Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

Chige

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2008
Posts
13,495
Reaction score
29,872
Nafahamu kwamba watu wengi wameanzisha threads wakijaribu kuelezea suala la CAG Kisheria! Hata hivyo, wengi wao kama sio wote walichofanya ni kurundika vifungu vya kisheria bila kutoa ufafanuzi!

Mbaya zaidi, hawatoi ufafanuzi wa matumizi ya neno SHALL kwa mujibu wa sheria zetu! Nimelazimika kuanzisha uzi huu ili kuondoa mapungufu yote hayo.

Tuendelee.

Bila kujaza vifungu vingi, Katiba yetu Ibara ya 144 (1) inasema wazi kwamba:-
Controller and Auditor-General of the United Republic shall be obliged to vacate office upon attaining the age of sixty or any other age which shall be prescribed by a law enacted by Parliament.
Kwamba, CAG ATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 60 au umri mwingine wowote utakaotajwa na sheria zilizotengenezwa na Bunge!

SWALI 1: Je, Profesa Mussa Assad amefikisha miaka 60?! Jibu HAPANA kwa sababu kumbukumbu zinaonesha amezaliwa Oktoba 06, 1961... kwa maana nyingine, atafikisha miaka 60 Oktoba 5, 2021.

SWALI 2: Je, Bunge limetaja huo UMRI MWINGINE WOWOTE?!

Jibu linapatikana kwenye Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma, yaani Public Audit Act ya mwaka 2008, Ibara ya 6(2)(a) inayosema:-
Unless the question of removal becomes the subject of investigation in terms of Article 144(3) of the Constitution, the Controller and Auditor-General shall vacate office upon attaining the age of sixty five years;

Kumbe, Bunge likatunga sheria kwamba badala ya miaka 60, hatimae CAG ATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 65. Tumeona Prof Assad ndo kwanza ana miaka 58.

SWALI 3: Nini hutokea CAG akimaliza miaka 5 ya kwanza?!

Hapa tena jibu linapatikana kutoka Public Audit Act 2008 Ibara ya 6 (1) inayosema:-
The Controller and Auditor-General shall hold office for the fixed term of five years and shall be eligible for renewal for one term only.
Hapo kwenye neno SHALL ndipo panapozua mgogoro!!

Watetezi wa uamuzi wa Rais wanasema neno SHALL sio shuruti! Kwa bahati mbaya sana, tafsiri yao wanaitoa kichwani na sio kwa mujibu wa sheria zetu!

Kwa mujibu wa sheria zetu, na kwa kuangalia Interpretation of Laws Act Ibara ya 53 (1&2) inasema kwamba:- Kumbe, kwa mujibu wa sheria zetu, pasipo na SHURUTI hutumika neno MAY lakini linapotumika neno SHALL, hiyo ni SHURUTI!

Kwa maana nyingine, Public Audit Act inaposema "...and shall be eligible for renewal for one term only. Hapo suala la renewal ni SHURUTI kama ilivyosema Interpretation of Laws Act 53 (2).

Itakuwa sio SHURUTI either kama ameshafikisha miaka 65, au kama ambavyo 2008 Public Audit Act Ibara ya 6(2)(a) inavyosema kwamba:-
Unless the question of removal becomes the subject of investigation in terms of Article 144(3) of the Constitution, the Controller and Auditor-General shall vacate office upon attaining the age of sixty five years;
Kwa maana nyingine, kwavile Prof Assad hajafikisha miaka 65, hapo tafsiri yake ni kwamba AMETUMBULIWA na sio kwamba muda wake umeisha!!

Na CAG atatumbuliwa "...Unless the question of removal becomes the subject of investigation in terms of Article 144(3) of the Constitution."

Hiyo Ibara ya 144(3) ya Katiba yetu inasemaje? Jibu ni hili:-If the President considers that the question of the removal of the Controller and Auditor-General from office under the provisions of this Article needs to be investigated, then the procedure shall be as follows: Kama tulivyoona hapo juu, CAG atalazimika kuachia ofisi endapo atakuwa amefikisha miaka 65, kinyume chake anaweza KUTUMBULIWA kabla ya huo umri ikiwa ametenda jambo linalohitaji investigation.

Hivyo basi, ni ama Rais atengue uamuzi wake wa awali wa kuteua CAG mwingine, au tuone akiunda Tume ya Kijaji ya Kumchunguza CAG kwa kosa analojua yeye na timu yake!!

CAG akiongezewa miaka mingine 5, ataimaliza akiwa na umri wa miaka 63... umri halali kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma ya mwaka 2008!![/QUOTE]




Zaidi soma:

 
Shall inayoongelea term limits mnaitafsiri vibaya.

Pia, likatiba lenyewe limejaa vituko linatakiwa kurekebishwa.

Ukiandika "shall be eligible for renewal" hapo ulazima unaongelewa kwenye eligibility. Eligibility ni potential ya kuwa CAG, si lazima aliye eligible kuwa CAG.

Mtu anaweza kuwa eligible voter, halafu akawa si voter.

Katiba inasema rais hawezi kuendelea kuwa rais baada ya vipindi vya urais viwili.

Je, hilo lina maana rais ni lazima awe rais kwa vipindi viwili vya urais?

Kama CAG anatakiwa kuwa CAG kwa miaka kumi, kwa nini mkataba wake ni wa miaka mitano?
 
Watanzania tuamke, Katiba ya mwak 1977 ina-limit mihula miwili ya miaka mitanomitano, ndiyo maana kabla ya hiyo katiba muda wao ulikuwa unabadilika.

Heb tupitie historia kidogo.


Yaani prof. Assad anavyochukiwa, hadi picha yake kwenye website (National Audit Office of Tanzania » The CAG) walishafuta kwenye orodha ya ma-CAG.

-Je, kafikisha miaka 60? (Mussa Juma ASSAD Born : 6 October 1961)
-Je, sheria ilibadilishwa lini kustaafishwa kabla ya miaka 60? (Mandatory retirement also known as enforced retirement or compulsory retirement)
-Je, anaumwa ama ametiwa hatiani na tume ya maadili?
-Je, Rais amefuata katiba inavyosema?


 
Unajua kuwa CAG ana kaa ofisi kwa vipindi visivyozidi viwili vya miaka mitano mitano?
 
Tumtakie CAG Mstaafu, Prof. Mussa Assad kustaafu kwema na amestaafu kwa heshima na kwa mujibu wa sheria na sio kwa hoja zozote za vitatange na vibirifitina, jina lake litaandikwa kwenye kile kitabu cha mashujaa wa kweli wa taifa wetu kwasababu ameacha Legacy.

Karibu CAG Mpya, Charles Kicheere, tunakutakia kazi njema.
Paskali
 
 
Ndo keshaondoka sasa wengine waendelee.
 
Legacy ipi p naona unauma na kupuliza

State agent
 
Hii comment yako Leo unaipaste kila kona kwenye uzi wa Prof Assad

Hutaki kujisumbua mkuu wala kuumiza kichwa au upo na John Mtembezi hapo aka John walker imepanda
 
Pongezi kubwa kwa Prof. Assad kwa utumishi uliotukuka, ijapokuwa weledi na maadili yako ulikuwa mwiba kwa wengine. Kwa hakika historia yako imeandikwa kwa wino wa dhahabu, ambapo si ajabu ukaaminiwa na IMF ama WB na kukabidhiwa nafasi mpya unayostahili.

Aidha, pongezi pia kwa CAG mteule, mtangulize Mola mbele kwa nafasi hii mpya ulioaminiwa na kukabidhiwa kwa maslahi mapana ya uzalendo na taifa letu, hilo ni kama zigo la misumari endapo utaweka maadili na weledi kando ili upate kufuraisha watu fulani, haswa kwa yale yenye makandokando mengi.
 
Huku nikuonyesha ukomavu. Safi P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…