Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Muulizie yule engineer mkuu wa kulitia taifa hasara kila agusacho inatakiwa apewe tuzo.Hivi wakati wanajenga ile ofisi pale jangwani kipindi chote cha ujenzi haijawahi kunyesha mvua wakaona mafuriko au ndio akili za wasomi ziliganda kama uji wa cement [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Maana unaweza kufikiri wakati wooote wa ujenzi wa zile ofisi na yard basi hapakuwahi kunyesha mvua zikafurisha eneo.
Watanzania ni viumbe wazito sana sijui tu. Hata na UDART wenyewe wamerudi kwenye ticket za vishina .
Saa nyingine unaamua kusahau kila kitu ila kuna kodi nilikatwa kwenye pato langu imechezewa pale ndio maana akili yangu haikubali kusahau kabisa. [emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25]
Kilometa 30 ongeza na ufinyu wa barabara patakuwa mbali mno. Ubungo terminal tunatumia barabara 2 kuingia na kutoka lkn alfajiri unaweza kujikuta unaachwa na basi ukiwa kwenye foleni kwenye traffic light.Mbezi louis ni karibu sana, labda unakaa Mbande au Kimbiji wewe. Kutoka city center, mbezi bado mi karibu sana. Mji wa Dar umekua sana.
Wanachojali 10% hawajali hata tukikosa dawa,hela haziwatoshi,hapo bado za stella George umeme wa maji.Sisi wengine ni wasindikizaji tu kwa wala keki ya taifa.Umeona eeh. Halafu walipiga marufuku watu kujenga wala Kuishi maeneo hayo wakayaita hatarishi.
Wanachezea pesa zetu sana halafu zisipoonekana kwenye hesabu za CAG wanakuwa wakali wanadai zipo. Zitakuwepo vipi kwa kuchezewa huko
bado na ukuta wa Mererani wamechezea pesa yetu. [emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]
Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo haraka (UDART), kilichopo Jangwani na kupeleka kwenye kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo UBT, kutokana na eneo hilo la Jangwani kujaa maji kila mara wakati mvua zinaponyesha.
Picha ya chini ni mchoro wa kituo kipya cha mabasi ya mikoani kitakachojengwa Mbezi Luois jijini Dar es salaam.View attachment 771061View attachment 771062
Na kule Kibaha jirani na TAMCO, kuna ujenzi wa stand unaendelea baada ya kuhamisha wafanyabiashara wa Maili Moja! Kibaha wamebahatika, wilaya moja itakuwa na stand 2 za kwenda mikoani! Yaani hapa lazima tuunge mkono juhudi hizi za Maendeleo!Sasa kituo kikipelekwa Kibaha, kitakuwa cha Dar au Mkoa wa Pwani?
Nimecheka sana! Ukiwa DSM afu unataka kwenda MOROGORO, unaenda kupandia Msamvu?Wangefanya msamvu ndo iwe stendi ya mikoani. Haina shida.
Nchi zinazoendelea zinapata Pesa nyingi sana kuliko za ulaya shida iko kwenye mipango ya maendeleo ndo tunashindwa na kutupa pesa nyingi kusiko na tija,sababu project zinapangiwa ofisini hazishirikishi watumiaji matokeo yake nyingi zinabuma kama ilivobuma machinga complex.Je jangwani patabomolewa?? VERY POOR PLANNING!
Na pia daraja la wavuka kwa miguu pale Ubungo bus terminal litakuwa linatumika kwa madereva ma staff wa udart kuvuka??
Tetesi za stendi kuhamia Mbezi ni za muda sasa, labla hata mwendokasi haujakamilika, sielewi kwa nini waliweka lile daraja uelekeo wa ndani ya syendi ya mkoa. Pesa hiyo ingejenga zahanati mahali kuliko ilivyotupwa pale maana ni wazi upande huo wa daraja hautakuwa na tija.
Dar hakuna umbali wa Chanika anapitia kinyerezi ni karibu kuliko Buguruni, na wa goba anapita juu kwa juu wa mbagala kuna miradi wa mwendokasi atawahi tu wengine unakuja kulala stand waweke huduma zote muhimu na sehemu za kulala, pia wahakikishe iwe na reserve ya eneo kubwa kwa ajili ya upanuzi wa baadae maana wakichelewa tu maghorofa yatachipuka kama uyoga.Unatumia mfano wa City center ndio unasema karibu.
Mbona huzungumzii mtu wa Gongo la mboto, Temeke, Chanika.
Hili jambo liangaliwe tena tusije kujilaumu tena baadae.
Hii stand bora waigawe, nyingine iwe kule Temeke(nadhani hii ipo tayari) kwa magari yaendayo mikoa ya Mtwara na Lindi.
Nyingine iwe Tegeta kwa magari yaendayo Tanga, KLM, Arusha, Manyara via Moshi.
Halafu hii ndio wailete Mbezi Louis.
Lakini bado kutakuwa na adha pia ya mtu anayeishi mbezi(Goba) akitaka kusafiri kwenda Mtwara na pia anayeishi Chanika akitaka kusafiri kuelekea mikoa mingine ambapo inabidi akapande gari Mbezi Louis.
Hivi, what's the point kupeleka stand nje ya mji? Hata hatuwezi kujifunza kwa walioendelea?
Tunadhani solutions ni kutoa stand Ubungo kupeleka nje ya mji but that's not, solution ni kutengeneza miundombinu inayokidhi, hata stand ingekuwa Kisutu, kama miundombinu ya barabara ipo vizuri hizo foleni tutazisikia tu.
Tuendelee tu kuhamisha stand, mwisho zitakuwa Chalinze.
Kimiundo mbinu bado tuko nyuma sana hivyo kwa sasa hatuna budi bali ni kusogea nje ya mji.Hivi, what's the point kupeleka stand nje ya mji? Hata hatuwezi kujifunza kwa walioendelea?
Tunadhani solutions ni kutoa stand Ubungo kupeleka nje ya mji but that's not, solution ni kutengeneza miundombinu inayokidhi, hata stand ingekuwa Kisutu, kama miundombinu ya barabara ipo vizuri hizo foleni tutazisikia tu.
Tuendelee tu kuhamisha stand, mwisho zitakuwa Chalinze.
Haya maneno ya JK, si ndio??"....kabla hawajaanza ujenzi, walinletea Ombi, wakitaka ruhusa ya kujenga pale Jangwani. Nikawakatalia kwa maelezo kuwa pale hapafai na si salama...... siku moja nikawa napita pale (Jangwani)..... nikakuta kuna pilikapilika nyingi..... nikauliza, kuna nini pale? Nikajibiwa: Kituo cha Mwendokasi, nikashangaa sana, nikasema ngoja ninyamaze Mswahili Mimi"
Pia ingekuwa vizuri sana mwendokasi ndo ziende mbezi ,Ubungo ibaki ya mabus pale ni centa kwa wengi,maana mwendokasi hata yard iwe mjini lazima aende mbezi akafate watu.Hivo ni bora yard yao iwe mbezi iamkie na kulalia huko huko mwisho wa ruti yake.Hii iko poa sana kama planner wakiizingatia.Kwa nini hao mwendo kasi wasipelekwe huko Mbezi! Wabongo bwana ni shida, yote hii ni kumuongezea shida mlalahoi, nitoke Kigoma, nilale Morogoro, nifike Mbezi nianze safari nyingine ya kwenda Mbagala viongozi hamlioni hili?
Halmashauri ya jiji hawawezi ruhusu kitoke nje ya Dar, wanajua wanapata mapato mengi sana! Kibaha, haitawezekana kukipeleka.Sasa kituo kikipelekwa Kibaha, kitakuwa cha Dar au Mkoa wa Pwani?
Hawa wasomi wetu ndio chanzo cha matatizo kwa asilimia kubwa.