Suala la ajira linazidi kuwa janga Tanzania

Ajira kweli ni tatizo tena tatizo kubwa mno, kwa hali ilivyo haijalishi kama mhandisi, daktari, nesi, mwalimu , fundi mchundo n.k ,
Ajabu ni kwamba kadri miaka inavyoenda mbele ajira zinazidi kua adimu,mfano tuu mdogo mwaka jana nilibahatika kufanya interview 6 , mwaka huu sijafanya interview yoyote mpk December hii,
Mkuu ile kauli mbiu kuwa elimu ni ufunguo wa maisha ina mana ilikosewa?
 
Mjinga wewe! Soma nilichoandika na kuelewa. Unaweza soma kada ya Afya na bado ukajiajiri/ukafanya shughuli nyingine tofauti na afya. Tatizo umekariri kuwa ukisoma afya lazima ufanye afya. Jiongeze!
We kweli box yaani mtu akomae miaka
Miaka 7 primary
Maika 6 secondary
Miaka 5 degree MD
Alafu unataka akajiajiri kuuza vitenge au supu ya pweza barabarani...??
Hujui mtu hadi kuwa daktari serikali imemgharamikia kiasi gani?
Na bado kuna hospital na zahanati hazina wahudumu wa afya
Alafu umevimbiwa na makande unakuja kuleta upupu wako huku.

Mijitu mkishashiba hamkumbuki na kuwahurumia wengine.

Jinga kabisa wewe.
Na kweli umedhihirisha ujinga wako.
 
Mjinga wewe unayedhani kusoma ndio kuajiriwa.
Mjinga kabisa usiyejua kuwa serikali kukusomesha sio lazima ikuajiri. Elimu uliyoipata ungeweza kuitumia bila kuajiriwa
Mjinga wewe zaidi ya wajinga unayedhani kujiajiri ni kuuza vitenge na supu ya pweza
Mjinga usiyejijua zumbu kuku ulimwengu uko huku kwa kuwa hujui ni kwanini zahanati hazina wahudumu wa afya na serikali imeshindwa kuwaajiri.
 
Kalamu1 tuwaache vijana wasote kitaa tu au tuweke utaratibu wa mtanzania kwanza kwenye ajira ya mashirika ya kigeni nchini?
 
Hawa sio mashabiki wa mpira au wafuasi wa chama fulani cha siasa. Hawa ni wataalamu wa kada ya afya. Madaktari, manesi, mafamasia etc. Wapo kwenye usaili kambi ya Twalipo, Mgulani, wakitaka kujiunga na jeshi,baada ya jeshi kutangaza nafasi za ajira. Hizi ni fani ambazo ilikua nadra sana kumkuta mtu anatafuta ajira. Wengi wao walikua wanapata ajira za moja kwa moja. Zamani kidogo haikua rahisi kukutana na daktari (MD) juani na bahasha ya kaki. Lakini leo tumefika hapa.

Halafu jiulize kama hawa ni wahitimu wa kada ya afya tu, vipi kada zingine kama ualimu, sayansi ya jamii, uhandisi, sheria, usimamizi wa biashara, etc. Hao ndio wengi zaidi na kila siku wanazidi kuhotimu.

Tatizo la ajira linazidi kukua siku hadi siku. Na bahati mbaya serikali badala ya kulipunguza, inafanya jitihada za kuliongeza. Kila siku tunasikia makampuni na mashirika binafsi yakifungwa na watu kupoteza ajira kwa sababu ya urasimu wa serikali.

Viongozi wetu nao wanatoa majibu mepesi eti 'watu waache kuwaza kuajiriwa badala yake wajiajiri' lakini anayesema hivyo yeye ni mtumishi serikalini, yani ameajiriwa. Unajiuliza kama kujiajiri ni rahisi hivyo kwanini yeye asiache kazi aingie mtaani? Watu wanahubiri vitu wasivyoviamini.

Mtu anajiajiri kwa mtaji gani? Hata akitaka mkopo hawezi kupata kwa sababu ya masharti magumu ya kibenki. Pia mazingira sio wezeshi kwa vijana kujiajiri. Akipata mtaji kidogo akanunua mchele kutoka Mbeya aje kuuza Dar, anakutana na sheria ya 'jiwe' kwamba hawezi kuuza bila kuonesha shamba. Akiamua kufanya online marketing anakutana na TRA wanamtaka alipe kodi. Anawezaje kusurvive?

Kuna watu wamekaa na 'degree' zao miaka mitano au zaidi, hadi walishasahau kama waliwahi kusoma. Wamehangaika juani kutafuta ajira bila mafanikio. Wengine wameamua 'kurudisha mpira kwa kipa'. Unakuta mtu ana miaka 30 ni msomi mzuri tu lakini anaishi kwa wazazi wake. Sio kwamba amependa ila mazingira yamemlazimu kufanya hivyo.

Kama ambavyo Rais Mkapa alihitaji mjadala wa kitaifa kuhusu elimu, nami nadhani tunahitaji pia mjadala wa kitaifa kuhusu ajira. Tatizo ni kubwa kuliko inavyofikiriwa. Lowassa aliwa kusema Tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka. Tujiandae.!View attachment 971960
Si mchezo kwa nyomi hilo hali ni tete mtaani.
 
Yaan Hali ni mbaya sanaaa hasa ukiangalia huko tuendako ........Tunaambiwa tutaajiriwa na viwanda!?! Kwa mazingira yap!? Lini!? Na kwa Viwanda vipi vya ku_absorb number ya wasomi wengi mtaani BILA KUSHINIKIZA MJADALA WA KITAIFA BUNGENI (kama Hoja ya dharura/mswada/ajenda).....UNAHITAJIKA

Hii Elimu yetu Imekuwa biashara na sehem ya kwenda kupoteza muda na fedha.... Mwishowe unataman ungeanza ujasiriamali kitambo ss pengine ungekuwa level nyingine kimaisha (maisha bora)......
 
Hakika mkuu kama maisha ni haya haya bora usome wastani tu uingie kwenye utafutaji mapema. Maana msomi hana deal wakati muuza chips anahesabu 100000 kwa siku! Kama yupo maeneo ya kona za town.
 
Swala la ajira kwa mpande mmoja nailaumu serikali na upande mwingine nalaumu sisi wenyewe.

Serikali inatakiwa kuwezesha upatikanaji wa ajira na pia kuwa na elimu inayo muwezesha mtu kujiajiri.

Kwa upande mwingine, sisi tunazingua tena sana. Mtu kaajiriwa 20 years hajajiongeza hata kidogo. Yaani kaajiri housegirl tu.

Sisi tunaamini mwekezaji ni mzungu na awe na hela ndefu, wakati sisi wenyewe tunatakiwa kuwa wawekezaji.

Umeajiriwa 20 years, angali basi ka fursa kakufungua walau ka consultant firm na wewe uwe umetengeneza ajira.

Maana bila hivyo ajira zinatoka wapi? Miaka hiyo 20 uliyokalia siti kuna watu kibao wanamaliza chuo.

Haiwezekeni serikali kuweza kuwaajiri watu wote. Secta binafsi zinahitajika. Yes najua kuna changamoto kwenye secta binafsi na changamoto zingine huchangiwa na serikali lakini bado, tujiongeze, sana yaani.
 
Hawa sio mashabiki wa mpira au wafuasi wa chama fulani cha siasa. Hawa ni wataalamu wa kada ya afya. Madaktari, manesi, mafamasia etc. Wapo kwenye usaili kambi ya Twalipo, Mgulani, wakitaka kujiunga na jeshi,baada ya jeshi kutangaza nafasi za ajira. Hizi ni fani ambazo ilikua nadra sana kumkuta mtu anatafuta ajira. Wengi wao walikua wanapata ajira za moja kwa moja. Zamani kidogo haikua rahisi kukutana na daktari (MD) juani na bahasha ya kaki. Lakini leo tumefika hapa.

Halafu jiulize kama hawa ni wahitimu wa kada ya afya tu, vipi kada zingine kama ualimu, sayansi ya jamii, uhandisi, sheria, usimamizi wa biashara, etc. Hao ndio wengi zaidi na kila siku wanazidi kuhotimu.

Tatizo la ajira linazidi kukua siku hadi siku. Na bahati mbaya serikali badala ya kulipunguza, inafanya jitihada za kuliongeza. Kila siku tunasikia makampuni na mashirika binafsi yakifungwa na watu kupoteza ajira kwa sababu ya urasimu wa serikali.

Viongozi wetu nao wanatoa majibu mepesi eti 'watu waache kuwaza kuajiriwa badala yake wajiajiri' lakini anayesema hivyo yeye ni mtumishi serikalini, yani ameajiriwa. Unajiuliza kama kujiajiri ni rahisi hivyo kwanini yeye asiache kazi aingie mtaani? Watu wanahubiri vitu wasivyoviamini.

Mtu anajiajiri kwa mtaji gani? Hata akitaka mkopo hawezi kupata kwa sababu ya masharti magumu ya kibenki. Pia mazingira sio wezeshi kwa vijana kujiajiri. Akipata mtaji kidogo akanunua mchele kutoka Mbeya aje kuuza Dar, anakutana na sheria ya 'jiwe' kwamba hawezi kuuza bila kuonesha shamba. Akiamua kufanya online marketing anakutana na TRA wanamtaka alipe kodi. Anawezaje kusurvive?

Kuna watu wamekaa na 'degree' zao miaka mitano au zaidi, hadi walishasahau kama waliwahi kusoma. Wamehangaika juani kutafuta ajira bila mafanikio. Wengine wameamua 'kurudisha mpira kwa kipa'. Unakuta mtu ana miaka 30 ni msomi mzuri tu lakini anaishi kwa wazazi wake. Sio kwamba amependa ila mazingira yamemlazimu kufanya hivyo.

Kama ambavyo Rais Mkapa alihitaji mjadala wa kitaifa kuhusu elimu, nami nadhani tunahitaji pia mjadala wa kitaifa kuhusu ajira. Tatizo ni kubwa kuliko inavyofikiriwa. Lowassa aliwa kusema Tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka. Tujiandae.!View attachment 971960
Sidhani kama Tanzania tuna baraza la Taifa la Vijana au organization yyte ya kitaifa ya vijana.... Na kama lipo bas wamelala na hawajitambui....... kuna haja ya kuwa muungano wa vijana wote na kupeleka mbele ya "Jiwe" kwa umoja wetu na ulisemea hilii (ajira na mazingira ya kujiajiri) kama state of emergency........ Mana vijana ndio nguvu kaz ya kulisukuma gurudumu la maendeleo ya taifa lolote dunian cha kushangaza hii nguvu kaz, taaluma na maarifa yanapotea hivi............

Gharama nyingi za kusoma had unamaliza unanza kuuza genge au shughuli nyingne za juakali ili uweze kuishi...... Hata nafsi inakuuma, mbaya zaid unakomaa kijiajiri kutafuta mtaji bado unabanwa na serikali...... Upate huo mtaji bado utajikuta unatapatapa tu kama mfa maji.......... Hala unakuta watu wameajiriwa wanakuhamasisha kujiajir.....

Vijana weng hata humu jf tuko bze na mijadala mingine hata isiyo na tija tunasahuu future ya hii nchi ni wajibu wetu........ Yaaan!......

Wacha niaachie hapo........ Mana bila vitendo yote ni siasa tu.....
 
Ni janga la duniani kote bana
Wenzetu huko wakiongelea ajira wanaongelea zile rasmi zinazoeleweka lakini zile za.kubeba maboksi zipo nyingi tu na watu hawafi njaa lakini bongo hata ukiomba kibarua ubebe kreti kiwandani hakuna maana viwanda vichache.
 
Haya ndio matokeo ya wazazi wetu kulilia Sera ya upepari

Huku wakijigeuza wanaharakati kushutumu Sera ya ujamaa na kujitegemea kwa kulikanyaga kwa dhihaka na kulitupilia mbali Azimio La Arusha

Tunahitaji elimu yetu waliyoikataa mababa zetu kwa kumuona nyerere ni mnafiki kwa sera zake

huko alipopaona mwasisi wa taifa hili ndipo penye nuru na mwanga, nyerere alifariki huku akililia AZIMIO LA ARUSHA

Tunahitaji elimu ya kutufanya tujitegemee sio kutegemea kuajiriwa.
 
Tulio wapa dhamana wamefeli
Wenzetu huko wakiongelea ajira wanaongelea zile rasmi zinazoeleweka lakini zile za.kubeba maboksi zipo nyingi tu na watu hawafi njaa lakini bongo hata ukiomba kibarua ubebe kreti kiwandani hakuna maana viwanda vichache.
 
Swala la ajira kwa mpande mmoja nailaumu serikali na upande mwingine nalaumu sisi wenyewe.

Serikali inatakiwa kuwezesha upatikanaji wa ajira na pia kuwa na elimu inayo muwezesha mtu kujiajiri.

Kwa upande mwingine, sisi tunazingua tena sana. Mtu kaajiriwa 20 years hajajiongeza hata kidogo. Yaani kaajiri housegirl tu.

Sisi tunaamini mwekezaji ni mzungu na awe na hela ndefu, wakati sisi wenyewe tunatakiwa kuwa wawekezaji.

Umeajiriwa 20 years, angali basi ka fursa kakufungua walau ka consultant firm na wewe uwe umetengeneza ajira.

Maana bila hivyo ajira zinatoka wapi? Miaka hiyo 20 uliyokalia siti kuna watu kibao wanamaliza chuo.

Haiwezekeni serikali kuweza kuwaajiri watu wote. Secta binafsi zinahitajika. Yes najua kuna changamoto kwenye secta binafsi na changamoto zingine huchangiwa na serikali lakini bado, tujiongeze, sana yaani.
Pia hatusemi serikal iajiri wote direct kwasabab haiwezekani bali indirect kwa kutengeneza mazingira na mifumo mizuri ya succession kwa hawalio ktk siti na wanahitaji siti.... Pia kuhamasisha walio na wazfa kuwekeza sector mbal mbal kwa kuwapa privilege ili wawaajiri wengine na wengine.... Kifupi itengenezwe Chain system ya ku-absorb wanaohitaji kuajiriwa.....
 
Succession kivipi? Waweke mfumo wa kuwaachisha kazi after miaka flani ama? Maana umri wa kustaafu upo.

Fursa wanapewa, mikopo ipo kwa wafanyakazi wote wa serikali. Wafanywe nini zaidi? Au ndo unataka mpaka ushikwe mkono uambiwe mchongo huu hapa, wekeza hapa. Maana hapo litakuja swala lingine la upendeleo.

Tatizo sisi tuna bweteka. Yaani ukipata kazi unaona maisha umeshayapatia. Ndo unalala kabisaa, hujigusi wala kujiongeza.
 
Mosi, Bila shaka ww ni mwairiwa pia muhanga wa vijana wengi walio toka vyuon recently especially kuanzia utawala wa Jiwe............

Pili, nimekuwa general kuruhusu mawazo mengine, pia ktk halo ikibi hata umri wa kustaafu upunguzwe wakat wana train wengine (vijana zaidi) kujaza hzo nafas.......

Tatu, kuhusu mkopo nadhan unajua changamoto zake kama hujui waulize wanaojua then ulete kwa hao vijana graduate wengi walio wanafunzi wa mtaa.........then utakuwa na jib

Note:

NI MTAZAMO TU SIO CONCLUSION WALA LEAGUE ..... NIA NI KUPATA SULUHU YA HILI SUALA (UNEMPLOYMENT)
 
..... #si muhanga.......
 
Kijana, hahaha,
Mosi, nime graduate 2008, nimeajiriwa for 8 years kwanzia nikiwa chuo nilianza kutafuta ajira na kufanikiwa kupata nikiwa mwaka wa 2.

Nimefungua kampuni yangu 2016 na nimeajiri vijana wengi na bado naendelea kupambana.

Kwahiyo siyo "recently" graduate as you put it.

Pili, wewe ungetaka umri wa kustaafu uwe umri gani? Maana kwa sasa kustaafu kwa hiari ni 55 years na Kwa lazima ni 60 years.

Jaribu kushusha hapo uone maandamano yake. Na sisi vijana tunavyo chelewa kuanza maisha na kujijenga. Sasa hivi wengi wana staafu hawana cha maana walicho kifanya.

Tatu, yes mikopo ina matatizo yake, lakina vilevile hakuna kitu kisichokuwa na matatizo, Mikopo ya serikalini bondi ni serikali (mshahara) na siyo mali zako.

Hizo changamoto ni za sisi tuliojiajiri.
 
Tatizo mfumo wetu wa elimu hautujengi kwa self reliance. Ni muda muafaka sasa mitaala yetu kuanzia shule ya msingi iwatayarishe watoto kwa kujitegemea na sio kuajiriwa.
 
Back
Top Bottom