Stephen Wassira: Watanzania wamemuelewa na kumuunga mkono Rais Samia; wanasema kiwango chao cha furaha kimeongezeka

Stephen Wassira: Watanzania wamemuelewa na kumuunga mkono Rais Samia; wanasema kiwango chao cha furaha kimeongezeka

Furaha lazima iwepo kwa wezi, wasiopenda kuambiwa kweli, wenye kutakabari, wenye ubinafsi, wanaojiwazia wao, wasiopenda kazi, wapenda kuna issue inaisikilizia haoo. By the way Wacha mjipe moyo mda huu ila siku Zaja nazo mtasema kumbe bora yule...
 
Kwa mujibu wa Prof. Assad ni kuwa wote waliokuwa wanamsifu na kumpamba walikuwa wanatafuta fursa!
Na amedai hatuhitaji viongozi wa aina hio! Hatutafika popote yani! We need people with integrity and who stand for the right sio kwenda na upepo tu.

Ndio vinyonga waliojaa serikalini!
 
Mzee Wasira ambaye amekuwa waziri katika serikali tangu uhuru mpaka serikali ya awamu ya nne ya JK amesema Kiwango cha furaha kwa Watanzania kimeongezeka. Ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na Azam TV. Aidha amesema baada ya masikitiko ya muda mfupi kufuatia kifo cha Magufuli nchi imerudi kwenye reli baada ya hotuba za Rais Samia Suluhu Hassan.

Kumbe furaha hii pia imetamalaki ndani ya CCM na wapambe wanafiki wa Magufuli!

===

Akizungumza Apr 9, 2021 kwenye kipindi cha Morning Trumpet kinachorushwa na Azam TV, Mzee Wassira amesema:

"Namwambia nini Rais? Namtakia heri. Namtakia heri aongoze nchi yetu vizuri. Na kitu kimoja ambacho ningependa Rais ajue ni kwamba: kwa hotuba hizi tu, Watanzania wengi wamemuelewa na wanamuunga mkono. Wanasema kiwango chao cha furaha kimeongezeka; kwasababu tumesikitika [kufuatia kifo cha Rais Magufuli] lakini tumerudi kwenye reli."


Mi naona wakongwe wote ambao mfumo uliwatema kwa sababu ya kuchuja kifikira wameanza kutoka mapangoni,lakini pamoja na hayo tumeishaamka,kila siku wanaimba vijana wajiajiri wao bado wana kasumba ya kutaka kuajiriwa,najiuliza swali kuna nini kinachopiganiwa?
mtu unataka mpaka upigane vikumbo ofisini na wajukuu zako hiyo si ni aibu.
Hivi mzee wetu alikuwa mtu kushindania ubunge na akina na Bulaya? Tusipoangalia tutaunga mkono vinyongo vya watu ambao wanaiona serikali iliyopita haikuwaunga mkono ktk mbio zao za kutaka warejee bungeni.
 
Ni Rais pekee ambaye anaishi moyoni mwa watanzania ingawa amelala. Shujaa wa Afrika nzima.
Kwa wapenda maendeleo,lakini walafi akiwemo mzee wetu bado ana machungu ya kushindwa ubunge na mjukuu wake huku akitegemea serikali imsaidie kwenye kesi,akakuta imepiga kimyaaa.
 
Walikuwa wanamuogopa
Kweli kabisa walikuwa wana muogopa. Kwa nini usimuogope mtu ambaye ana miliki kikosi cha WASIOJULIKANA ambacho kina nguvu kuliko jeshi la Polisi. Ukimkosoa tu wanakuja popote na Noah wanakukamata na kukupoteza.

Kwa nini usimuogope mtu ambaye anakupeleka Segerea na kujufungulia mashtaka ya kutakatisha fedha yasiyo na dhamana kisa umemkosoa tu??
 
Back
Top Bottom