Story za ujambazi wa jiwe Fatuma na utekaji mabasi katika mapori

Tofautisha mwizi na jambazi !
Hao walioiba radio, pasi sijui na nn ni wezi ! Sio majambazi !

Ahsante..... PSG Bingwa UEFA
Kipindi hiko nao walikuwa majambazi, acha kutofautisha wa zama hizo na sasa. Kipindi hiko hizo ndizo zilikuwa zana za kuogopwa na wakikukuta hawakuachi hivi hivi either ufe au ubaki na majeraha. Wa zama hizo ukiibiwa 100k ni sawa na sasa aliyeibiwa 10m.
 
Kuna hili pori la kutoka Geita kwenda KATORO ni kubwa mno
Sijui matukio ya miaka hiyo ya black and white
 
Majambazi mengi yalikuwa kwenye pori la Biharamulo Ile Lusahunga ilikuwa hatari
Wahuni wanapiga tukio kama serikali haupo
Polisi walikimbizwa
Walikuwa wakisikisikia tu mlio wa bunduki wanahepa
 
Hawa Gen Z hawajui habari za majambazi
Zamani ilikuwa risky sana
Mtu anauza mazao, mifugo, au mshahara unapokea mkononi halafu Ile night wanaingia wahuni kuchukua chao
 

Fuatilia story youtube kwa Power Mangwana aka Salmin Masikita Yeba sai Sai Sukisa na RFA Jonathan Meshaki Jambazi mtoto aliyetikisa Kanda ya ziwa miaka ya 2010-2013.

Kanda Mbili tunaita DABO DEKI.
 
Huko nishakutana na mziki aise

Ova
 
Gentleman, unafahamu au unajua chimbuko la umaarufu wa wimbo wa mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe?
basi, ambatana nami kwa uchache nikujuze,


Kuna mahali kuna pori inaitwa Mtungutu hiyo, upande wa kulia kuna mlima umefunga msitu mnene wa maana sana na mawe machache makubwa yanaonekana kichele, kushoto mlima mwingine uko mbali kidogo , ila kuufikia katikati ni msitu msitu kweli wakati huo, huenda mabadiliko ya tabia ya nchi imebadili kitu kwa sasa,

basi bana,
manjambazi kwenye mbinu zao za kutafuta riziki, si wakasambaza magogo ya maana sana katikati ya barabara,
kila basi la abiria au gari lolote lile likija, linapigwa mkono na kuegeshwa kadiri ya maelekezo ya jambazi, utadhani traffic wa ukaguzi wa usalama barabarani vile,

Abiria wote tukashushwa chini moja moja, wakati huo, jamaa wameweka ndoo kadhaa hapo nje ya mlango wa basi, kila moja ajisachi mwenye na kutupia kwenye ndoo kila kitu kinachoitwa pesa au dhahabu kama kutoa sadaka kwenye nyumba za ibada, iwe ni pete au hereni unaambiwa weka kwenye ndoo,

wakati huo, njungu za maana zinafyatuliwa hewani kwa fujo, zinafurushwa bila utaratibu hewani hadi maskio yanaziba kabisa,
na kuraruliwa hewani utadhani mizinga21 ya uapisho wa mkuu wa nchi fulani, acha kabisa gentleman,

namalizia kula cha usiku,
narejea kumalizia tukio,

lema ametoka mbali acheni tu ndugu zangu 🤣
 
Mtungutu!!napapata sana huko nyumbani kabisa!!

Nilizisikia nikiwa shule msingi huko kondoa vijijini kwamba mtungutu hapapitiki kizembe zembe!!
 
Katika mihangaiko yangu zamani,nlikuwa nacheza sana dodoma
Kuna wakati nlikuwa naenda sana kondoa(mambo ya struggle tena)
Kuna pori moja lilikuwa linaitwa msitu mtungutu (mm nlibabatiza jina mtukutu)
Kuna siku tunapita pale narudi dom natokea aneti
Enzi hizo road ile vumbi tu
Tuko kwenye bus ,mara tukashangaa bus limepigwa mkono jamaa walkuwa kwenye landrover kipande cha kizamani,abiria wote tulishushwa....abiria ndani wacha waanze kupanick wengine wanalia,unaambiwa toa ulicho nacho kama huna ulikuwa unapewa kipondo
Wale majambazi walikuwa wanajuwa fika Kuna warangi wanaotokea kondoa ni watamu pesa ipo,maana kuna wengine wanalima ufuta na wametoka uza pesa ipo
Kikubwa mimi ile njiaa nlishapewa ramani yake na mambo ya utekaji,nlipopanda bus nlipigilia pesa mahali kwenye siti (docho)
Alafu mfukoni nlibakiza kihela kdg,jamaa waliponisogelea mm sasa wakaniambia toa hela nkasema hapa nna 70,000 tu maana mm nmetoka kondoa kusalimia ndugu(zuga)kiukweli mambo ya ambush nishakutana nayo sana so uzoefu nnao na najuwa namna ya kudeal na situation kama hizo,jamaa wakwalaaa na siku zote waporaji wanapofanya mission hizo wanakuwaga na haraka hawana muda wa kupoteza
Basi jamaa wakwala wakaxhkua chao
Kuna dada mmoja na ustaz fulani zam walipoambiwa toa hela waliyokuwa nacho wakagoma aise walikula kipondo sana 😄
Badaye sana Kuna malalamiko yakapelekwa kwa maafisa wa polisi dodoma kuhusu ile njiaa na utekaji,ndy wakaja kuweka barrier pale izava
Mimi t3na nkaja nkabadilisha root ya kwenda kondoa nkawa naingilia narco --- matui---kiteto mpaka soya---kondoa

Ile ya nyakanaz nliyokutana nayo ndy ilikuwa balaa ile nlikuja kupigwa risasi ya paja 😄

Kuna nyingine nlikutana nayo kidodi njia ya kwenda kilombero tuliwekew Gogo sema tulishtka 😄 tuka save
Naona napo badaye pale polisi walikuwa wanakaa

Bado kuna visa za msumbiji
Tuscarora huko ...kongo tushaporwa....Sudan kusini tushaporwa

Hii duniaaa ni uwanja wa fujo tu

Ova
 
Mtungutu!!napapata sana huko nyumbani kabisa!!

Nilizisikia nikiwa shule msingi huko kondoa vijijini kwamba mtungutu hapapitiki kizembe zembe!!
Sasa mm nlikua natokea soya---naitafuta mwakisabe--- nakuja sajilwaa----segara au itiso pale
Nkiona machale yananicheza nakula docho naelekea dabalo nkifika hapo ndy naitafuta dodoma mjini
Yote na kwepa kuporwaa

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…