Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Absolutely trueKatiba unayoongelea ni katiba ipi?
Kukanyaga katiba kama unaonyesha ni kutafuata katiba, Je nani anafuata katiba hapa Tanzania?
Wakati tunajadili rasmu ya warioba mlijadili kichama na kupinga hoja kwa kufunika kombe, Leo unakuja na story za Kukanyaga katiba
Nyie kama wana ccm mlikanyaga rasmu ya maoni ya wananchi, Tulikaa kimya
Sasa ndani ya chama mwisho wenu kupiga kura ilikuwa 2015,Kwa sasa hata ukishinda kura za maoni mwenyekiti anaweza kukata jina ndani ya ccm
Mwaka 2020 ndio utajua picha ni ya kichina au kisukuma
Ben Saanane aliongelea sana PhD ya huyu jamaa. Kama yeye anaweza kupata PhD, nani atashindwa??Mjadala mzito sana unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii hapa nchini hivi sasa ni iwapo Rais Magufuli alikuwa sahihi kikatiba kumwachisha kazi CAG, Profesa Assad, kabla ya kufikisha umri wa kustaafu kwa lazima atakapofika umri wa miaka 60
Tutambue pia kuwa Profesa Assad, hivi sasa amefikisha umri wa miaka 58
Nimeipitia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 144, na sijaona mahali popote palipoelezea kuwa CAG, anaweza kuachishwa kazi mara tu amalizapo kipindi chake cha kwanza cha miaka 5, hoja inayopigiwa debe sana na hao watetezi wa serikali, waliomwachisha kazi, Profesa Assad
Hata hivyo nije kwenye kipengele cha pili, ambacho kwangu Mimi ndicho nilichokiiona cha hatari zaidi, pale nilipomsikia Rais Magufuli akimsisitizia, huyo CAG mpya, Charles Kicheere, kuwa aende akachape kazi na asifikiri kuwa hiyo nafasi yake ni mhimili mwingine na akaendelea kusisitiza kuwa awe mtii kwa mihimili mingine ya Bunge na Mahakama na asithubutu kubishana nayo na akaendelea kusisitiza kuwa yeye nafasi yake ni ya utumishi wa kukagua huesabu za serikali pekee na akaendelea kumpiga mkwara mzito kuwa kwenye mamlaka ya kidunia, haiwezekani Rais apewe mamlaka ya kuteua bila pia kupewa mamlaka ya kutengua!
Akaendelea kumpiga mkwara mzito huyo CAG mpya kuwa anaweza akadumu kwenye nafasi yake kwa mwaka mmoja pekee, kwa kuwa yeye Rais ndiye mwenye uwezo wa kumtumbua!
Tunajua kuwa zipo nafasi nyeti ambazo zimepewa kinga Kikatiba, ikiwemo hiyo ya CAG na majaji wa Mahakama kuu wa kutoweza kutumbuliwa "kienyeji" na Rais
Tunajua kuwa Rais kabla hajaanza kutumikia nafasi hiyo ya Urais, anaapa kuitii na kuilinda Katiba ya nchi yetu.
Hivi kwa mwenendo anaoendelea nao Rais wetu wa kuisigina Katiba ya nchi yetu waziwazi, ndipo ninapoyakumbuka maneno ya usia na busara sana ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Nyerere, aliposema kuwa tunamchagua Rais wetu na anaapa kuitii na kuilinda Katiba ya nchi yetu, kwa hiyo inapotokea Rais wetu anaamua kuivunja Katiba hiyo, Rais wa aina hiyo HATUFAI
Ni wajibu wa watanzania wote tukemee Tabia hii ya Rais wetu ya kuisigina waziwazi Katiba ya nchi yetu na tusipofanya hivyo hivi sasa, huko mbele kilio kitatuumbua!
Karibuni wadau tujadili kwa staha mada hiyo muhimu sana kwa mustakabali wa Taifa letu
Umenena vyema mkuu Kingsman
Yaani Jiwe "hobby" yake kubwa ni KUTEUA na KUTENGUABen Saanane aliongelea sana PhD ya huyu jamaa. Kama yeye anaweza kupata PhD, nani atashindwa??
Yani mtu pamoja na kutumikia nafasi za kisiasa kwa miaka 30 lakini bado hajui ukubwa wa KATIBA.
AIBU KUBWA SANA HII....USHAMBA ni ugonjwa mbaya sana.
Kwa sababu CAG akionyesha kuna ufisadi basi yeye anaonekana hajadhibiti ufisadi kama wengi wanavyodhania. Yeye angependa CAG aseme hakuna ufisadi kabisa na mashirika yote ya UMMA yanajiendesha kwa faidaKama yeye Rais anatamba kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa serikali yake inapiga vita ufisadi, ni kwanini basi "amchukie" CAG anayeonyesha kwenye ripoti zake mahali kulikofanyika ufisadii wa kutisha nchini??
Kwa sababu anayepiga hela sasa hivi kabaki yeye tu, miradi mingi nchini inafanywa na kampuni zilizopo chini yake kwa jina la ndugu, au nyingine zinazoshirikiana na kampuni zake, kama sio hivyo tenda hupewi. Jamaa atamaliza miaka 10 kawa billionaire kabisa, in USD sio hata TZSKama yeye Rais anatamba kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa serikali yake inapiga vita ufisadi, ni kwanini basi "amchukie" CAG anayeonyesha kwenye ripoti zake mahali kulikofanyika ufisadii wa kutisha nchini??
Kwa hali hii inavyoendelea, ni kweli tutakuwa tunakamuliwa hiyo kodi, kumbe kodi yetu inaingia kwenye mifuko binafsi ya Jiwe!Kwa sababu anayepiga hela sasa hivi kabaki yeye tu, miradi mingi nchini inafanywa na kampuni zilizopo chini yake kwa jina la ndugu, au nyingine zinazoshirikiana na kampuni zake, kama sio hivyo tenda hupewi. Jamaa atamaliza miaka 10 kawa billionaire kabisa, in USD sio hata TZS
Hebu weka hicho kifungu cha sheria kinachosema atatumikia kwa kipindi cha miaka 5, na baada ya miaka hiyo, ATACHAGULIWA CAG MWINGINE!Wewe unayumbisha ukwerli; sheria inasema hivi. CAG atatumikia kwa kipindi cha miaka mitano; baada ya miaka hiyo mitano atachaguliwa CAG mwingine. Huyo CAG mwingine anakuwa ni mtu mwingine tofauti kabisa au anaweza kuwa ni huyo huyo CAG aliyekuwapo, lakini hataruhusiwa kutumikia kwa zaidi ya Miaka 10. Kifungu cha umri kinakuja tu kuwa iwapo atakuwa hajamaliza kipindi chake lakini akafikisha umri huo, basi atatakiwa kuachia.
Tunachouliza Mkuu Pascal, je kumtumbua Profesa Assad, hajavunja Katiba ya nchi, ibara ya 144??Tusimlaumu Rais Magufuli kwa lolote, yote anayoyafanya ni kwa mujibu wa katiba
He has all the powers to hire and fire as he pleases
P.Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi hizi hazihojiwi popote na yeyote!
Wanabodi, Bandiko hili ni kufuatia watu fulani humu wenye viherehere na vimbelembele kutaka kuhoji kila kitu sasa wameingilia kuhoji uwezo wa serikali ya JPM kufanya vetting kabla ya teuzi fulani fulani, kumbe hawajui kuwa now days vetting is nothing!. Kinachoangaliwa sasa ni uwezo wa utendaji...www.jamiiforums.com