Story za ujambazi wa jiwe Fatuma na utekaji mabasi katika mapori

Story za ujambazi wa jiwe Fatuma na utekaji mabasi katika mapori

Miaka ya kuelekea 2004-2005 kutokea Nyakakanzi, Kakonko hadi Kibondo palikua na askari wanajificha porini ili kudhibiti ujambazi na wakati huo wengine walikua wanapiga doria na chuma moja walikua wanaiita kimbuka 110 Defender ilikua na RPG kwajuu qudadadeqi hiyo njia nilikua napenda kuona wanyankazi wakipambania kivile... Sema nini pale mto Malagalasi wajomba waligingeshwa vyuma kinyama aiseeee
Huko majambazi konki kweri kweri na wana silaha nzito
Na magruneti...hawafai kabisa

Ova
 
well done serikali sikivu ya CCM,
kuweka vituo vya polisi maeneo hatarishi kwa usalama wa magari na wapita njia kwa ujumla.

I hope gentleman ,
ni mwenyeji wa pande hizo kwenye vindege vya kuaanga 🤣
Hahahaha ni hatari Gentleman, ndg zetu hawa Warangi wanapenda Vindege balaa, unakuta PC kali ya Kirangi inatafuna Videnge unajiuliza hii PC namna gani tena, mrangi

Kuanzia maeneo ya Chemba hadi Bicha, hadi Kondoa mjini
 
Bila kusahau pori la ushirombo
Nakumbuka Mwaka 2015 kama Mwezi wa pili hivi kabla ya Jiwe hajawa Rais.

Ulitokeaga Ujambazi saa tatu asubuhi katika Mnada wa Ng'ombe wa Busozo.

Warundi hawana Masiala hata kidogo, Mnada siku hiyo ulikuwa umefurika sana, punde si punde mnada mzima uliwekwa chini ya ulinzi mkali na Majambazi.

Risasi zilikuwa zinapita Kimo cha kawaida cha kati watu woteeee chini.

Wale Majambazi walitumia kama dakika 20 nahisi siku hiyo watu wengi sana walipolwa Fedha zao.

Mnada wa Busozo, Lusahunga, Benaco Matajiri wengi huja na fedha nyingi sana za kununua ng'ombe.

Baada ya wale majambazi kukamilisha lile zoezi walitokomea kusikojulikana, nahisi waliingia pori la Kigosi.

Polisi wanafika nusu saa baada ya tukio kutokea.

Ila Jiwe amekomesha sana Ujambazi, Ujambazi ulishamiri kipindi cha JK.

Kahama yametokea matukio mengi sana ya Ujambazi na utekaji.

Haswa utekaji ulikuwa unafanyika pale Busoka njia ya kwenda Kakola. Oya ilikuwa ni hatari ilikuwa haipiti mwezi bila kusikia milio ya bunduki.
 
Nakumbuka mwaka 2014 kama mwezi Desemba ivi au Novemba lilitokeaga tukio la Ujambazi pale kahama mchana kweupe.

Majambazi waliendaga kuvamia kwa Tajiri wa Kahama (kwa ndegesera), baada ya ujambazi ule zile kurupashani za polisi na wale majambazi mtaa wa Manzese kuna mwana mmoja alipigwa risasi, pale pale umauti ulimfika.

Ila ujambazi kahama ulikuwa balaa sana
 
Tukio jingine lilitokea Kahama kwenye mwaka 2010 ivi njia ya kweda Kakola - Geita.

Wale wanyarwanda siku ile waliotewa bwana wote waliuawa.

Ilikuwa hivi, wale majambazi walichojichanganya walifika site mapema kabla hapajawa giza, kuna sehemu walipaki gari yao kwenye kapori ka pale miembeni busoka kumbe bwana kuna mwana nchi ameusoma mchezo akawa ametoa taarifa kwa uongozi wa mtaa, na uongozi wa mtaa ukatoa taarifa polisi.

Kilichofanyika polisi walizuiya gari zinazotoka kakola zisivuke nyambura na gari zinazotoka kahama mjini zisivuke pale Manzese.

Polisi walichukua Fuso kama lakuzugia wakajifanya raia, walipofika sehemu ya tukio kama kawaida Wanyarwanda hawaapa, siku ile waliingia cha kike wote waliuawa.
 
Ni hatari sana mkuu
 
Miaka ya kuelekea 2004-2005 kutokea Nyakakanzi, Kakonko hadi Kibondo palikua na askari wanajificha porini ili kudhibiti ujambazi na wakati huo wengine walikua wanapiga doria na chuma moja walikua wanaiita kimbuka 110 Defender ilikua na RPG kwajuu qudadadeqi hiyo njia nilikua napenda kuona wanyankazi wakipambania kivile... Sema nini pale mto Malagalasi wajomba waligingeshwa vyuma kinyama aiseeee
Hatari ilikuwa ,hapo sijajua kama bado inaendelea ,ilikuwa lazima basi likikatiza hapo lazima ndani kuwe na askari escort wakiwa na magitaa.
 
kisa cha Jambazi mrundi aliyeitwa Swaga Ng'ombe, na Komando Dogo ilikuwa hatari sana sema Nini , Operation Kimbunga ilisaidia sana kikwete Hadi akataka kutuingiza vitani Na Rwanda.
 
Back
Top Bottom