio 0.

Kinachokera hawapo vizuri katika kusimamia agenda zao za kipindi
Wanaweza kusema kuwa leo wataongelea jambo fulani lakini katikati ya majadiliano mwingine analeta jambo lingine kabisa na wote wanatoka katika mjadala husika na kuingia katika mjadala mpya pasipo kumalizia ule wa awali.

Na hili linatokana na kujazana sana hapo studio matokeo yake kila mmoja anataka asikike,kuna haja ya kupunguza watu hapo studio wakabaki wachache tu ili utlivu na usikivu uwepo,kwa mfano huyu Ricardo Momo sijui anafanya nini hapo maana hamna lolote analolijua katika soka zaidi ya stori za Liverpool tu; yeye akiwa anazungumzia mada zake mifano yake ni VVD, Salah, Bob Filmino na Mane.

Punguza huyooooo huyu Eddo Kumwembe ni mzuri katika magazeti tu lakini huku anapuyanga tu na kujaza wingi tu, anzisheni gazeti la Wasafi mumpe page yake huko.

Kipindi ni cha hovyo sana siku hizi limekuwa kama maskani ya masela au kijiwe cha kahawa, wana mkusanyiko wa watangazaji na wachambuzi wazuri lakini teamwork 0.0000

Mumeachwa mbali sana na EFM, MAGIC na EA Radio
Acha roho mbaya na chuki
 
Back
Top Bottom