Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu asikuambie mtu kada ya watu wanaonyanyaswa kimapenzi ni hao jamaa wa bakabaka.JW nao mapenzi yanawatesa aisee, zile "mbwembwe" zote za ugumu kumbe mdudu penzi haziogopi
R I P mjeshii
Few of themIla siyo wote, Wanawake wengine ndiyo wanakuwa ma jinamizi wakubwa kwa Wanaume!!
Mkiambiwa muwe na michepuko hamsikii, ona sasa. Anakosaje mke mdogo wa pembeni? Hili ni tatizoKwa ambaye anamfahamu SSGT Ruta alikuwa Msata amejiua kwenye kaburi la mke wake ambaye alifariki siku ya Jumamosi huko kilakala kaacha ujumbe kuwa alikuwa anampenda mke wake.
========
Dar es Salaam. Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Reginald Ruta amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa juu ya kaburi la mkewe, Godebertha aliyezikwa katika makaburi ya Mekyuri Kipawa jeshini mkoani Dar es Salaam.
Juni 7, mwaka huu mwili wa askari huyo aliyezikwa katika makaburi hayo jana, ulikutwa katika kaburi la mkewe aliyefariki dunia Alhamisi iliyopita baada ya kuugua ghafla.
Kifo cha askari huyo wa kambi ya Msata mkoani Pwani kimeacha simanzi kwa ndugu, jamaa na marafiki, kwa kuwa kilitokea siku tatu tangu mkewe afariki.
Akisoma risala kwenye ibada ya kuaga mwili wa askari huyo, iliyofanyika nyumbani kwake mtaa wa Karakata Kipawa, diwani wa Karakata, Idary Karugendo alisema marehemu ameacha watoto wanne na wajukuu watano waliokuwa wanamtegemea.
“Mzee Ruta alikuwa tegemeo kwenye familia yake kama baba, hasa baada ya kifo cha mke wake kutokea siku chache zilizopita,” alisema Karugendo.
Akizungumza katika ibada hiyo, Katekista wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Kipawa, Silivester Sadick alisema kifo hicho ni funzo kubwa kwa watu wote na kinaonyesha wazi hakuna binadamu mkubwa mbele ya Mungu.
“Juzi tulikuwa hapa hapa, tena nawaongoza kwenye ibada ya kumuaga mke wake, hakuna aliyekuwa anajua nani anafuata lakini leo mzee Ruta anafuata, ni funzo kubwa ndio maana nawakumbusha kuzidi kumuomba Mungu wakati wote,” alisema.
Alisema kifo kinaharibu mipango yote ambayo binadamu anakuwa amejipangia kuitekeleza na ndiyo maana watu husema kifo hakina huruma, lakini ukishakufa unakwenda kwa Mwenyezi Mungu.
“Maisha ya hapa duniani yanapita, juzi tulizungumza hatujui nani anafuata, lakini mume ameenda, kama maisha yetu yako namna hii binadamu ni nani mbele ya Mungu.
Familia ipo kwenye wakati mgumu, kama ingekuwa ni mimi leo ingekuwaje, kikubwa tujitengenezee njia ya kufika mbinguni mapema na naiomba familia kuzidi kufanya maombi na kusimama katika imani kwa Mungu kwani hawezi kuwaacha,” alisema.
Kifo kilivyotokea
Kwa mujibu wa jirani mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake, alidai kuwa walikuwa wote na Ruta siku ya Jumamosi ambayo yalifanyika mazishi ya mkewe aliyefariki ghafla wakati akijiandaa kwenda kazini.
Alisema baada ya mazishi Jumatatu iliyopita, vijana waliokuwa wanachunga mbuzi waliukuta mwili wake juu ya kaburi hilo.
Chanzo hicho kilieleza kwamba watoto hao baada ya kuona mwili huo wakaenda kutoa taarifa jeshini kwa sababu eneo hilo linamilikiwa na Jeshi na walipofika pale wakampekua hawakuona chochote zaidi ya kitambulisho chake.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya mazishi ya mkewe, Jumapili iliyopita Ruta alifanya vikao vya mara kwa mara na watoto wake wanne na kuwaeleza mali alizonazo na sehemu zilipo.
“Baada ya kufanya vikao virefu na watoto wake huku akiwachekesha muda wote, aliwaambia kuwa atakwenda kununua marumaru kwa ajili ya kujengea kaburi la mkewe na aliwaeleza kuwa akishafanya manunuzi atawaeleza,” zinaeleza taarifa hizo.
Habari zaidi zinaeleza kuwa alimuomba mwanaye mmoja ampe Sh50,000 kwa ajili ya kununua marumaru hizo na alipopewa fedha hizo aliondoka nyumbani hakurejea tena.
Polisi wanena
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Ilala, Janeth Magomi alikiri kupokea taarifa ya kifo na kudai ililetwa na wanajeshi wenzake kutoka kituo cha Polisi Stakishari.
“Kwamba kuna mwenzao wamemkuta amefariki juu ya kaburi la mkewe, wakati wanatoa taarifa hiyo tayari mwili ulishachukuliwa na kupelekwa hospitali ya Lugalo,” alisema Janeth.
View attachment 1815077
View attachment 1815080
Dah..nimeshindwa kbs kuvaa viatu vyako...kweli ww mkomavu! Hongera ..sio pole tenaHiyo situation ilitaka kunitokea mwaka fulani ndani ya huo mwaka nilifiwa na mama mzazi, first born pia na mke the same year ona sasa dunia ilivyonielemea kwa majanga ujasiri uliniisha
Upo sahihi kabisa. Nilisema vile kwa sababu niliamini ktk umri wake ule ameshashudia mambo mazito ikiwemo hata vifo vya ndg zake wa karibu kiasi kwamba moyo na ubongo vimeshakuwa na uwezo kuhimili mambo mazito!Inawezekana kilichommaliza ni kwamba yeye kazi yake ilikua kutafuta pesa na wife alikua mhasibu mkuu na bibimanunuzi mkuu wa familia..... Na inawezekana hapo alipojiua alikua hajui hata zinakokaa socks na boxer zake..... inawezekana hajuagi hata bei ya vest wala chupi, yeye anachojua ni kutafuta pesa tuuu
Wewe unaweza kuviona vidogo ila kwake ni mzigo mkubwa sana tena usiobebeka
Basi itakuwa shuntama, wife kaondoka nalo mzee akaona akaifuatie hukohukp.Mtu ana Nyumba tano,gari 4 huyu anakuwaje Marioo!?
Basi itakuwa shuntama, wife kaondoka nalo mzee akaona akaifuatie hukohuko.Mtu ana Nyumba tano,gari 4 huyu anakuwaje Marioo!?
Hujapenda wewe...hata mimi naweza jitoa uhai kwaajili ya mapenzi...wee acha kbs!ndo maana kasema wanaye wamsamehe
Hapa ilikua Chalamila style, sikumaanisha yaliyoandikwa na vidole vyangu.Nakusoma kwa makini soulmate wangu
Hahaha yuko wapi huyu jamaa aisee. Kitambo kweli sijasikia hbr zake[emoji2][emoji2][emoji2] namfahamu vizuri tuu
Aisee mimi mwenyewe ni almost two years sijamsikiaHahaha yuko wapi huyu jamaa aisee. Kitambo kweli sijasikia hbr zake
Mimi hata kwenye usugu nimepita.. sijui niko stage gani nw🤣🤣Nilikuwa na mawazo kama ya kwako, na nilikuwa pia na hisia kama za kwako, ila kwa sasa nishakuwa sugu[emoji81][emoji23], yaani ni kama ambulance vile unalia huku safari inaendelea.
Yaani amekutwa tuu amekufa juu ya kaburi kwa kuugua ghafla?
Njia pekee ninayoiona ni yeye kunywa sumu na kulala/kwenda hapo kusubiri kifo, japo kutetea hoja hii inahitaji nguvu...
Halafu wamelizika na kuamua kumzika fasta tuuh??
Anyway R.I.P.