Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa FBI nchini Marekani, James Comey, ameandika katika kitabu chake A HIGHER LOYALTY maneno ya kuleta tafakuri kubwa. Amendika _“it is very hard to leave a group of people who are committed only to doing the right thing”_. Alikuwa anaeleza ugumu wanaopata watu waadilifu katika utumishi wa umma kutenda mambo kwa kufata sheria na taratibu. Mara nyingi hujikuta wapo peke yao. Athari ya wanayokutana nayo ni kuzidisha hofu kwa wengine wenye ujasiri na hatimaye kuendelea kuporomoka kwa maadili ya utendaji wa umma.

Katika hili la CAG, imeonyesha wazi kwamba wanasheria katika ngazi mbali mbali hawakutimiza wajibu wao.

Ibara ya 144 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano imeeleza wazi kama ifuatavyo:

*_"144 (1) bila ya kuathiri masharti mengine yaliyomo katika ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Jamhuri ya Muungano atalazimika kuacha kazi yake atakapotimiza umri wa miaka siti au umri mwingine wowote utakaotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge”_*

*_“(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aweza tu kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake(ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya [4] ya ibara hii”_*

Ibara hiyo ya Katiba inaeleza wazi kwamba umri wa kuacha kazi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ni miaka 60. Hata hivyo Bunge limepewa uwezo wa kubadili umri na sio muda wa kazi wa Mdhibiti na Mkaguzi. Ni kanuni ya msingi ya kutafsiri sheria kwamba neno linapokuwa na maana mahsusi, haliwezi kutaftiwa tafsiri nyengine mbadala inayopingana na maana mahsusi ya neno hilo. Ibara ya
144 (1) ilikusudia kuweka umri wa kustaafu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kama ulivyowekwa umri wa kustaafu wa Majaji chini ya ibara ya 110 ya Katiba ambao nao ni miaka 60.

Ibara ya 144 haitoi mwanya kwa Bunge kutunga Sheria ya kuweka muda wa kuendelea na kazi kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ambao utamfanya aondolewe kazini kabla ya muda uliowekwa na Katiba au kuongezwa na Sheria [miaka 65].
Hili linathibitishwa zaidi na ibara ya 144 (6) ya Katiba inayosema:

*_“ Mtu ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu au aliyepata kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hawezi kuteuliwa kushika au kushikilia madaraka ya kazi nyingine yoyote katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano”_*

Kwa ibara hiyo, Profesa Musa Assad hawezi hata kukaimu nafasi yoyote katika utumishi wa umma, na hivyo atakuwa amestaafishwa katika utumishi wa umma kabla ya umri wa kustaafu. Hakuna kiumbe cha namna hiyo katika utumishi wa umma. Ikitokea hivyo, tafsiri sahihi ni kuwa mtu huyo amefukuzwa au kukatishwa utumishi wake. Na hilo, ni batili ya wazi kwa vile inakiuka masharti ya ibara ya 144(2) na (3) ya Katiba.

Sheria au tafsiri inayotoa mwanya kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kuondolewa kabla ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria na kwa matakwa ya Rais bila ya kufuata masharti ya wazi ya utaratibu wa kumuondoa kabla ya kufikiksha umri wa kustaafu chini ya ibara ya 144(3) na (4), inavunja msingi wa kinga ya kikatiba [security of tenure].

Inasikitisha sana unapoona wanasheria katika mazingira kama haya, ambapo kuna mgongano baina ya Katiba na Sheria, wanaanza kutafsiri Sheria kuipindua Katiba na sio kutafisiri Katiba ili kuipindua Sheria inayopingana na Katiba kama inavyoelekezwa na ibara ya 64(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Mwanasheria yeyote aliyemshauri Rais kumuondoa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kutumia Sheria inayoweka masharti ya vipindi bila kuzingatia masharti ya wazi ya ibara ya 144(1) ya Katiba amemkosea sana Rais, amewakosea sana Watanzania na ameifedhehesha sana taaluma ya Sheria.

Fedheha kubwa zaidi kwa taaluma ya sheria ni pale wanasheria watapoanza kutofautiana katika kutafsiri masharti hayo ya wazi ya Katiba kwa itikadi au mirengo ya kisiasa au kwa baadhi kufanya hivyo kwa kupotosha ili kumfurahisha mteuzi.

Athari ya jambo hili haitokuwa kwa Profesa Mussa Assad. Athari kubwa ni katika mfumo wetu wa kikatiba, utawala wa sheria na matumizi ya mamlaka ya umma.
 
Wanasheria wa Tanzania wamenyamaza kimya. Hawatoi ufafanuzi kumtetea bosi wao aliyejitetea mwenyewe siku ya kuapishwa. Jamani wanasheria mlioajiriwa na serikali, msaidieni Rais kutoa ufafanuzi wa kisheria mliompa ili a-terminate mkataba wa CAG. Sasa kimya ndio nini?
 
Nmeshangazwa na haya mapambio dhidi ya CAG Prof Assad. Wengi wa wasiomfahamu wanamuona kwa yeye kuendesha IST ni mtu aliyejishusha sana na ni mwenzao.

Prof Assad anachofanya ni kucheza na akili za Watanzania. Mimi namfahamu akiwa anamiliki Benz pale UDSM na sijajua kama kwa sasa hana gari nyingine au ni maamuzi tu kutumia IST.

Kuna picha moja ashawahi kupiga Mo Dewji akiwa amepanda boda boda. Hii iliwapa sana faraja Watanzania. Lakini wanasahau Mo alipanda bodaboda wakati kuna Range Rove inamsubiri sehemu. Wewe unapanda bodaboda sababu ndiyo usafiri unaomudu.

Siku Mo Dewji akitembea kwa miguu toka anapoishi mpaka ofisini si sawa na wewe kutembea kwa miguu toka unapoishi mpaka ofisini. Yeye atakuwa anafanya mazoezi. Wewe utatembea sababu huna nauli.

Push-ups ukiamua upige mwenyewe hata 100 ni mazoezi. Push-ups hizo hizo ukiambiwa na mtu kwa kulazimishwa upige 50 ni adhabu.

Prof Assad kutumia IST si kwa sababu yeye ni maskini. Ni maamuzi tu but anaweza kuwa na gari za thamani zaidi. Anafahamu akili za Watanzania. Angeweza kwenda hata na bodaboda na wakashangilia sana kuwa huyu ni mwenzetu kabisa amejishusha.

Katika kujishusha pia kuna maana yake. Ni rahisi kwa mtu ambaye yupo juu kushuka chini na asifikiri ni shida, but kwa mtu aliye chini, siku zote hutamani kuwa juu. Je, aliye juu anaweza kujishusha chini na kuendelea kukaa chini?

Katika maisha kuna maigizo mengi. Tujiulize: Je, tunasoma na watoto wa Pro-Assad Nyanyembe Secondary Schools? Au Kitangoma Primary School? Je walisoma nasi Nyegehizi High School?

Je, huyu aliyejishusha anaishi nasi Buguruni kwa Mnyamani, au anaishi nasi Kigogo Mburahati? Tutofautishe maisha halisi na maigizo ndugu Watanzania.
Wewe ndio MVIVU wa kufikiri, hakukuwa na haja ya kuja kuanzisha UZI wakati kuhusu masuala ya Benzi na mambo mengine yameshaandikwa kwenye UZI wa GUSSIE.

Umekuja na hoja ya IST, wakati kwenye UZI ambao umetumia kama reference hayo yote yameandikwa.
 
Nyie mnapenda kulazimisha mawazo yenu ndio iwe sheria. Mbona vitu vipo wazi tu kuwa CAG anaweza kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake(ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote). Mbona hicho kipengele cha sababu nyingine yoyote hamkisemi? Na bahati mbaya au nzuri sheria haimlazimishi Rais kuitaja hiyo sababu wala kuunda tume. Bali inampa uhuru wa kuamua kama aunde tume au hapana.

(3) Iwapo Rais anaona kwamba suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti ya ibara hii lahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mambo yatakuwa ifuatavyo:
(a) Rais atateua Tume Maalum ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili. Huyo Mwenyekiti na angalau nusu ya wajumbe wengine wa Tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni Majaji au watu waliopata kuwa Majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchi yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola;
 
Nmeshangazwa na haya mapambio dhidi ya CAG Prof Assad. Wengi wa wasiomfahamu wanamuona kwa yeye kuendesha IST ni mtu aliyejishusha sana na ni mwenzao.

Prof Assad anachofanya ni kucheza na akili za Watanzania. Mimi namfahamu akiwa anamiliki Benz pale UDSM na sijajua kama kwa sasa hana gari nyingine au ni maamuzi tu kutumia IST.

Kuna picha moja ashawahi kupiga Mo Dewji akiwa amepanda boda boda. Hii iliwapa sana faraja Watanzania. Lakini wanasahau Mo alipanda bodaboda wakati kuna Range Rove inamsubiri sehemu. Wewe unapanda bodaboda sababu ndiyo usafiri unaomudu.

Siku Mo Dewji akitembea kwa miguu toka anapoishi mpaka ofisini si sawa na wewe kutembea kwa miguu toka unapoishi mpaka ofisini. Yeye atakuwa anafanya mazoezi. Wewe utatembea sababu huna nauli.

Push-ups ukiamua upige mwenyewe hata 100 ni mazoezi. Push-ups hizo hizo ukiambiwa na mtu kwa kulazimishwa upige 50 ni adhabu.

Prof Assad kutumia IST si kwa sababu yeye ni maskini. Ni maamuzi tu but anaweza kuwa na gari za thamani zaidi. Anafahamu akili za Watanzania. Angeweza kwenda hata na bodaboda na wakashangilia sana kuwa huyu ni mwenzetu kabisa amejishusha.

Katika kujishusha pia kuna maana yake. Ni rahisi kwa mtu ambaye yupo juu kushuka chini na asifikiri ni shida, but kwa mtu aliye chini, siku zote hutamani kuwa juu. Je, aliye juu anaweza kujishusha chini na kuendelea kukaa chini?

Katika maisha kuna maigizo mengi. Tujiulize: Je, tunasoma na watoto wa Pro-Assad Nyanyembe Secondary Schools? Au Kitangoma Primary School? Je walisoma nasi Nyegehizi High School?

Je, huyu aliyejishusha anaishi nasi Buguruni kwa Mnyamani, au anaishi nasi Kigogo Mburahati? Tutofautishe maisha halisi na maigizo ndugu Watanzania.
Anaishi atakavyo yeye,haishi ili aonekane na watu.

Kwa hiyo hoja yako ni mufilisi
 
Hili la GAG ni ushahidi kuwa uongozi wa Tanzania una mambo ya ovyo ovyo kabisa, wendawazimu mtupu.
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa
 
Kosa lako ni kila jambo kuandika upinzani...nyumbulisha usigundulike mapema...
 
Nmeshangazwa na haya mapambio dhidi ya CAG Prof Assad. Wengi wa wasiomfahamu wanamuona kwa yeye kuendesha IST ni mtu aliyejishusha sana na ni mwenzao.

Prof Assad anachofanya ni kucheza na akili za Watanzania. Mimi namfahamu akiwa anamiliki Benz pale UDSM na sijajua kama kwa sasa hana gari nyingine au ni maamuzi tu kutumia IST.

Kuna picha moja ashawahi kupiga Mo Dewji akiwa amepanda boda boda. Hii iliwapa sana faraja Watanzania. Lakini wanasahau Mo alipanda bodaboda wakati kuna Range Rove inamsubiri sehemu. Wewe unapanda bodaboda sababu ndiyo usafiri unaomudu.

Siku Mo Dewji akitembea kwa miguu toka anapoishi mpaka ofisini si sawa na wewe kutembea kwa miguu toka unapoishi mpaka ofisini. Yeye atakuwa anafanya mazoezi. Wewe utatembea sababu huna nauli.

Push-ups ukiamua upige mwenyewe hata 100 ni mazoezi. Push-ups hizo hizo ukiambiwa na mtu kwa kulazimishwa upige 50 ni adhabu.

Prof Assad kutumia IST si kwa sababu yeye ni maskini. Ni maamuzi tu but anaweza kuwa na gari za thamani zaidi. Anafahamu akili za Watanzania. Angeweza kwenda hata na bodaboda na wakashangilia sana kuwa huyu ni mwenzetu kabisa amejishusha.

Katika kujishusha pia kuna maana yake. Ni rahisi kwa mtu ambaye yupo juu kushuka chini na asifikiri ni shida, but kwa mtu aliye chini, siku zote hutamani kuwa juu. Je, aliye juu anaweza kujishusha chini na kuendelea kukaa chini?

Katika maisha kuna maigizo mengi. Tujiulize: Je, tunasoma na watoto wa Pro-Assad Nyanyembe Secondary Schools? Au Kitangoma Primary School? Je walisoma nasi Nyegehizi High School?

Je, huyu aliyejishusha anaishi nasi Buguruni kwa Mnyamani, au anaishi nasi Kigogo Mburahati? Tutofautishe maisha halisi na maigizo ndugu Watanzania.
Hata hivyo, mtu yeyote aliyesoma uzi huu atakubaliana na mimi kuwa wewe pia una shida kubwa sana kichwani, kuliko hata hao unaowaponda,..., and the worst case scenerio ni kwamba una shida kichwani na ambayo hujui kuwa unayo. Kazi kwako
 
Kwani alipaswa kuendesha gari gani?

Kama vipi afunguliwe kosa la utakatishaji fedha na uhujumu uchumi kwa kuanza kuendesha IST yake bila ya kufunga Mkanda kama tulivyoona wakati anaondoka National Audit Office maana makosa mengine tumepekua tangu akiwa Udsm tumekosa
 
Wanasheria wa Tanzania wamenyamaza kimya. Hawatoi ufafanuzi kumtetea bosi wao aliyejitetea mwenyewe siku ya kuapishwa. Jamani wanasheria mlioajiriwa na serikali, msaidieni Rais kutoa ufafanuzi wa kisheria mliompa ili a-terminate mkataba wa CAG. Sasa kimya ndio nini?
Wataishia kuambiwa nakulipa mshahara mimi,posho,mafuta ya gari na bado unanishauri vifungu vyako hovyo hovyo vya sheria hiiiiiiiiiiiiiii
 
Katiba ndio sheria mama

Kwa kifupi wamebugi[emoji57]

Tunawacheka hi hi hi hi hi![emoji3]( kwa sauti ya mwenye Sirikali)
 
Nachukua tu twakwimu. Na wewe pia ni mmojawapo.

Back
Top Bottom