Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

Rais amefuata taratibu;

Maamuzi yake yametokana na tafsiri sahihi ya sheria.

Kwakuwa kaongozwa na sheria katika kufanya maamuzi, ni sahihi kusema kuwa amefuata taratibu.

Mimi nataka tu kujua kuwa, wanaodai rais kavunja katiba, wanadai hivyo kwa mujibu gani?

Wanasadiki au?
 
Zaidi soma:

Mtaalamu wa sheria hebu tusaidia kifungu cha 40 (i) cha Katiba inasema hivi:
40.-(1) Subject to the other provisions of this Article, any person who holds office as President shall be eligible for re-election to that office. (2) No person shall be elected more than twice to hold the office of President.

Hapo "SHALL" inamaana kama ulivyoeleza hapo juu??!!
[/QUOTE]Look at you guys... hapa tunazungumzia sheria kuhusu CAG na sio kuhusu rais!! Nyie watu vipi?! Ndo reference gani ya sheria inayofanya hivyo?!

Kama mnadhani reference kisheria ndo inakuwa hivyo, kwenye Ibara hiyo hiyo ya 40, Ibara ndogo ya pili inasema:-
No person shall be elected more than twice to hold the office of President.
Je, unataka kusema kuna option ya kuweza kuchaguliwa zaidi ya mara mbili?!

Isitoshe, hiyo ibara ya 40 (1) inasema:-
Subject to the other provisions of this Article, any person who
holds office as President shall be eligible for re-election to that office.
As a Bush Lawyer, my legal opinion suggests hiyo ibara imekosewa, na ilitakiwa isomeke kama:-
Subject to the other provisions of this Constitution, any person whoholds office as President shall be eligible for re-election to that office.
Hiyo ni kutokana na ukweli kwamba, Katiba (sio named article) imetaja sifa za mtu kugombea urais, kwahiyo wakati anapokuwa na hiyo sifa ya re-election, inabidi sifa hiyo isi-violate vifungu vingine vya katiba!!

Kwa mfano, Katiba yetu kwa sasa, kama sikosei Ibara ya 38, inataka mtu anayegombea urais apendekezwe na chama cha kisiasa! Kwahiyo Article 40(1) ingesema "subject to the provisions of this constitution", hapo hiyo re-election ingefanya reference kwenye vifungu vingine vya katiba na sio ibara!!

All in all, mjadala ni uteuzi wa CAG na sio uchaguzi wa Rais ambao sifa na utaratibu wa uchaguzi/uteuzi wao ni tofauti!
 
Kama sheria inataka CAG atumikie mihula miwili, kwa nini isiseme tu moja kwa moja kuwa hivyo ndivyo itavyokuwa?

Kwanza, kwa nini kuwepo hata na mihula miwili?

Kwa nini term isiwe fixed for 10years?

Sikubaliani na tafsiri ya Shivji.

And yes, I can disagree with him.
Hukubaliani na Shivji kwa vile ni mgumu kuelewa. Miaka mitano inaacha lope holes kwa Rais kumuundia tume ya kumchunguza ili aondolewe in case inabidi iwe hivyo kwa sababu zilizotajwa kwenye sharia husika. Hivyo ndivyo ilivyo na tunajadili kutokana na katiba ilivyo kwa sasa ukisema kwanini isingekuwa vipi sijui, ndo haiko ivyo sasa
 
Kama sheria inataka CAG atumikie mihula miwili, kwa nini isiseme tu moja kwa moja kuwa hivyo ndivyo itavyokuwa?

Kwanza, kwa nini kuwepo hata na mihula miwili?

Kwa nini term isiwe fixed for 10years?

Sikubaliani na tafsiri ya Shivji.

And yes, I can disagree with him.

zipo sababu nyingi
1. Moja inawezekana kabisa CAG yeye mwenyewe baada ya kazi ngumu ya miaka mitano, kiroho safi tu yeye mwenyewe akataka kupumzika.

2.Au Inawezekana kwa nia njema kabisa na za manufaa kwa taifa zikawepo sababu za CAG kung'olewa kwa mfano tabia mbaya na mwenendo mbaya au na ufanisi basi ikatakiwa asiweze kupewa term ya pili, lakini kwa Sababu ofisi ya CAG inahitaji independence ya hali ya juu si busara kumpa Mteuzi mamlaka ya kumfire CAG kirahisi kwa hiyo inaweka option ya kumuondoa after 5 years lakini kumuondoa kwenye kuwe na sababu genuine ndiyo maana akapewa option ya kutumia hiyo ibara ya 144(3) ambayo ni ngumu ngumu kidogo kumng'oa CAG lakini kama zipo sababu za msingi na evidence basi anang'oka tu.

Hii ndiyo hekima ya miaka mitano mitano
 
Nope!

Shall is a modal verb which expresses a necessity.

It means the same thing across the board.

If it doesn’t, show me, with authority, where it means totally something else.
Your interpretation is based on general English use but not a legal definition/interpretation of our own laws! Our INTERPRETATION OF LAWS ACT says:-
SHALL2.png

Frankly speaking, the word is confusing if there's no legal definition/interpretation, but we have one! It's from this confusion that's why other countries including the United States replace the word SHALL with MUST, but we haven't!

They decided to drop the word SHALL because when the law schools teach SHALL is mandatory, in the common use it's not mandatory!
 
Inatambulika huo mwaka wa kuongeza anayeuidhinisha ni Mh.Rais.
Lazima kuna kipengele kinampa nguvu Mh.Rais kuendelea kumpa ziada hiyo CAG au kuteua mwingine.
 
Hukubaliani na Shivji kwa vile ni mgumu kuelewa. Miaka mitano inaacha lope holes kwa Rais kumuundia tume ya kumchunguza ili aondolewe in case inabidi iwe hivyo kwa sababu zilizotajwa kwenye sharia husika. Hivyo ndivyo ilivyo na tunajadili kutokana na katiba ilivyo kwa sasa ukisema kwanini isingekuwa vipi sijui, ndo haiko ivyo sasa

Na wewe unakubaliana naye kwa sababu huelewi.
 
We will miss you Proff Assad.
You are loved by many.
 
Nafahamu kwamba watu wengi wameanzisha threads wakijaribu kuelezea suala la CAG Kisheria! Hata hivyo, wengi wao kama sio wote walichofanya ni kurundika vifungu vya kisheria bila kutoa ufafanuzi!

Mbaya zaidi, hawatoi ufafanuzi wa matumizi ya neno SHALL kwa mujibu wa sheria zetu! Nimelazimika kuanzisha uzi huu ili kuondoa mapungufu yote hayo.

Tuendelee.

Bila kujaza vifungu vingi, Katiba yetu Ibara ya 144 (1) inasema wazi kwamba:-
Kwamba, CAG me mgeni haya mamboATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 60 au umri mwingine wowote utakaotajwa na sheria zilizotengenezwa na Bunge!

SWALI 1: Je, Profesa Mussa Assad amefikisha miaka 60?! Jibu HAPANA kwa sababu kumbukumbu zinaonesha amezaliwa Oktoba 06, 1961... kwa maana nyingine, atafikisha miaka 60 Oktoba 5, 2021.

SWALI 2: Je, Bunge limetaja huo UMRI MWINGINE WOWOTE?!

Jibu linapatikana kwenye Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma, yaani Public Audit Act ya mwaka 2008, Ibara ya 6(2)(a) inayosema:-

Kumbe, Bunge likatunga sheria kwamba badala ya miaka 60, hatimae CAG ATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 65. Tumeona Prof Assad ndo kwanza ana miaka 58.

SWALI 3: Nini hutokea CAG akimaliza miaka 5 ya kwanza?!

Hapa tena jibu linapatikana kutoka Public Audit Act 2008 Ibara ya 6 (1) inayosema:-Hapo kwenye neno SHALL ndipo panapozua mgogoro!!

Watetezi wa uamuzi wa Rais wanasema neno SHALL sio shuruti! Kwa bahati mbaya sana, tafsiri yao wanaitoa kichwani na sio kwa mujibu wa sheria zetu!

Kwa mujibu wa sheria zetu, na kwa kuangalia Interpretation of Laws Act Ibara ya 53 (1&2) inasema kwamba:-
Kumbe, kwa mujibu wa sheria zetu, pasipo na SHURUTI hutumika neno MAY lakini linapotumika neno SHALL, hiyo ni SHURUTI!

Kwa maana nyingine, Public Audit Act inaposema "...and shall be eligible for renewal for one term only. Hapo suala la renewal ni SHURUTI kama ilivyosema Interpretation of Laws Act 53 (2).

Itakuwa sio SHURUTI either kama ameshafikisha miaka 65, au kama ambavyo 2008 Public Audit Act Ibara ya 6(2)(a) inavyosema kwamba:-Kwa maana nyingine, kwavile Prof Assad hajafikisha miaka 65, hapo tafsiri yake ni kwamba AMETUMBULIWA na sio kwamba muda wake umeisha!!

Na CAG atatumbuliwa "...Unless the question of removal becomes the subject of investigation in terms of Article 144(3) of the Constitution."

Hiyo Ibara ya 144(3) ya Katiba yetu inasemaje? Jibu ni hili:-If the President considers that the question of the removal of the Controller and Auditor-General from office under the provisions of this Article needs to be investigated, then the procedure shall be as follows:Kama tulivyoona hapo juu, CAG atalazimika kuachia ofisi endapo atakuwa amefikisha miaka 65, kinyume chake anaweza KUTUMBULIWA kabla ya huo umri ikiwa ametenda jambo linalohitaji investigation.

Hivyo basi, ni ama Rais atengue uamuzi wake wa awali wa kuteua CAG mwingine, au tuone akiunda Tume ya Kijaji ya Kumchunguza CAG kwa kosa analojua yeye na timu yake!!

CAG akiongezewa miaka mingine 5, ataimaliza akiwa na umri wa miaka 63... umri halali kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma ya mwaka 2008!!

Zaidi soma:

[/QUOTE]
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi ya Taifa Na. 11 ya Mwaka 2008 kifungu cha 6(1) "basic tenure" ya CAG ni miaka mitano na sheria inasema anaweza (Shall) kutumikia vipindi viwili vya miaka mingine mitano.

CAG anaulinzi mkubwa kisheria na moja ya ulinzi wake ni kuwa akiwa katikati ya tenure yake hawezi kuondolewa hivi hivi bila masharti kadhaa kufuatwa, lazima utumie masharti ya Ibara ya 144(3) ya Katiba au yeye mwenyewe achukue hatua under subsestion 2 ya hiyo Sheria ya Ukaguzi niliyoitaja hapo juu. Lakini kwa ujumla anaweza kuondolewa, si ngumu. Nitaeleza.

View attachment 1253918

Matumizi ya neno "Shall" lililotumika katika Sheria ya Ukaguzi kwenye kifungu cha 6 .

Kwa heshima na taadhima, Sheria hapo haijakusudia ulazima na ndio maana sheria haifasiriwi kwa matakwa ya mtu bali sheria zenyewe zinavyokusudia kufasiriwa katika muktadha wa jambo husika na lengo la mtunga sheria.

Katika muradi wa sheria na taratibu za kiutawala (admimistrative law point of view) sheria zinajulikana kuwa zitajitafsiri zenyewe na msingi unaokubalika ni kuwa kila ambapo tenure inapomalizika na kuwepo kwa kanuni ya kuongezewa tena kipindi cha pili neno "Shall" halina maana kama ilivyo katika Sheria ya Kufasiri Sheria (The Interpretation of Laws Act), hapa maana huwa ya kimazingira zaidi (contextual meaning) na haiwi LAZIMA bali INAWEZA.

Na moja kwa moja ni kuwa kuongezewa kipindi cha pili Mtendaji yeyote mwenye vipindi viwili na hata Rais mwenyewe sio "automatic" lazima kuwe "subject to good performance."

Na anayeamua akuongezee tenure ya pili, hiyo sheria haijambana, ni yule yule mwenye mamlaka ya kuteua na kukutengua.

Rais anapewa mamlaka hayo kwa CAG na watendaji wengine Serikali aliowateua kwa sheria yoyote kwa mamlaka aliuonayo katika Ibara ya 36. Tena 36(3) ndio inampa mamlaka ya jumla zaidi ya kudeal na tatizo lolote kwa nia ya kuweka utulivu katika utumishi kwa kuweza kumtengua mtu yeyote aliyemteua.

View attachment 1253920

Ukifasiri neno "shall" katika Sheria ya Ukaguzi ili kumtetea CAG Assad kwamba ilikuwa lazima aendelee miaka mitano ya pili ni kuleta dhahama kubwa nchini inayoweza kushawishi hata Uchaguzi Mkuu wa Mwakani usifanyike. Najua utashangaa!!!

Ndio, tafsiri ya Zitto na wenzake ni ya hatari zaidi kwa nchi kwani ukisoma Ibara ya 40 ya Katiba inapozungumzia Rais aliyeko madarakani kwa kipindi cha miaka mitano ya mwanzo kuwa anaweza kuchaguliwa tena kwa miaka mingine mitano ya pili na ya mwisho neno lililotumika ni "shall."
View attachment 1253921


Kama tafsiri SISISI na "#shallow" ya ACT ni ya kufuatwa basi kwa muktadha wa neno "Shall" pia katika Ibara ya 40 ya Katiba, Rais Magufuli naye mwakani hakuna haja ya kupimwa utendaji wake kwa kurudi katika sanduku la kura, aendelee tu, kusiwe na uchaguzi, aapishwe moja kwa moja kuendelea na Urais maana "shall" ina maana ya LAZIMA.

Lakini hapana, muradi wa "shall" katika masuala ya utawala sio kama inavyotumika katika sheria za kawaida, hapa bado dhana ya mhusika kuwa "subjected to good performance" kwa kutazamwa utendaji wake kama unaridhisha mamlaka ya uteuzi (kwa kesi ya CAG) na kwa kurudi kuomba kura tena kwa wananchi (kwa kesi ya Rais) ndio utaratibu kabla ya kulamba awamu ya pili.

Kitaalamu ni kuwa CAG aliyemaliza muda wake hakuonewa na kama ni kuonewa au aliyemteua ana nia mbaya angeweza kuondolewa hata kabla hajamaliza miaka hii mitano.

Ibara ya 144(2) inampa madaraka Rais kumuondoa CAG kwa sababu ya utendaji mbovu, maradhi au sababu nyingine yoyote.

View attachment 1253922

Nimeona wengi wanasema Rais hawezi kufanya hivyo mpaka aunde Tume, si kweli. Watanzania tuachane na kasumba ya kutosoma kwa umakini.

Tuzisome sheria vyema na tunaposhindwa kuelewa tuwatafute wataalamu sio wanasiasa.

Katika Ibara ya 144(3) Rais ataunda Tume (If) kwa maana ya "kama" ataona kuchunguza sababu hizo za kumuondoa CAG kunafaa kuchunguzwa. Maana yake akijiridhisha hana haja ya kuunds Tume.

View attachment 1253923

Kisheria na Kikatiba, namsifu sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk Magufuli na wataalamu wake wa sheria, hakika ni wabobezi, wanazisoma sheria zetu kwa utulivu na kuzifasiri kwa mujibu wa viapo vyao.

Naamini Rais Mhe. Dk Magufuli hakuwa na jambo baya la kutaka kumfukuza CAG isipokuwa "subject to good performance" anahitaji kasi zaidi katika eneo hilo na utulivu zaidi na kuaminika zaidi kwa kiongozi wa muhimili huo ambako Assad alishafeli kwa kufikia hatua ya kugombana na mhimili wa Bunge.

Kwa uchambuzi huu kudai Rais kavunja Sheria ni uchochezi mkubwa usiofaa kufumbiwa macho.


/chanzo Wakili wa Kujitegemea fb
Huyu kweli ni mwanasheria aliyebobea kwenye sheria na anachambua kisheria akiwa ametulia!
 
Zaidi soma:

Usiniambie SOMA threads ambazo nimeshasoma, na ndio maana mwanzoni tu mwa thread yangu nimezungumzia hizo threads zingine!

Toa hoja yako kupitia hizo threads zingine!
 
Mbona kuna nguvu nyingi sana inatumika kutetea hili swala? Mwenzio anakwambia ata mwaka mmoja anakuondoa.

Tukubali tu Magufuli anapenda kuvunja katiba.
Katiba ipi mkuu? Kaisome vizuri Katiba ibara ya 144 na Sheria ya Ukaguzi kifungu Na. 6 ukiwa umetulia neno kwa neno pia unaweza kusoma ibara ya 36 ya Katiba then urudi hapa useme amevunja ibara ipi? Usiwe na mhemuko mkuu kama unataka kuelewa!
 
zipo sababu nyingi
1. Moja inawezekana kabisa CAG yeye mwenyewe baada ya kazi ngumu ya miaka mitano, kiroho safi tu yeye mwenyewe akataka kupumzika.

Kwa hiyo CAG akishateuliwa haruhusiwi kabisa kuondoka kwenye hiyo nafasi kabla ya kipindi cha miaka mitano? Vipi kama baada ya miaka miwili akaamua kuachia ngazi? Hawezi tu kusema kuwa ‘nimechoka na nimeamua kujiuzulu’ kabla ya miaka mitano kuisha?

2.Au Inawezekana kwa nia njema kabisa na za manufaa kwa taifa zikawepo sababu za CAG kung'olewa kwa mfano tabia mbaya na mwenendo mbaya au na ufanisi basi ikatakiwa asiweze kupewa term ya pili, lakini kwa Sababu ofisi ya CAG inahitaji independence ya hali ya juu si busara kumpa Mteuzi mamlaka ya kumfire CAG kirahisi kwa hiyo inaweka option ya kumuondoa after 5 years lakini kumuondoa kwenye kuwe na sababu genuine ndiyo maana akapewa option ya kutumia hiyo ibara ya 144(3) ambayo ni ngumu ngumu kidogo kumng'oa CAG lakini kama zipo sababu za msingi na evidence basi anang'oka tu.

Hii ndiyo hekima ya miaka mitano mitano

So let me get this straight, hapa ni wewe unasadiki, siyo?

Au kuna sehemu umeyatoa haya maelezo?
 
Mkuu ule utaratibu ni wa wazi sio wa kificho. Majaji wa ndani na nje wanahusika. Sote tungejua

Wa wazi kivipi? Ni kwamba kunakuwa na matangazo magazetini, redioni, runingani?

Na proceedings zake zinakuwa open to the public au?
 
Magufuli hajavunja kifungu chochote cha katiba.

Wanachoshindwa kuelewa watu wengi ni gist ya Ibara ya 144, ambayo lengo lake ni kuweka utaratibu wa kumuondoa CAG ndani ya muda wake alioteuliwa wa miaka mitano.

Katiba linapokuja swal la tenure of office of CAG ipo silent.

Office of CAG ni zao la sheria ya Bunge ambayo ni THE PUBLIC AUDIT ACT,2008, hii ndio imeestablish office of CAG baada ya Constitution kuitambua, hivyo basi kwakua kuna parent ACT inayo establish hiyo office linapokuja swala la tenure ya office of CAG lazima turely na provisions za hiyo parent act.

Sasa parent act kwa office ya CAG imeset time limit ya five years na renewal of another one term only , hivyo kama akifaninkiwa kuwa na term nyingine hapaswi kuzidi ten years,

Kama kusudio la sheria ni kwa CAG Kuserve kwa muda wa miaka kumi ilishindikana nini kusema hivyo katika hicho kipengele. Ili kuondoa utata sheria imgesema wazi kabisa kuwa tenure yake ni two terms of five years each,lkini sheria haijasema hivyo, kilichopo ni fixed period of five years .

Wnachoshn dwa kuelewa hapa hawa watu ni kuwa CAG was not removed from office, his tenure expired thus he was replaced.

Linapokuja swala la replacement sasa huko Ibara ya 144 haihusiki, ila kamma ni rem oval basi section 7 y Public Audit Act, na Ibara ya 144 vinahusika.
Kwa nini unasema Katiba iko sikent kwenye kumuondoa CAG wakati ime stipulate soecific conditions za CAG kuondolewa, zikiwa ni ugonjwa, umri au impeachment tribunal?

Mbona vioengele viko wazi na vime stipulate very specifically? Kwa maneno yenye ckear logic kama unless.
 
Mtaalamu wa sheria hebu tusaidia kifungu cha 40 (i) cha Katiba inasema hivi:
40.-(1) Subject to the other provisions of this Article, any person who holds office as President shall be eligible for re-election to that office. (2) No person shall be elected more than twice to hold the office of President.

Hapo "SHALL" inamaana kama ulivyoeleza hapo juu??!!
Look at you guys... hapa tunazungumzia sheria kuhusu CAG na sio kuhusu rais!! Nyie watu vipi?! Ndo reference gani ya sheria inayofanya hivyo?!

Kama mnadhani reference kisheria ndo inakuwa hivyo, kwenye Ibara hiyo hiyo ya 40, Ibara ndogo ya pili inasema:-Je, unataka kusema kuna option ya kuweza kuchaguliwa zaidi ya mara mbili?!

Isitoshe, hiyo ibara ya 40 (1) inasema:-As a Bush Lawyer, my legal opinion suggests hiyo ibara imekosewa, na ilitakiwa isomeke kama:-Hiyo ni kutokana na ukweli kwamba, Katiba (sio named article) imetaja sifa za mtu kugombea urais, kwahiyo wakati anapokuwa na hiyo sifa ya re-election, inabidi sifa hiyo isi-violate vifungu vingine vya katiba!!

Kwa mfano, Katiba yetu kwa sasa, kama sikosei Ibara ya 38, inataka mtu anayegombea urais apendekezwe na chama cha kisiasa! Kwahiyo Article 40(1) ingesema "subject to the provisions of this constitution", hapo hiyo re-election ingefanya reference kwenye vifungu vingine vya katiba na sio ibara!!

All in all, mjadala ni uteuzi wa CAG na sio uchaguzi wa Rais ambao sifa na utaratibu wa uchaguzi/uteuzi wao ni tofauti!
[/QUOTE]
Umeshasema kuwa wewe ni bush lawyer then sitegemei ukaweza ku interpretate Katiba ya Sheria vizuri. Hii ni professional ya watu mkuu!
 
Back
Top Bottom