Stan Katabalo: Tunauhitaji mzimu wako wa habari za Uchunguzi!

Tungepata mtu anaejua mjane aliko angekuwa anatunzwa jamani umenikumbusha mbali sana, alifia msumbiji kwenye ule mkutano sijui ulikuwa wa nini!!
Nawafahamu watoto wake watatu Charles , Kazaula na Rweyemamu kuna kaka yake na marehemu anaishi kibaha elimu sehemu moja inatwa Mwanalugali pia kuna mdogo wake na Marehemu Katabalo inatwa Mzee Slivesta Katabalo alikua mwalimu wa Shule ya Secondary Nyakato nje kidogo ya mji wa bukaba Mjini anaishi kijiji kimoja kinatwa Buhembe ukifika Nyakato ukaulizia familia ya Katabalo utapelekwa.
 
Sasa tunaye Magufuli
 
Haya magazeti yapo kweli tena?...hivi magazeti yaliyo kwenye mrengo wa ukosoaji mfano Raia mwema (ambayo wewe ni mwandishi wa makala humo) hufanya pia habari za kiuchunguzi ?
Kwa sasa gazeti la Jamhuri la kina Manyerere Jackton ndio wamejipambanuwa kuandika habari za uchunguzi lakini tatizo kubwa naliona ni resources.

Huwezi kufanya investigation journalism huku una njaa na unatamani bahasha za kaki, hawa watu wanahitaji grants za kuwawezesha kufanya kazi bila kutegemea takrima kutoka kwa mtu.

Sasa hivi tuna waandishi wanazurula tu mitandaoni kuokoteza habari then wanaunganisha tayari news room.

Ndio maana ukimuuliza Mtanzania mgogoro wa Urusi na Ukraine atakueleza vizuri, lakini ukimuuliza tatizo la Ngorongoro na Loliondo ni nini hawezi kukupa majibu kwa sababu hajui lolote, ni kwa nini hajui lolote ni kwa sababu wenye jukumu hilo la kuupa umma ukweli wa mambo wamekimbia majukumu yao.

Sasa hivi kila siku kuna press za machawa tu, Haji Manara, Mwijaku na Baba Levo na waandishi wanafurika, hawa machawa ni kila siku wanaita press mahotelini.

Powered by bahasha ya kaki.
 
Nimeguswa!.
RIP Stan Katabalo.
P
 
Kashfa ya Loliondo ilitufundisha mengi,tulijua kuwa wawekezaji uchwara walipokuja mara ya kwanza - Loliondo 1 hawakwenda Bungeni bali nyumba nyeupe; waliporudi tena kwenye Loliondo - 2 hawakwenda Bungeni bali nyumba nyeupe, na mwaka ule alipokuja tena mwana wa Zayed hakwenda Bungeni bali nyumba nyeupe! Nyumba nyeupe ndio mlango wao rahisi kabisa na ndio wamekuwa wakiutumia,kama nyumba nyeupe wakitaka kubadilisha sera wanaweza! RIP Stan Katabalo.
 
Raisi Mwinyi ndio aliamrisha kuuawa kwa Stan Katabalo ! Full stop ! Na sasa raisi mchongo Samia anaamrisha wamasai wa Ngorongoro wauwawe ! Period !!!
 
Kuna ukweli kadhaa katika maandishi yako ingawa pia Kuna uongo mwingi Sana.Ni kweli kwamba Kabendera alijitosa ziwa Victoria na kufariki Dunia.Kabendera alizaliwa na kukulia Kagera,alihamia Rwanda baada ya RPF ya akina Kagame kuchukua madaraka.Akiwa huko ndo alitofautiana na Kagame na ikabidi arudi Kagera .Alikamatwa anajiandikisha kama mpiga kura.Akafunguliwa kesi kwakuwa alishaukana uraia wa Tanzania.Kwa kipindi kirefu Kabendera alikuwa mwandishi wa BBC bila shida.Kabendera asingeweza kukaa makambini ilihali asili yake ni Katoro hapo Kagera ,alichoharibu ni kuchukua paspot ya Rwanda.Ni kosa kubwa kumhusisha Kabendera na mauaji ya kimbari ya Rwanda na pia kumhusisha na Habyarimana ni kumkosea Kabendera.
 
Mkuu balibabambonahi , asante sana for this, marehemu watendewe haki. Hivyo huku ni kumtendea haki Kabendera Shinani.
P
 
hivi ni mfanyakazi au motomoto hebu tuwekane sawa sababu ni kitambo.
 
CCM watakuwa walipita naye kama kawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…