Suala la ajira linazidi kuwa janga Tanzania

Suala la ajira linazidi kuwa janga Tanzania

'Time bomb'! Lazima njia mbadala za kukabiliana na hili tatizo zibuniwe bila kusahau kutengeneza mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji (uwekezaji wa ndani na nje iwe mkubwa au mdogo), Ushirikishwaji wa sekta binafsi (kupunguza utitiri wa kodi), Vitaumbele vitolewe kwenye sekta zilizo ajiri raia wengi kama kilimo na mifugo ili wengi wavutiwe kujikita huko.
 
Kweli hali ni mbaya napata wasiwasi, inabidi kujiandaa kisaikolojia muda wangu utakapofika.
 
Niliwaambia marafiki zangu 2016 kuwa Magu lazima awasomeshe namba vijana kwenye, wakaleta ule utoto wa chuo oooohhh ananyoosha nchi, anaweka mambo sawa, sasa hivi kila mmoja kakimbilia kusikojulikana hali tete mwaka wa 3 no ajira na mtaji wengi hawana.
 
ajira zimeongezeka jeshini, make koro show lazima zibanguliwe
 
Hata hivyo jamani tujue kuwa serikali haiwezi kuajiri wahitimu wote wa vyuo, wanaohitimu ni wengi mno ukilinganisha na uhitaji wenyewe.

Serikali inatakiwa kuboresha sekta zisizo rasmi na kutoa mikopo kwa vijana au vikundi ili wajiajiri,

Inabidi tubadilike kifikra, tusisome kwa lengo la kuajiriwa, tusome kupata maarifa, tunakoelekea ndiyo kubaya zaidi.
 
Wewe ni ZWAZWA Kuu.
 
Tatizo linakuja hata wanaokushauri ujiajiri wao ni watumishi wa serikali

Maana kinachokwamisha watu kujiajiri ni

1. Mtaji wa kutosha
2.wateja

Fikiria mtu amemaliza MD huyu anajiajiri vipi au ndo kurudi kuuza duka
 
Tanzania hata kama ukiwa na mtaji plus a "million-dollar idea" utakwama tu.

Diamond, Ruge, Mengi ni kati ya wafanyabiashara wanaoongoza kujipendekeza kwa watawala ili mambo yao "kampuni" ziende lakini huwa wanakwama mara nyingi tu seuse wewe KAPUKU graduate mwenye kimtaji cha mkopo, usiye na jina, humjui mtu na ki- START UP chako ??

Kwanza ukianza tu, kodi utakayokadiriwa TRA lazima kichwa kikuume.

Ukiwa na roho ngumu, ukaendesha ki-start up chako hata mwaka tu utashangaa unaanza kupigwa faini zisizo na majibu,
- Leo wanakuja TRA, kesho FIRE, kesho kutwa TBS, TFDA, Meat Council, OSHA, BRELA, NEMC n.k

- Hapo hata faida hujapata, bado kodi za HALMASHAURI na michango iliyoambatana na vitisho ya MWENGE na CCM.
 
Mm nashangaa mtu unasema watu wajiajiri wakat swala la ajira liko dunia nzima, serikali na makampuni kwenye nchi zilizoendelea wanaajiri na kule kuna matumizi makubwa ya roboti ila wanaajiri Serikali inatakiwa itafute mbinu za kupunguza ili tatizo lakini kwa inavyoonekana serikali yetu ndyo ya kwanza kuongeza ili tatizo maana imeongeza kodi kwenye kila kitu ambapo makampuni mengi yamebidi kupunguza wafanyakazi, wakulima wamekatazwa kuuza mazao nje japokuwa walivuma mazao mengi kuliko uwezo wa nchi na wakashindwa ata kuyanunua.
Kwa mtazamo wangu sioni hali ikiboreka hata miaka miwili ijayo naisi ndyo itakuwa mbaya kuliko
 
Haya ndio matunda ya mazingira tuliyojiwekea kuwa UKISOMA NA KUMALIZA MASOMO VIZURI UTAAJIRIWA.

Tumejidumaza akili kwa kuwaza kuajiriwa tu, yaani tumejengewe maisha ni kuajiriwa... haya ndio matokeo yake!
Ukisema ujiajiri tra wanaua hiyo biashara soko hamna sababu pesa imekuwa ngumu hivyo wengi wanachagua ajira. Mkuu wewe umejiajiri?
 
Kwa hiyo unawashauri walio soma kada ya afya wajiajiri kwa kuanzisha hospital zao??

Acha ujinga
Mjinga wewe! Soma nilichoandika na kuelewa. Unaweza soma kada ya Afya na bado ukajiajiri/ukafanya shughuli nyingine tofauti na afya. Tatizo umekariri kuwa ukisoma afya lazima ufanye afya. Jiongeze!
 
Back
Top Bottom