Sri Lanka: Wananchi wayatumbukiza kwenye maji, wayachoma magari ya kifahari ya wanasiasa kisa ugumu wa maisha

Sri Lanka: Wananchi wayatumbukiza kwenye maji, wayachoma magari ya kifahari ya wanasiasa kisa ugumu wa maisha

Ni tukose sote mkuu

Hapo Wote mnakuwa wahalifu, wao wanakuwa corrupts na ninyi mnakuwa transgressors--- mbele ya sheria kila mmoja anayo mashitaka yake na hata mbele ya Mungu pia kila mmoja anayo mashitaka yake.
 
Hapo Wote mnakuwa wahalifu, wao wanakuwa corrupts na ninyi mnakuwa transgressors--- mbele ya sheria kila mmoja anayo mashitaka yake na hata mbele ya Mungu pia kila mmoja anayo mashitaka yake.
Haiwezekani wao wafe njaa halafu waliowaletea majanga waendelee kufaidi walivyoiba
 
Saafi, binadamu wakipata madaraka wanakuwa wabinafsi sana. Tz tunachakujifunza hapo.
Hebu rudia tena? Wapi? Tulishalogwa kule Bagamoyo Mlingotini kuna Kisima kimoja kiongozi alitumbukizwa huko. Nasi bongo zetu ziko ndani kisimani mule. Mpaka tukombolewe kwa miujiza. Hahahaha
 
Wapumbavu hao wananchi, kwanini wanachoma magari??!! Badala ya kiyapiga mnada na pesa zinazopatikana zitumike kwa ajili ya shughuli ya umma!!!.
We unaweza kutoa pesa yako kununua gari ambayo haina card?

Au shamba lenye mgogoro?

Hamjifunzi kwa makonda na GSM?
 
Wapumbavu hao wananchi, kwanini wanachoma magari??!! Badala ya kiyapiga mnada na pesa zinazopatikana zitumike kwa ajili ya shughuli ya umma!!!.
Si bora yao wapumbavu wewe si ndiyo matako kabisa ambaye hujachukua hatua yeyote hadi sasa!!
 
Wapumbavu hao wananchi, kwanini wanachoma magari??!! Badala ya kiyapiga mnada na pesa zinazopatikana zitumike kwa ajili ya shughuli ya umma!!!.
Utapiga mnada, nani atanunua wakati wananchi wameamua kutoa adhabu kwa mafisadi? Wanunue halafu yachomwe?
 
Utapiga mnada, nani atanunua wakati wananchi wameamua kutoa adhabu kwa mafisadi? Wanunue halafu yachomwe?

Hiyo sio adhabu kwa mafisadi bali ni adhabu kwa jamii, adhabu kwa mafisadi ni ama afungwe au mali zake za kifisadi zinataifishwa na yeye anatumikia adhabu, kuharibu mali ni uhalifu mwingine huo, mali inaharibiwa imefanya kosa gani???---- mali inaharibiwa pale mali hiyo inapokuwa ni kitu cha hatari kuendelea kuwepo katika jamii.
 
We unaweza kutoa pesa yako kununua gari ambayo haina card?

Au shamba lenye mgogoro?

Hamjifunzi kwa makonda na GSM?

Kuharibu mali isiyokuwa hatarishi ni Makosa, mali hadi inaharibiwa imefanya kosa gani??--- Watu waliofanya makosa na kujipatia hizo mali haramu mnawaogopa kinyume chake mnakwenda kushambulia mali ambazo wala haziumi bali mnawapa nafuu hao wakosefu kwa kumaliza hasira zenu juu ya mali walizochuma badala ya kumaliza hasira zenu juu ya hao wakosefu i!!, Mafisadi wenafanya makosa na wananchi wao pia wanafanya makosa hapo sasa unaona wote wanakuwa ni wakosefu yaani mmoja kajipatia mali kihalifu na mwingine kaharibu mali kihalifu.
 
Haiwezekani wao wafe njaa halafu waliowaletea majanga waendelee kufaidi walivyoiba

Sasa kuharibu mali sio suluhisho bali inatakiwa walioiba ndio wahukumiwe ili wasitokee wezi wa aina hiyo tena.---- Mali inaharibiwa imefanya kosa gani???, Mali ni mali yenu iliyopatikana kifisadi anayetakiwa kuhukumiwa ni yule aliyeiba na kujipatia hiyo mali, kuharibu mali ni dalili ya UWOGA wala sio njia ya kutibu ugonjwa wa ufisadi.

"Angalia ulipojikwaa wala usiangalie ulipoangukia"---- kuharibu mali ya kifisadi ni kuangalia ulipoangukia.
 
Wapumbavu hao wananchi, kwanini wanachoma magari??!! Badala ya kiyapiga mnada na pesa zinazopatikana zitumike kwa ajili ya shughuli ya umma!!!.
Jaribu kutumia akili kidogo, yaani mali sio yako utaiuzaje na huyo mnunuzi atakuwa mjinga kiasi gani kununua mali iliyotokana na maandamano ya wananchi,?dawa ni kufanya kama walivyofanya tu.
 
Jaribu kutumia akili kidogo, yaani mali sio yako utaiuzaje na huyo mnunuzi atakuwa mjinga kiasi gani kununua mali iliyotokana na maandamano ya wananchi,?dawa ni kufanya kama walivyofanya tu.

Akili kubwa ni: Kuharibu mali ni woga na uhalifu pia, mali inaharibiwa imefanya kosa gani??--- kosa afanye mtu adhabu ipewe kitu??!!--- hiyo ndio akili unayojivunia nayo??!!.

Hao mafisadi ni wahalifu na njia ya kuharibu mali za kihalifu sio njia ya kutibu uhalifu, njia ya kutibu ni kupambana na wahalifu wenyewe kwa njia za kisheria na kama njia hizo ni corruptive basi kuharibu mali ni ujinga kwani halitanzui kiini cha matatizo hadi pale mambo hayo yatakaporekebishwa, kuharibu mali in that case ni mob justice driven by mob pyschology na hakuna mob pyschology inayoleta + ve results. Watachoma mali leo kesho ananunua mali nyingine kuwaonyesha kwamba wao ni wapumbavu kwani hao watu corrupts wanazo pesa kibao za kifisadi.
 
Back
Top Bottom