Sisi millennials tupeane story za ujambazi wa kutisha uliotikisa miaka ya 2000 kurudi nyuma
Watu wa mkoa wa Kagera tukumbuke Yale mapori ya Kasindaga na Kimisi,
Pale wahuni waliuwa na kuibia watu kibabe sana
Namkumbuka ilikuwa 1998 nikiwa mdogo mno, nadhani chekechea.
Usiku wa manane kijijini tulivamia na majambazi ambao walivunja mlango Kwa jiwe na kuingia ndani kuiba
Walimjeruhi Mzee Kwa panga usoni na kumuibia pesa elfu 90,000 za mauzo ya kahawa,
Pia wakaiba redio kaseti Ile ya Kanda mbili, pasi ya mkaa, pampu ya kuoshea mifugo na sanduku la nguo
Nikikumbuka Huwa nacheka mno 😄🤣😄yaani jambazi anakesha akaibe redio cassette na pasi
Basi kimsingi tuliumia mno
Kuna kipindi majambazi walivamia gulioni na ku search na kuiba kila kitu pale gulioni kijijini
Aisee ilikuwa story kubwa
Kuna story ya bro akiwa anasoma seminary majambazi wakasimamisha gari pale pori la Kimisi na kuchukua ada yote,
Zamani hazikuwepo benk au huduma za kifedha
Ubabe wa zamani noma sana
Gentleman, unafahamu au unajua chimbuko la umaarufu wa wimbo wa mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe?
basi, ambatana nami kwa uchache nikujuze,
Kuna mahali kuna pori inaitwa Mtungutu hiyo, upande wa kulia kuna mlima umefunga msitu mnene wa maana sana na mawe machache makubwa yanaonekana kichele, kushoto mlima mwingine uko mbali kidogo , ila kuufikia katikati ni msitu msitu kweli wakati huo, huenda mabadiliko ya tabia ya nchi imebadili kitu kwa sasa,
basi bana,
manjambazi kwenye mbinu zao za kutafuta riziki, si wakasambaza magogo ya maana sana katikati ya barabara,
kila basi la abiria au gari lolote lile likija, linapigwa mkono na kuegeshwa kadiri ya maelekezo ya jambazi, utadhani traffic wa ukaguzi wa usalama barabarani vile,
Abiria wote tukashushwa chini moja moja, wakati huo, jamaa wameweka ndoo kadhaa hapo nje ya mlango wa basi, kila moja ajisachi mwenye na kutupia kwenye ndoo kila kitu kinachoitwa pesa au dhahabu kama kutoa sadaka kwenye nyumba za ibada, iwe ni pete au hereni unaambiwa weka kwenye ndoo,
wakati huo, njungu za maana zinafyatuliwa hewani kwa fujo, zinafurushwa bila utaratibu hewani hadi maskio yanaziba kabisa,
na kuraruliwa hewani utadhani mizinga21 ya uapisho wa mkuu wa nchi fulani, acha kabisa gentleman,
namalizia kula cha usiku,
narejea kumalizia tukio,
lema ametoka mbali acheni tu ndugu zangu 🤣