Sports Arena ya Wasafi FM ni moja ya kipindi cha hovyo cha michezo Bongo

Mimi kile kipindi huwa nakisikiliza kwa sababu ya George Ambangile, ila naona kama hapewi dakika za kutosha za mimi kusikia madini yake.

Nimeacha kwa muda kuwasikiliza.
Sahihi kabisa mkuu,utakuta George anachambua kiufundi ghafla anatokea Momo anaingiza maneno mpaka jamaa anasahau alikuwa anazungumzia nini...hawampi muda kabisa
 
Redio ziko nyingi,sio lazima uwasikilize
 
Sahihi kabisa mkuu,utakuta George anachambua kiufundi ghafla anatokea Momo anaingiza maneno mpaka jamaa anasahau alikuwa anazungumzia nini...hawampi muda kabisa

Kwangu George ni mchambuzi pekee ninayeweza kumsikiliza muda wowote akichambua soka Tanzania.

Jamaa anajua.
 
Nilichokiona ni kwamba mtoa mada ana chuki na habari za liverpool, mengine ni mbwembwe tu na unafiki
Umenielewa vibaya mkuu,maana mimi ni shabiki wa kutupwa wa Liverpool,huku mtaani wananiita Momo Sissoko
 
Na wewe unayeweka nukta kwanza alafu ndio unashangaa? 🙂 sawasawa,punguza ujuaji ilhali na wewe hujui,khaaaaaa
Nikurudishe darasani?
unapoweka alama ya koma acha nafasi ndio uandike neno jingine sawa eeeh?
 
Wengine wote pale wanajua kusimulia kilichotokea uwanjani,ila George anachambua soka na anajua

Kwa kweli jamaa anajua, mara ya kwanza kumsikia akiwa Magic nilijikuta napenda kusikiliza kipindi chao kabla hata sijamfahamu jina.

Baadae nikaona topic humu ya kumhusu, ndo kujua kumbe kuna wana kibao wanamwelewa.
 
Wewe kweli ni mtu wa hovyo kuwahi kutokea yaani unanilazimisha kuuliza!!kama lengo langu lilikuwa kushangaa je?khaaaaa
Rekebisha hapo nilipo bold kwa red kama hutagundua makosa yako niambie I'm hia hia tu tichi yu!
 
Nikurudishe darasani?
unapoweka alama ya koma acha nafasi ndio uandike neno jingine sawa eeeh?
lugha ni art, na kila mtu ana swaga zake za kiundashi, usiishi kwa kukrem, don't take everything serious, life is very simple, kama mimi uandishi wake unanipa attention ya kusoma na tukaelewana, hilo ndiyo dhumuni la lugha, hayo ma grammar yako peleka kwa wanafunzi wako shuleni, humu watu wamesoma tena huyo unayemkosoa si ajabu akawa profesa wa kilimo somewhere, acha ujuaji.
 
Acha roho mbaya na chuki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…