Story gani katika kitabu cha dini yako unafikiri ni hadithi ya ngano tu?

Wewe unaweza kunipa ushahidi Abunuwasi hayupo au hajawahi kuwepo?
Au unaweza kunipa ushahidi wale Sungura wanaozungumza kwenye hadithi za watoto hawajawahi kuwepo?
Sijaelewa swali lako.

Unamuongelea Muandishi au ? Lakini mfano wako ni tofauti na habari za Dini. Naomba ulinganishe habari za dini na habari za visa vya Abuu Nuwas ? Huyu alikuwa mshairi mwenye kujulikana,baba yake alikuwa Muarabu na mama yake alikuwa na asili Irani,aliitwa Abū Nuwās al-Ḥasan ibn Hānī al-Ḥakamī.

Ninachokuomba mimi utoe ulingano kati ya habari za Abuu Nuwas na habari za dini,kwa uchambuzi wa kielimu. Ukishindwa nitakusaidia kisha uje ukiri ya kuwa wewe ni mjinga katika hili.
 
Hiyo ni ya Kweli
 
🤪🤣🤣Ni kweli hiyo.

Kipindi cha uimbaji kulikua hakuna sheria ya kutokulala na dada yako. Na Adam watoto wanaojulikana ni wawili tu lakini alikuwa na watoto wengi sana. Kwa hiyo Kaini alimwoa dada yake.
 
Habari za dini yako zina tofauti gani na visa vya Abu Nuwas?
 
Habari za dini yako zina tofauti gani na visa vya Abu Nuwas?
Nimekuuliza wewe swali hilo,unaniuliza mimi tena ?

Jibu swali langu,kama huwezi kiri kisha nine nikuonyeshe utofauti uko wapi.

Hatutaki sanaa na kuendekeza ujinga. Inakuwaje unalinganisha vitu kisha unashindwa kuonyesha ulinganifu wake ? Usikimbie swali.
 
watunzi wa hizi riwaya walikuwa hadi wanajisahau stori zinakuwa kama vile Mungu anafikiri na kutenda kama mwanadam tulivyo! kilaza tu anaweza kuamini biblia na quran kuwa si mila, tamadun na desturi za watu wa mashariki ya kat zilizoandikwa na binadam namna bora waishi. faida za vitabu hivi ni kutuletea hofu itiayo aman na upendo, la tungeishi kama wanyama. ingekuwa ngum mno kutawalana.
 
Naomba nikujibu swali lako kama ifuatavyo.
1, kabla ya kuwepo au kuumbwa kwa adamu mbinguni kulitokea vurugu ambayo majeshi ya malaika yalijigawa, robo tatu ya malaika yakawa upande wa shetani ambaye alitaka kuweka mapinduzi mbinguni na robo iliyo bakia ikabaki upande wa Mungu na mda ambao mapinduzi ya shetani kutaka kuchukua kiti cha Mungu ndo mda ambao Mungu alikuwa yupo duniani kuumba yaani kuyagawanya maji, n.k

Hivyo lile kundi lililo mfuata shetani lilishushwa duniani ila Adamu na eva walifichwa katika bustani ya edeni, na baada ya kutenda dhambi alitoka nje ya bustani na kujitengenezea majani ya miti kama kujistili kutokana na walijiona wapo uji, na kama wewe ni msomaji mzuri wa bible kuna pahara Mungu anauliza Adamu upo wapi, maana kwenye bustani hakuwepo.

Kwa hiyo Kaini alienda kuoa majitu yale ambayo ni malaika waasi kutoka mbinguni na majitu hayo nadhani ndio wa Nefili ambao Mungu aliwaonya kuwa wanadamu wasichangamane na hao majitu wa kuoa / kuolewa.
kama kuna swali nakaribisha
 
Naomba nipe reference katika biblia nasoma wapi hiyo hadithi. Na pia naomba kukuuliza je hao malaika waasi ni watu?
 
Wacha upuuzi wako, nani aliyekuambia Qur'an ni ujumbe wa ulimwengu wote.....usipende kujipa ujinga, una akili za kuzaliwa zitumie.
 
Wacha upuuzi wako, nani aliyekuambia Qur'an ni ujumbe wa ulimwengu wote.....usipende kujipa ujinga, una akili za kuzaliwa zitumie.
Pinga kwa hoja usilete utoto katika mambo ya kielimu.

Amesema Allah muumba wa mbingu na ardhi.

Allah anasema :

1. Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni.(an-Nisaa : 2)

Akasema tena :

47. Enyi mlio pewa Kitabu! Aminini tuliyo yateremsha yenye kusadikisha yale mliyo nayo, kabla hatujazigeuza nyuso tukazipeleka kisogoni, au tukawalaani kama tulivyo walaani watu wa Sabato (Jumaamosi). Na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima ifanyike. (an-Nisaa : 47)

Unahoja ya kukataa kwamba siyo ujumbe kwa watu wote ?
 
Mkuu tutajie huyo aina ya samaki aliyemeza Yunus....??? Tukianzia hapo itakuwa sawa
 
Mkuu tutajie huyo aina ya samaki aliyemeza Yunus....??? Tukianzia hapo itakuwa sawa
Sijui ni Samaki gani. Jenga hoja yako sasa.

Maana kuna maswali ya kipuuzi watu wanauliza,kiasi ambacho hayabadilishi chochote katika tukio zima. Ni sawa uulize wale mbwa walio kiwa pamoja na vijana wa pangoni,walikuwa majike au madume au mchanganyiko. Maswali ya kipuuzi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…