kwamwewe
JF-Expert Member
- Jul 15, 2010
- 1,908
- 604
Said, sikatahi mtizamo wako. Inaweza ikawa kweli kwamba wengi tunakusoma kwasababu tunataka kujua kiwango cha chuki za udini mlionao Waislam dhidi ya ukristo hasa Ukatoliki, lakini ushahuri wangu ulilenga uandike makala bila kuingiza ushabiki na chuki za kidini.
Hakuna mtu yoyote ambae alifuta au kupotosha historia ya Waislam na Uislam. Labda nikwambie palipo na shida. Sykes na Waislam wenzake kwa mfano, walianzisha vuguvugu la uhuru kama Watanganyika na siyo kama Waislam. Na Nyerere nae pamoja na waklisto wengine waliungana nao kama Watanganyika siyo kama Wakristo au Wakatoliki. Kilichowaunganisha baba zetu hawa ni dhamira yao ya kutafuta Uhuru wa Tanganyika siyo Imani ya dini zao. Kinachokuuma ni kule kusikia historia inayotambua mchango wa kanisa katoliki kama taasisi kusaidia harakati za Uhuru wa Tanganyika. Na kama Waislam wangefanya hivyo kama taasis nani hangeacha kutambua mchango wao?
Kwa hiyo bwana Said, Mara nyingi ukweli una tabia ya kujipigania wenyewe na hudumu muda mrefu.
Simjibii Sheikh Muhammed Said isipokuwa nilitaka uangalie huyu Kardinali anavyokuambia yaani eti mupepewa jukumu na mungu kuulinda huu muungano ,
Kama Huo si udini ni kitu gani ??
Kardinali Pengo: Muungano si bahati nasibu
- May 02, 2016
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka waamini na wananchi kwa ujumla kutambua kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar si jambo la bahati nasibu.
Kardinali Pengo ameyasema hayo ofisini kwake hivi karibuni alipoitisha vyombo vya habari vya Kanisa Katoliki kuzungumzia pamoja na mambo mengine ongezeko la Parokia mpya jimboni kwake pamoja na mabadiliko kwa Maparoko na Maparoko Wasaidizi katika baadhi ya Parokia jimboni humo.
Asemema suala la Muungano linapaswa kuchukuliwa kwa uzito wa pekee kwa kila Mtanzania hasa waamini Wakatoliki na kwamba kila mwamini anapaswa kutambua kuwa amepewa jukumu na Mwenyezi Mungu kulinda na kuombea Muungano huo.