TANZIA SSGT Reginald Ruta wa JWTZ amejiua kwenye Kaburi la marehemu Mkewe

Daa Mungu atusaidie, wengine tukiwa na nyumba ya kuishi na ka usafir naona dunia yangu wengin wananyumba za ziada bado usafiri wa ziada upo na anaona dunia imemdhulumu. Hakika tumwombe alietuumba atupe tu utulivu wa nafsi. Kwa sababi bila hili hakika ndio mtu anaishia kufanya maamuzi kama haya
 
Ni muhimu sana wajeda wakashiriki vitani sehemu mbali mbali!

Ova
 
Basi ni laana maana kuna wanawake wakifa kwenye mateso ya ndoa yanayotokana na mume basi husema kabisa nikifa huyu mtu hachukui round atanifuata na inakuwa kweli.
Ndo hicho kilichotokea.
Babangu alikuwa mjeda so I know, hawa watu kuua au kujiua ni mara moja tu
 
Duh! Huyu alikuwa anampenda sana Mkewe. Hakustahili kuachwa peke yake hata kwa dakika chache. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi 🙏🏾🙏🏾🙏🏾
 
Kipo alichokikosa kwa mkewe huku akiamini hawezi kuishi bila yeye, na mbaya zaidi akakosa hata faraja ya walimwengu
Afande huenda alikuwa maryo! Hivihivi haiingii akilini kwa mtu wa umri wake kujipiga risasi as simple as that. Angekuwa kijana mdogo sawa, mzee tena mwenye wajukuu?! No.
 
Kabisa Mkuu ndiyo sababu vifo vya Mzazi, Mke/Mume na mtoto huitwa misiba mikubwa kwani wahusika 9/10 times huumia zaidi wanapofikwa na misiba ya hawa watu.
Maumivu ya moyo wewe acha tu
 

Hakuna mtu anajiua kwasababu ya kukutwa na VVU siku hizi!!! Ukimwi sio passport ya kifo tena; kuna dawa watu wanakunywa na wala huwezi jua kuwa wameathirika.
 
Afande huenda alikuwa maryo! Hivihivi haiingii akilini kwa mtu wa umri wake kujipiga risasi as simple as that. Angekuwa kijana mdogo sawa, mzee tena mwenye wajukuu?! No.

Inawezekana kilichommaliza ni kwamba yeye kazi yake ilikua kutafuta pesa na wife alikua mhasibu mkuu na bibimanunuzi mkuu wa familia..... Na inawezekana hapo alipojiua alikua hajui hata zinakokaa socks na boxer zake..... inawezekana hajuagi hata bei ya vest wala chupi, yeye anachojua ni kutafuta pesa tuuu

Wewe unaweza kuviona vidogo ila kwake ni mzigo mkubwa sana tena usiobebeka
 
Hakuna kitu kama hicho ni Obsession tu, TZ yote hii akosekane mwanamke mwingine wa kupanga bajeti!!
 
Dah, poti kazingua sana. Ila poa tu .
Hivi Mshana Jr hujawahi kuwa pale milambo barracks na jamaa mmoja alikuwa anaitwa zero zero? Alikuwa MP then akajoin kufanya mortuary
 
Hii ni depression lakini kibongobongo tunaichukulia poa kisa mjeshi lazima awe na roho ya chuma.
Comments za baadhi ya watu humu zimenifanya niache kusoma huu uzi..watu wanahukumu ile mbay hadi moyo unaniuma

Watu hawaoni jinsi huyu mtu alivyopata sonona kwa kufiwa
Huwezi jua waliishi vipi na mkewe

msione watu wanatembea jmn
Watu sio wazima.,kila mtu anajua msalaba wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…