Suala la mzee Mwinyi kuzikiwa Zanzibar wala lisifanywe la kisiasa, pitieni hapa msome muelewe sababu

Mfano uliotoa hauufanani kabisa na suala la Mzee Mwinyi.
Kwa nini haufanani?

Kwanza kabisa, sijajibu suala la Mzee Mwinyi, nimejibu suala la mwanamme hazikwi alikooa.

Pili,

Kwa muktadha wa kukataa mwanamme kuzikwa sehemu aliyooa, wewe ni nani uamue mtu mwingine azikwe wapi? Unajipa vipi mamlaka ya kumuamlia mtu mwingine sehemu ya kuzikwa?
 
Kuhusudu mila na desturi sio ujinga, na wala sio kweli wanaofuata mila na desturi huishia kufulia, naona wewe ndie unaishi kwa kukariri.

Kuhusu Mzee Mwinyi kujadliwa ni kujadiliwa tu, iwe kwa story zenye ushahidi au zisizo na ushahidi, hiyo yote ndio mijadala yenyewe, usitufunge midomo.

Kama hupendi story za uzushi kwanini wewe huitaka serikali ikwambie wapi walipolazwa viongozi wetu, ikiwa wewe hujui lini waliondoka nchini na ugonjwa upi unaowasumbua?

Kwanini usiitake serikali kwanza ikupe ushahidi wa ugonjwa wao, ili uanze kutaka kujua wapi walipoenda kulazwa viongozi wetu?

Hujioni nawe kutaka kujua wapi walipolazwa viongozi wetu, bila kujua kwanza ugonjwa wao nawe ni miongoni mwetu wanaopenda uzushi wa vijiweni?

Kaa chini tafakari.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mila na desturi hazisimami, zinaendelea kila siku. Na unajuaje kama Mwinyi, kiongozi aliyeweka rekodi ya kuzaliwa bara na kuwa rais visiwani, katuanzishia mila na desturi mpya ya kuzaliwa bara na kuzikwa Zanzibar ili kuudumisha zaidi Muungano?

Kuna tofauti kati ya kujadiliwa na uzushi, hizo habari za wosia wa Mwinyi ni uzushi tu, hakuna mtu mwenye ushahidi wa wosia huo.

Unaniuliza "kama hupendi story za uzushi kwa nini..." ina maana wewe unapenda stories za uzushi na unatetea kupenda kwako stories za uzushi?
 
Huwezi kulitenga suala hili na siasa hasa siasa za Zanzibar
Kuzikwa popote siyo tatizo, hata Raza aliyeuchukia Muungano alizikwa Kisutu.

Unguja wangependa azikwe huko kwasababu ni mwana Mapinduzi na itaondoa hoja za Wapemba
Mwinyi alikubalika Zanzibar kwasababu ilikuwa timu ya Kombo Thabiti , watu wa Mapinduzi

Kwasiasa za ubaguzi, wapo wanaoamini Mwinyi na waliotoka Bara kama VP Seif Idd si Wazanzibar.

Rais Hussein Mwinyi anakutana na wakati mgumu sana akisemwa si ''Mzanzibar halisi'' , anapigwa vita hata ''Shangazi' amewahi kulisema.

Kwa kutambua hilo kwa maoni yangu Familia iliamua azikwe Zanzibar ili kujenga msingi wa vizazi vijavyo kwamba ni Wazanzibar! Siasa ipo ndani ya hili

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Suala la kuzaliwa hapa na kuzikwa pale sio la kimuungano, wala sio la kisiasa, hata Magufuli aliwahi kupinga kuzikwa Dodoma akifariki, ni suala la mila na desturi zetu unazoziita ni ujinga hutaki kuzifuata.

So, kwangu naona kuleta habari ya kuzaliwa hapa na kwenda kuzikwa kule ili kukuza muungano ndio ujinga wenyewe, kwani huko Zanzibar hakuna waliozaliwa na kuishi huko? kama wapo kwanini wakifariki wasizikwe kwao walipozaliwa?!

Unaonekana hujui hata tetesi wewe unaita uzushi ni chanzo kimojawapo cha habari, hapo ndipo huwasukuma waandishi wanaojielewa kuanza kuchimba kuutafuta ukweli, kuzikataa tetesi/uzushi kama unavyoita, ni kujinyima haki yako ya kupata habari.

Ndio mimi stories za uzushi nazipenda kwasababu zina expand my brain muscles, zinaifanya akili yangu itanuke, napata wasaa wa ku- connect dots, sipendi kuwa na lazy mind ya kusubiri ushahidi wa kila jambo kama vile niko mahakamani.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mwinyi kajenga msikiti kisalawe na alikuwa akiwa dar ijumaa anasali kisarawe.aidha usia wake aliandika azikwe kisarawe na hadi barabara zilichongwa wakawaza madhara ya hilo
 
Babu Duni wa ACT moja ya mikutano yake alimwiita mzee Mwinyi "MZARAMO" na si Mzanzibari, alitakiwa kuzikwa makaburi ya Kinondoni!!!!
 
1. Huna ushahidi wowote kuhusu wosia wa Mwinyi. Habari zozote kuhusu wosia huu ni uzushi tu.
2. Suala la mazishi ya Mwinyi ni maamuzi ya familia, wewe ni mtu wa familia?
3. Uki support stories za uzushi zisizo na ushahidi, ume support chaos, mimi naweza kuanzisha uzushi kwamba wewe ni mpinzani wa kisiasa wa familia ya Mwinyi unaleta uzushi ili ukufaidishe kisiasa tu. Tukaanza kubishana uzushi juu ya uzushi mpaka maongezi yakwa hayana maana.
 

Ngoswe kaokotwa wapi?
 
Nimeshakuonesha umuhimu wa unachokiita uzushi kwenye jamii, yapo mambo mengi huanza kama uzushi lakini baadae huthibitika kuwa uzushi ule ulikuwa ni kweli, amsha akili.

Hata kama suala la mazishi ya Mzee Mwinyi ni maamuzi ya kifamilia, lakini Mzee Mwinyi kuwahi kuwa kiongozi wa kitaifa kunatufanya na wengine tujadili sababu za maziko yake kuwa Zanzibar, kama hakupenda kujadiliwa angeacha kuwa kiongozi wa kitaifa hakuna ambaye angehaika nae leo.

Mimi nina support stories unazoita za uzushi ili kuwasukuma waandishi wetu wa habari wakachimbe kuutafuta ukweli, suala la "chaos za kisiasa" ni maoni yako binafsi, siwezi kuyapinga.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Huo uzushi wako hauna hata muelekeo wa kuwa kweli. Kwa sababu hakuna logical inconsistency yoyote Mwinyi kuamua kuzikwa Zanzibar.

Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, sehemu ambayo Mwinyi kasoma, kaishi, kalowea, mpaka kawa rais, mbona unafanya kama vile Mwinyi kaenda kuzikwa Misri?
 
".... Hauna hata muelekeo wa kuwa kweli" naona unajigeuza mtabiri sasa, kwani hii nayo ni fani yako? kama sio basi tuache muda uamue.

Mzee Mwinyi hata kama angezikwa Misri nisingeshangaa chochote kama asingekuwa "political figure", na ndio maana hata wewe umesema kule juu ukifa utazikwa Marekani, sikushangaa chochote.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
"....Hauna hata muelekeo wa kuwa kweli" naona unajigeuza mtabiri sasa, kwani hii nato ni fani yako?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Hiyo kauli sikuiandika kwa urahisi, nilivyoiandika, nikajirudi na kutaka kuipatia justification.Nimekupa sababu ya kuandika hivyo.

Hujaiweka sababu hiyo hapa tuichambue.

Ama kwa sababu uelewa wako ni mdogo sana hukuweza kuielewa, ama kwa sababu umeielewa huna nia ya kuichambua kwa sababu itakupa mzigo wa kuthibitisha mambo ambayo huwezi kuthibitisha.

Sasa, wewe uko kundi gani?

Mjinga sana hujaelewa au muongmuongo tu umeelewa lakini unataka kukwepa mazungumzo ya mantiki?
 
Kwani wewe hiyo statement "hauna muelekeo wa kuwa kweli" umeiona kwa kutumia kipimo gani? kilichothibitishwa wapi?

Kama ni fikra zako, basi tuliza hicho kichwa, fikra zako sio kipimo cha kuthibitisha mambo hapa ulimwenguni, wewe ni mwanadamu tu, kama nilivyo mimi, na wengine ...

Hatuko complete kila wakati kifikra, mara nyingine hukosea pia, hata kama mwanzo hujiona tuko sahihi.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…