Baada ya Mahakama kutamka kuwa Hakimi hamiliki pesa wala mali yoyote, Hakimi akaanza ku trend mitandaoni. Watu wakampatia sifa zenye rangi, harufu na maumbo yote.
Ikumbukwe kwamba, swala hili halijaisha wakati ndiyo kwanza game ipo mapumziko.
Inathibitishika kuwa Hakimi ni muajiriwa, hivyo basi chini ya jina lolote ambapo hela na mali zake zinaenda kuhifadhiwa inakua ni salama kwa maswala mengine ya kisheria lakini si kwa mke wake.
Kesi itakayofuata, Hakimi anaweza akahitajika kutoa maelezo ni wapi ambapo pesa na mali alizozipata kutokana na kazi yake amekua akizipeleka, maana pesa ile ni mali halali ya familia yake, inakuwaje familia ijikute haina umiliki wa kitu chochote kile?
Vyovyote itakavyokuwa, kesi itakayofuata itamuweka Hakimi mahala pabaya zaidi. Mama yake atahitajika kuelezea chanzo cha mapato cha pesabna mali zilizo chini ya jina lake.
Hii kesi ya kwanza imeishia hapo na mdiyo ina trend kwa sasa, ila kesi ya pili nabashiri itakua mbaya zaidi na huenda Hakimi akajikuta mahala pagumu kuliko Emmanuel Ebue.