Suala la ajira linazidi kuwa janga Tanzania

Suala la ajira linazidi kuwa janga Tanzania

Kalamu1 tuwaache vijana wasote kitaa tu au tuweke utaratibu wa mtanzania kwanza kwenye ajira ya mashirika ya kigeni nchini?
Naona wewe ni mgumu sana wa kuelewa. Hujui kitu kabisa. Wewe unayetaka kukwamisha wanaochangia kuleta ajira unawasaidiaje hawa vijana?
Nadhani unalo tatizo la uelewa wa mambo. Haya maswala yako juu ya uwezo wako wa kuyaelewa.
 
Tatizo la ajira linazidi kukua siku hadi siku. Na bahati mbaya serikali badala ya kulipunguza, inafanya jitihada za kuliongeza. Kila siku tunasikia makampuni na mashirika binafsi yakifungwa na watu kupoteza ajira kwa sababu ya urasimu wa serikali.

"Urasimu wa serikali", na ukiangalia kwa karibu, unaweza kukuta sio serikali hasa inayofanya urasimu huo, ni baadhi tu ya watumishi ndani ya serikali hiyo. Chilubi wa JF analielewa vizuri sana jambo hili. Aiambiwa hataki kuelewa.
 
Haya ndio matunda ya mazingira tuliyojiwekea kuwa UKISOMA NA KUMALIZA MASOMO VIZURI UTAAJIRIWA.

Tumejidumaza akili kwa kuwaza kuajiriwa tu, yaani tumejengewe maisha ni kuajiriwa... haya ndio matokeo yake!
Wacha ujinga aisee. Unataka mtu anayemaliza chuo na digrii ya nursing akajiajiri wapi? Daktari, Pharmast wakajiajiri wapi? Unajua unachokizungumza hapa, na naona umepata 'like' za kutosha toka kwa wajinga wenzako! Kuna baadhi ya taaluma huwezi kwenda mtaani ukaanzishe karakana yako ya kuosha vidonda au kudunga sindano.
 
Jana nimekutana na bar med ana degree ya sociology "" anaongea fluent English sikuamin nilimdadis Nika confirm anachokisema nikweli,,
 
Jana nimekutana na bar med ana degree ya sociology "" anaongea fluent English sikuamin nilimdadis Nika confirm anachokisema nikweli,,
Duuuh hatari sana ndo tulipo fika kama taifa.
 
Bado roli liko barabara ya vumbi muda si mrefu litaingia garage
 
Ha ha haaaa.....wengi wenu hapo mmesoma afya ili kupata ajira, ikipigwa interview ya maana hamfai kuhudumia watu....Mliwacheka wenzenu wa sanaa et wamekalili zinjatropas...pambaneni na hali zenu
Acha dharau wewe
 
Haya ndio matunda ya mazingira tuliyojiwekea kuwa UKISOMA NA KUMALIZA MASOMO VIZURI UTAAJIRIWA.

Tumejidumaza akili kwa kuwaza kuajiriwa tu, yaani tumejengewe maisha ni kuajiriwa... haya ndio matokeo yake!
Sasa ulitaka wafanye Nini?? Au utawapa mtaji?? then matapeli wakijaa mitaani mnalalama.
 
Kijana, hahaha,
Mosi, nime graduate 2008, nimeajiriwa for 8 years kwanzia nikiwa chuo nilianza kutafuta ajira na kufanikiwa kupata nikiwa mwaka wa 2.

Nimefungua kampuni yangu 2016 na nimeajiri vijana wengi na bado naendelea kupambana.

Kwahiyo siyo "recently" graduate as you put it.


Pili, wewe ungetaka umri wa kustaafu uwe umri gani? Maana kwa sasa kustaafu kwa hiari ni 55 years na Kwa lazima ni 60 years.

Jaribu kushusha hapo uone maandamano yake. Na sisi vijana tunavyo chelewa kuanza maisha na kujijenga. Sasa hivi wengi wana staafu hawana cha maana walicho kifanya.

Tatu, yes mikopo ina matatizo yake, lakina vilevile hakuna kitu kisichokuwa na matatizo, Mikopo ya serikalini bondi ni serikali (mshahara) na siyo mali zako.

Hizo changamoto ni za sisi tuliojiajiri.
Hukunielewa....... Nilimaanisha ur probably not a recently years of Maguful....come on men!
 
Hukunielewa....... Nilimaanisha ur probably not a recently years of Maguful....come on men!
Isome post yako tena...alafu useme sijakuelewa...

"Mosi, Bila shaka ww ni mwairiwa pia muhanga wa vijana wengi walio toka vyuon recently especially kuanzia utawala wa Jiwe............"
 
employment problem solved. - JamiiForums
Hawa sio mashabiki wa mpira au wafuasi wa chama fulani cha siasa. Hawa ni wataalamu wa kada ya afya. Madaktari, manesi, mafamasia etc. Wapo kwenye usaili kambi ya Twalipo, Mgulani, wakitaka kujiunga na jeshi,baada ya jeshi kutangaza nafasi za ajira. Hizi ni fani ambazo ilikua nadra sana kumkuta mtu anatafuta ajira. Wengi wao walikua wanapata ajira za moja kwa moja. Zamani kidogo haikua rahisi kukutana na daktari (MD) juani na bahasha ya kaki. Lakini leo tumefika hapa.

Halafu jiulize kama hawa ni wahitimu wa kada ya afya tu, vipi kada zingine kama ualimu, sayansi ya jamii, uhandisi, sheria, usimamizi wa biashara, etc. Hao ndio wengi zaidi na kila siku wanazidi kuhotimu.

Tatizo la ajira linazidi kukua siku hadi siku. Na bahati mbaya serikali badala ya kulipunguza, inafanya jitihada za kuliongeza. Kila siku tunasikia makampuni na mashirika binafsi yakifungwa na watu kupoteza ajira kwa sababu ya urasimu wa serikali.

Viongozi wetu nao wanatoa majibu mepesi eti 'watu waache kuwaza kuajiriwa badala yake wajiajiri' lakini anayesema hivyo yeye ni mtumishi serikalini, yani ameajiriwa. Unajiuliza kama kujiajiri ni rahisi hivyo kwanini yeye asiache kazi aingie mtaani? Watu wanahubiri vitu wasivyoviamini.

Mtu anajiajiri kwa mtaji gani? Hata akitaka mkopo hawezi kupata kwa sababu ya masharti magumu ya kibenki. Pia mazingira sio wezeshi kwa vijana kujiajiri. Akipata mtaji kidogo akanunua mchele kutoka Mbeya aje kuuza Dar, anakutana na sheria ya 'jiwe' kwamba hawezi kuuza bila kuonesha shamba. Akiamua kufanya online marketing anakutana na TRA wanamtaka alipe kodi. Anawezaje kusurvive?

Kuna watu wamekaa na 'degree' zao miaka mitano au zaidi, hadi walishasahau kama waliwahi kusoma. Wamehangaika juani kutafuta ajira bila mafanikio. Wengine wameamua 'kurudisha mpira kwa kipa'. Unakuta mtu ana miaka 30 ni msomi mzuri tu lakini anaishi kwa wazazi wake. Sio kwamba amependa ila mazingira yamemlazimu kufanya hivyo.

Kama ambavyo Rais Mkapa alihitaji mjadala wa kitaifa kuhusu elimu, nami nadhani tunahitaji pia mjadala wa kitaifa kuhusu ajira. Tatizo ni kubwa kuliko inavyofikiriwa. Lowassa aliwa kusema Tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka. Tujiandae.!View attachment 971960
 
Kama unataka kujiunga na free mason soma hapa ili uwe tajiri kama dimond

There are authorities, hierarchies and positions in the Freemason brotherhood and every of this personnels have their individual roles to play when it concerns a new membership in different nations. The Freemason brotherhood finance master for Africa is in charge of the payment of this installation materials for African new members I am suggested to as the finance master of the Freemason brotherhood in Africa so you have to do this payment to my individual details and I receive the payment then pass it onto the Headquarters for confirmation of this items payment before they proceed with the payment of your membership welcome redemption money of 3 hundred thousand dollars($300,000.00) which will enable you to pay your flight and go for installation of your membership before going back to your country to enjoy this benefits and live a brand new life.
that money will be paid to you direct through western union ,but you have to pay first activation fees of us 169 then within three days after payment you will receive your money.
 
Nilikosea kuandika....... I meant bila shaka ww ni mwajiriwa na si muhanga kama vijana wengi..............

Chin nili correct kwa # si muhanga..... Sory misleadings....

Pia congrats for ur achievement but at this thread ww ni kama aliyeshiba (employed) kat ya wengi wenye njaa (unemployed youth)......... Hyo 2008 yako ya tangu kikwete had kuanzia 2016 u can't compare #neither the same nor similar. Kipnd hcho (2008) mm ndio namaliza form 4 so......

Note:
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa........ By Wahenga.
Isome post yako tena...alafu useme sijakuelewa...

"Mosi, Bila shaka ww ni mwairiwa pia muhanga wa vijana wengi walio toka vyuon recently especially kuanzia utawala wa Jiwe............"
 
Tena watakupeleka kwenye maombi faster😀 Ukweli ni kwamba mfumo huu unatuumiza sasa, inabidi tubadilike kabisa. Tuanze kuwajengea watoto wetu kuwa kusoma ni kuondoa ujinga na kufunguka kiakili zaidi SIO kuajiriwa na kuwa mtumwa kama hivi
Wakuu Tuachane na Habari za Mfumo! Ili hili litimie Sehemu kubwa ni mzazi ndiye anaye-play part kubwa; Mimi mtoto wangu anasoma Shule, na Yuko Vizuri class kwa kweli anajitahidi, Binafsi Nimeajiriwa Lakin pia nina Business zangu za Upigaji Picha na Video; Dogo akiwa Std Four/Five, nilikuwa namchukua Tunaenda nae Ofisin(Private office) anashinda huko, Kuanzia Std six had seven, nikienda Location naenda Nae, Nampa Camera Moja nilioanza nayo kazi namwambia apige Picha zake, then kesho tukienda Ofisin, Namwambia acopy kwenye computer nazikagua na Kumsifia na Kumwambia alichokosea kwenye uchukuaji matukio; Currentyl yuko Form 3, Sina hofu kumwachia apige Ubarikio/Wedding/Sendoff akisimamiwa na Vijana wangu wa kazi, Anafunga screen Ukumbini, anafanya connection zote; Desemba hii amerudi kutoka shule, anapiga kazi nzuri sana ambazo kweli nazifurahia kama mzazi, Drone Anarusha na Picha anapiga Vizuri tu; Wiki mbili zilizopita alipiga kazi ya Wedding kwa Drone, yaan hata baadhi ya Vijana wangu ambao nimekuwa nao kwenye Kazi wanakubali kazi zake, japo sio kwa kiwango lakini sio mbaya; Yuko so Interested na Hii Industry, Ananishauri sasa, kwamba Kuna Camera hii na Hii, Ukimkuta Youtube yeye ni mambo ya Camera tu na editing; Kwa sasa naona anaanza kumuambukiza na Mdogo wake wa Kike, Wanapigana picha wanakuja kunionesha etc.

Sasa ukiniuliza dogo shule anasoma, lakini hayo mambo yote hajayapata shule; Sasa kama mzazi ingekuwa Ngumu kumwambia mtoto awe na mawazo ya kujiajiri wakati wewe binafsi hata Bussiness Huna; Hivyo succesional Planing inakuwa ni kuajiriwa tuu.
Wazazi tubadilike sisi kwanza, inakuwa rahisi kuambukiza watoto
 
Umeambiwa wote hao hawana kazi? Pia kuwa makini na hiyo picha imepigwa kimakosa haikupaswa kupigwa.
 
Hawa sio mashabiki wa mpira au wafuasi wa chama fulani cha siasa. Hawa ni wataalamu wa kada ya afya. Madaktari, manesi, mafamasia etc. Wapo kwenye usaili kambi ya Twalipo, Mgulani, wakitaka kujiunga na jeshi,baada ya jeshi kutangaza nafasi za ajira. Hizi ni fani ambazo ilikua nadra sana kumkuta mtu anatafuta ajira. Wengi wao walikua wanapata ajira za moja kwa moja. Zamani kidogo haikua rahisi kukutana na daktari (MD) juani na bahasha ya kaki. Lakini leo tumefika hapa.

Halafu jiulize kama hawa ni wahitimu wa kada ya afya tu, vipi kada zingine kama ualimu, sayansi ya jamii, uhandisi, sheria, usimamizi wa biashara, etc. Hao ndio wengi zaidi na kila siku wanazidi kuhotimu.

Tatizo la ajira linazidi kukua siku hadi siku. Na bahati mbaya serikali badala ya kulipunguza, inafanya jitihada za kuliongeza. Kila siku tunasikia makampuni na mashirika binafsi yakifungwa na watu kupoteza ajira kwa sababu ya urasimu wa serikali.

Viongozi wetu nao wanatoa majibu mepesi eti 'watu waache kuwaza kuajiriwa badala yake wajiajiri' lakini anayesema hivyo yeye ni mtumishi serikalini, yani ameajiriwa. Unajiuliza kama kujiajiri ni rahisi hivyo kwanini yeye asiache kazi aingie mtaani? Watu wanahubiri vitu wasivyoviamini.

Mtu anajiajiri kwa mtaji gani? Hata akitaka mkopo hawezi kupata kwa sababu ya masharti magumu ya kibenki. Pia mazingira sio wezeshi kwa vijana kujiajiri. Akipata mtaji kidogo akanunua mchele kutoka Mbeya aje kuuza Dar, anakutana na sheria ya 'jiwe' kwamba hawezi kuuza bila kuonesha shamba. Akiamua kufanya online marketing anakutana na TRA wanamtaka alipe kodi. Anawezaje kusurvive?

Kuna watu wamekaa na 'degree' zao miaka mitano au zaidi, hadi walishasahau kama waliwahi kusoma. Wamehangaika juani kutafuta ajira bila mafanikio. Wengine wameamua 'kurudisha mpira kwa kipa'. Unakuta mtu ana miaka 30 ni msomi mzuri tu lakini anaishi kwa wazazi wake. Sio kwamba amependa ila mazingira yamemlazimu kufanya hivyo.

Kama ambavyo Rais Mkapa alihitaji mjadala wa kitaifa kuhusu elimu, nami nadhani tunahitaji pia mjadala wa kitaifa kuhusu ajira. Tatizo ni kubwa kuliko inavyofikiriwa. Lowassa aliwa kusema Tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka. Tujiandae.!View attachment 971960
if you dont kwow where your going you will end to be in the area you have never planned to be........WORK LIFE BALANCE IS BOGUS LIFE ingawaje hajira hakuna na kwamuendelezo huu naamini 100 suala la ajira litaendelea kuwa tatizou kubwa zaidi miaka ya usoni naona tujitahidi pia kupambana wenyewe tusijidharau we have to do whatever it takes. .
 
Naona wewe ni mgumu sana wa kuelewa. Hujui kitu kabisa. Wewe unayetaka kukwamisha wanaochangia kuleta ajira unawasaidiaje hawa vijana?
Nadhani unalo tatizo la uelewa wa mambo. Haya maswala yako juu ya uwezo wako wa kuyaelewa.
Kwa sababu tumewaambia wawe na permit ndiopo wafanye kazi Tanzania ndio tumekuwa tunawakwamisha? 😀
 
Back
Top Bottom