Suala la Bandari TEC hawakupata kama walivyozoea


Simjibii Sheikh Muhammed Said isipokuwa nilitaka uangalie huyu Kardinali anavyokuambia yaani eti mupepewa jukumu na mungu kuulinda huu muungano ,

Kama Huo si udini ni kitu gani ??

Kardinali Pengo: Muungano si bahati nasibu​



- May 02, 2016

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka waamini na wananchi kwa ujumla kutambua kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar si jambo la bahati nasibu.

Kardinali Pengo ameyasema hayo ofisini kwake hivi karibuni alipoitisha vyombo vya habari vya Kanisa Katoliki kuzungumzia pamoja na mambo mengine ongezeko la Parokia mpya jimboni kwake pamoja na mabadiliko kwa Maparoko na Maparoko Wasaidizi katika baadhi ya Parokia jimboni humo.

Asemema suala la Muungano linapaswa kuchukuliwa kwa uzito wa pekee kwa kila Mtanzania hasa waamini Wakatoliki na kwamba kila mwamini anapaswa kutambua kuwa amepewa jukumu na Mwenyezi Mungu kulinda na kuombea Muungano huo.
 
Ingependeza kama focus ingekuwa katika mada husika kuliko kuzielekeza kwa Mohamed Said.
Mjadala wako wote umeelekea kwa Mohamed Said tu, na hakuna sehemu iliyojibu hoja.

Napata tabu sana kujibu andiko lako, kwa vile sipati mawazo yako katika mada husika.
 
Ahsante, ndio maana nilikushauri ufute bandiko #1 kwasababu huwezi kulitetea kwa hoja au mantiki.
Tatizo kubwa la Tanzania na watanzania ni kutokuwa na uvumilivu wa kusikia historia ya Tanzania hasa toka ukoloni mpaka sasa. Na mbaya zaidi ni kwa viongozi kuchagua nini kiandikwe na nini kisiandikwe (haswa ni historia toka 1961 mpaka leo). Hii ni mbaya sana katika kuandika historia ya nchi.

Nguruvi3, kama Mohamed Said aliyoyaandika hayaakisi ukweli katika mada asili, Tafadhali tufafanulie vipengele unavyoviona kakosea.
Na ikikupendeza hapa Jamvini andika upya historia kama unavyoijua wewe katika somo husika. Hapo sote tutafaidika na ni jukumu letu kuamini ya kwako au kuja na fikra mpya.
 
Pengine katika uandishi kunaweza kutokea hisia za hapa na pale. Lakini, je maudhui yanaukweli ukiacha hisia za mtoa thread?

Kinachokuuma ni kule kusikia historia inayotambua mchango wa kanisa katoliki kama taasisi kusaidia harakati za Uhuru wa Tanganyika. Na kama Waislam wangefanya hivyo kama taasis nani hangeacha kutambua mchango wao?
Kwa hivyo, kwa maoni yako Waislam hawakufanya hivyo kama Taasisi. Au unalenga nini katika kipengele hiki.
Waingereza husema: Kila kitokeacho, hutokea kwa sababu. Kama katika kusoma kwako historia, hukuona mchango wa waislam pengine kulikuwa na sababu na kusudio.

Kwa hiyo bwana Said, Mara nyingi ukweli una tabia ya kujipigania wenyewe na hudumu muda mrefu
Ukweli unaouzungumzia hapa ni upi?
 
Pengo ni askofu wa wakatoliki ameaddress akiwa kanisani unaitaje udini hivyo unafikiria sawa sawa
 
Kwamwewe, Hayo ni maoni yake binafsi kama Mtanzania mwingine. Na ndiyo maana nimetoa mfano awali kwamba akina Sykes na Waislam wengine walianzisha vuguvugu la kudai Tanganyika huru kama Watanganyika na si kwasababu ya Uislam wao. Hivyohivyo kwa Nyerere na wenzake.

Nakumbuka kipindi fulani Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam wa wakati huo alimfananisha RC Makonda na Yesu pamoja na/au mtume Mohammed, huwezi kusema hayo ni maoni ya Waislam wa Dar bali ulikuwa mtizamo wake binafsi.

Kwa hiyo Pengo ana Uhuru wa maoni yake kama Mtanzania mwingine, hisipokuwa angeyatoa kama tamko mfano walivyofanya TEC kwenye saga ya Bandari basi tungesema ni msimamo wa kanisa Katoliki Tanzania.
 
Vilevile bwana Kwamwewe, tofauti na Sheikh aliyetamka akiwa kwenye vikao vya kisiasa, umesema Pengo aliyatamka hayo maneno akiwa kanisani. Kanisani ndiyo dini yenyewe wala huo siyo udini.
 
Zawadi, husinilishe maneno. Hakuna sehemu niliyosema Waislam hawakuwa na mchango wowote. Ni Watanganyika wa dini zote na makabila yote walihusika kupigania Uhuru wa Tanganyika. Tumehamisha mada ya bandiko la Said, lakini ukilisoma bandiko lake la mwaliko wa Rais Vatican lina hisia kali za udini na ni la kichochezi.

Historia ya Tanganyika imeandikwa tangu enzi kabla ya utumwa hadi tulipopata Uhuru. Mzee Said hataki kusiki historia ya mtu anaeitwa Tip tip na biashara ya utumwa. Anataka Waarabu wapambwe kwamba walikuwa watu wema sana, walitujengea misikiti na madrasa. Hataki kusikia habari za Wamissionary wala shule na hospital walizozijenga. Ndiyo maana nikasema ukweli utabaki ukweli.
 
Kwani dini kujitenga na siasa wakati Wa Uhuru lilikiwa ni kosa?? Na waislam kuonekana walianzisha vuguvugu LA Uhuru ndo wanahaki sana kuliko wengine???
 
Nakuunga mkono
 

Hayo maoni ya kulinda anawaambia nani ?? kwani Zanzibar ni mali ya kanisa hata wafuasi wake walinde ??
 
Vilevile bwana Kwamwewe, tofauti na Sheikh aliyetamka akiwa kwenye vikao vya kisiasa, umesema Pengo aliyatamka hayo maneno akiwa kanisani. Kanisani ndiyo dini yenyewe wala huo siyo udini.
Kwani kwenye Biblia imeandikwa mungu aliwaambia wakristo walinde muungano ?? Huu muungano si wa hiari ?? Wazanzibari wakati wote wanasema hawautaki muungano , kwa nini yeye atake kuulinda tena na kumhusisha Mungu ??
 
Ni kweli unayosema na kwa kuongezea tu Historia haiandikwi bali inawasilishwa. Historia hujiandika yenyewe sisi wanadamu tunainukuu nakuiwakilisha kama ilivyotokea na si kama tunavyodhani
Mbona umesoma bandiko moja na kufikia tamanati! Nilipomwambia afute bandiko nilikuwa na sababu za msingi na moja ni kumsetiri kwasababu bandiko lipo chini ya viwango. Hebu pitia mabandiko haya #46 ,#47 #54 #60 nakuendela utabaini nimeeleza kwanini afute

Pili, mada si Historia bali yatokanayo na video ya Ansbert Ngurumo ambayo Mohamed ameiweka mwenyewe
Badala ya kujenga hoja, kutetea hoja au kubomoa hoja kwa kutumia Video katika haya hapa chini ameingia kwingine. Hoja ni hizi

1. Ziara ya Rais Vatcan
2. Uarabu na DP
3 Chadema na Ukatoliki, Waislam na CCM

Kinachoshangaza ni kusikia Nyerere, Mtikila , Mwinyi, Mabucha ya Nguruwe, Abdul Sykes n.k. vikitawala mjadala bada ya hoja alizoleta mwenyewe. Sijui kwa wengine mlisoma , kwasisi wenye elimu ya kubabaisha hili linatupoteza, tunashindwa kujua mjadala unahusu nini.

Lakini pia jiulize ikiwa ndio mada imewasilishwa mbele ya kadamnasi halafu hakuna mpangilio wa hoja hiyo si mada ni vurugu.

Nilipomshauri afute bandiko lake, si kwamba linakera, si kwamba lina maudhui mabaya bali nilifahamu hoja ni nyepesi na hawezi kuzijengea hoja, au kuzitetea kwa mantiki .

Ndicho kinachotokea kwamba tunapuyanga kwa Abdul Sykes n.k. hatujali tena mada aliyowasilisha
 
wewe ni nuts yaani umeandika uzi kuhusu Zanzibar na Mungano halafu unajijibu mwenyewe , hata sijui umekuja hapa kufanya nini . Si uanze kufuta lile bandiko lako kwanza
Yes nimeandika sana kuhusu Zanzibar na Muungano na kuanika uozo wake. Watanganyika wamejua mengi
Sikujua kama kuna Wasomaji wengi ukiwemo, nitarejea tena kuendelea.

Mada iliyopo hapa ni kuhusu Video ya Mo na hoja alizotoa.
Kuhusu uwepo wangu hapa ! mbona ni mwenyeji sana miongo mingi tu, Mo anajua !
 

Mbona umejifungia ndani ya uzi wako hutaki watu wengine wachangie , unaogopa ukweli ? Pumba tupu umejaza kwenye uzi
 

Anza kufuta bandiko lako ulilowazuia watu kuchangia hoja zako Za kipuuzi. Chadema nilikuwa nawaumga mkono sana kabla lakini walipokuja na hoja Za kitoto Za kidini Za DP nimewashtukia kumbe ni mamluki wa Roma
 
Hekaya za Mohamed Said
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…