Champ
Senior Member
- Aug 14, 2018
- 109
- 190
Hawa sio mashabiki wa mpira au wafuasi wa chama fulani cha siasa. Hawa ni wataalamu wa kada ya afya. Madaktari, manesi, mafamasia etc. Wapo kwenye usaili kambi ya Twalipo, Mgulani, wakitaka kujiunga na jeshi,baada ya jeshi kutangaza nafasi za ajira. Hizi ni fani ambazo ilikua nadra sana kumkuta mtu anatafuta ajira. Wengi wao walikua wanapata ajira za moja kwa moja. Zamani kidogo haikua rahisi kukutana na daktari (MD) juani na bahasha ya kaki. Lakini leo tumefika hapa.
Halafu jiulize kama hawa ni wahitimu wa kada ya afya tu, vipi kada zingine kama ualimu, sayansi ya jamii, uhandisi, sheria, usimamizi wa biashara, etc. Hao ndio wengi zaidi na kila siku wanazidi kuhotimu.
Tatizo la ajira linazidi kukua siku hadi siku. Na bahati mbaya serikali badala ya kulipunguza, inafanya jitihada za kuliongeza. Kila siku tunasikia makampuni na mashirika binafsi yakifungwa na watu kupoteza ajira kwa sababu ya urasimu wa serikali.
Viongozi wetu nao wanatoa majibu mepesi eti 'watu waache kuwaza kuajiriwa badala yake wajiajiri' lakini anayesema hivyo yeye ni mtumishi serikalini, yani ameajiriwa. Unajiuliza kama kujiajiri ni rahisi hivyo kwanini yeye asiache kazi aingie mtaani? Watu wanahubiri vitu wasivyoviamini.
Mtu anajiajiri kwa mtaji gani? Hata akitaka mkopo hawezi kupata kwa sababu ya masharti magumu ya kibenki. Pia mazingira sio wezeshi kwa vijana kujiajiri. Akipata mtaji kidogo akanunua mchele kutoka Mbeya aje kuuza Dar, anakutana na sheria ya 'jiwe' kwamba hawezi kuuza bila kuonesha shamba. Akiamua kufanya online marketing anakutana na TRA wanamtaka alipe kodi. Anawezaje kusurvive?
Kuna watu wamekaa na 'degree' zao miaka mitano au zaidi, hadi walishasahau kama waliwahi kusoma. Wamehangaika juani kutafuta ajira bila mafanikio. Wengine wameamua 'kurudisha mpira kwa kipa'. Unakuta mtu ana miaka 30 ni msomi mzuri tu lakini anaishi kwa wazazi wake. Sio kwamba amependa ila mazingira yamemlazimu kufanya hivyo.
Kama ambavyo Rais Mkapa alihitaji mjadala wa kitaifa kuhusu elimu, nami nadhani tunahitaji pia mjadala wa kitaifa kuhusu ajira. Tatizo ni kubwa kuliko inavyofikiriwa. Lowassa aliwa kusema Tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka. Tujiandae.!