Suala la mzee Mwinyi kuzikiwa Zanzibar wala lisifanywe la kisiasa, pitieni hapa msome muelewe sababu

Nimekupa kipimo cha logical consistency, hizo si fikra zangu tu.

Ila, naona logical consistency si kitu muhimu kwako, kwanza unahusudu uzushi.

Pili, unajipa umuhimu kwenye mazishi ya Mwinyi kuliko familia ya Mwinyi.

Familia iliomba faragha yao ya kifamilia iheshimiwe tangu Mzee wao alivyoumwa, wewe huna ustaarabu wa kuheshimu matakwa ya familia.

Unajipa umuhimu kwenye mazishi ya Mwinyi kuliko familia ya Mwinyi.

Ni upumbavu usio kifani.
 
Sisi wabongo ni watu wa ajabu sana.
Hivi kati yetu na familia ni nani hasa anaweza kuujua wosia wa Mzee.
 

Afadhali kama anazikwa Zanzibar kwa sababu nyingine, na siyo hizo za masuala ya madaraka.

Mwanadamu kuna wakati inabidi uyaone madaraka si chochote ukilinganisha na nafsi yako au ya mtu unayemthamini.

Marehemu hupewa uzito mkubwa sana kwa sababu moja kubwa kuwa akishalala hawezi kubishana na yeyote wala kuwa na nguvu ya kushindana. Hivyo kutenda kinyume na matakwa yake huonekana kama dhuluma kubwa sana dhidi ya haki ya marehemu.

Kwa mapenzi ya Mungu na hekima yake, tunamwomba Mungu aipe pumziko jema la mzee Ali Hassan Mwinyi.
 

Hayati Mh.Mwinyi kuzikwa Zanzibar ni kuepusha shari na maswali kuhusu Dr.Mwinyi ambae kwasasa ndiye amekalia kiti huku kwetu Zanzibar... maana sio mwanakwetu kwa uhalali bali nikwa hisia tu.
 
[emoji23][emoji23]
Yani mtu anajiona ana haki kabisa ya kuipangia familia ya Mwinyi baba yao azikwe wapi.

Kabisaaa, kabisaaa, anajiona ana fikra timamu kabisa kuipangia familia ya watu imzike wapi baba yao!
 
Hayati Mh.Mwinyi kuzikwa Zanzibar ni kuepusha shari na maswali kuhusu Dr.Mwinyi ambae kwasasa ndiye amekalia kiti huku kwetu Zanzibar... maana sio mwanakwetu kwa uhalali bali nikwa hisia tu.
Kwa hivyo, unataka kutuambia kuwa kuna sheria za physics zisizopindika ambazo zinasema kwamba Ali Hassan Mwinyi kwa mapenzi yake binafsi hakuweza kutaka kuzikwa Zanzibar kwa sababu nyingine yoyote ile?
 
Kwa hivyo, unataka kutuambia kuwa kuna sheria za physics zisizopindika ambazo zinasema kwamba Ali Hassan Mwinyi kwa mapenzi yake binafsi hakuweza kutaka kuzikwa Zanzibar kwa sababu nyingine yoyote ile?
Naona umenielewa ila ukaweka tena maneno yako mengine....Tutauliza kuhusu huyu kishobeka..
 
Naokuona unarudi kule kule tulipotoka...

Unasema mimi najipa umuhimu kwenye mazishi ya Mzee Mwinyi, vipi wewe huwa hujipi umuhimu kutaka kujua wapi viongozi wetu wa kitaifa huenda kutibiwa ikiwa hujui ugonjwa unaowasibu?

Kule huwa unajitetea kwamba unataka kujua wapi walipolazwa sababu wao ni public figure, vipi kwa Mzee Mwinyi, kwanini yeye hakuwa public figure?

Au kwao hao viongozi wa kisiasa unaopenda kuwazungumzia bila ushahidi ni wale wagonjwa wanaoenda kulazwa usipopajua, lakini wakishafariki huoni tena sababu ya kutaka kujua mambo yao?

Nimekuuliza kuke juu hukunijibu, kwanini kabla hujajua wapi walikoenda kulazwa viongozi wa kitaifa, usiulize kwanza serikali ugonjwa unaowasibu ili upate validity ya kujua wapi walipolazwa?

Hujioni nawe huwa unajipa umuhimu bila sababu kwa mambo ya familia za watu? Punguza ego, tafuta glass ya maji unywe, naona umeshachemka.

Nakuona kama umeshapata moto tu, tulia kunywa glass ya maji, usi

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Bado upo nao? Waache waamini wanachoamini,yeyote anaruhusiwa kuamini anachotaka kuamini,ila unaposema unajua tutakutaka utujulishe unachojua,wanaosema diaspora hawana pesa za kusafirisha maiti ndiyo ambao daily wanatafuta connection za kuchomoka,ili nao wapate hiyo hadhi ya kuwa dispora,wasaidie familia zao in 1and2, ishi man.
 
Waafrika wengi tunasumbuliwa na kuishi kwa kukariri mambo.

Ndiyo maana hata kuendelea inakuwa tabu, kwa sababu, kuendelea kunataka mtu anayeweza kubadilika na wakati, hakutaki mtu anayeishi kwa kukariri.

Waafrika wengi wamekariri mtu akifa arudishwe kwao alizozaliwa akazikwe na wazazi wake.

Hizi ni fikra za kizamani. Wazungu wale walioenea na kutawala dunia nzima kwenda kuwa na makoloni Africa, kwenda kuishi Australia, kwenda kuishi Marekani, wangekuwa na fikra hizi za kutaka kila mtu azikwe kwenye makaburi ya wazazi wake, wasingetawala dunia.

Mwinyi kuzikwa Zanzibar ni desturi mpya, desturi ya kupanua makazi, kusema kwamba si lazima mimi kuzikwa kwenye makaburi aliyozikwa baba yangu, nawez akuvuka bahari nikaanzisha makao sehemu mpya, nikawa kiongozi huko, nikazikwa huko.

Waafrika wengi ukiwaletea habari za kubadilisha desturi ili kwenda na wakati wanapata ukakasi sana, wamezoea maisha ya kukariri.

Ndiyo maana Mwinyi kuzikwa Zanzibar wanamuanzishia all types of conspiracy theories.

Ame challenge desturi zao vibaya sana.
 
Toa mfano specific tuujadili kwa muktadha, tena utoe mfano kwa kutumia maandishi yangu, si kwa maneno unayofikiri wewe tu.

Ukweli ni kwamba, sijawahi kutaka kuipangia familia ya mtu baki wapi pa kumzika baba yao.

Wewe unataka kuipangia familia ya Mwinyi wapi pa kumzika baba yao.
 
Kwanini walimshadadia akazikwe kule kama yeye alitamani kuzikwa bara? Nini mzizi wa yote?
 
Wabongo wengi huwa wanatoa maneno kama wanatoa kwa logic, ila wengine ni kwa wivu na chuki.

Wewe mtu gani anataka kulazimisha familia ya watu, tena familia ambayo ilishaomba kuachiwa faragha tangu baba yao anaumwa, kwa kuwajua wabongo wanavyopenda uzushi na umbea, unawezaje kuilazimisha familia hiyo imzike wapi baba yao?

Unataka kuwapangia wamzike wapi baba yao kwani unataka kumfukua ukamle nyama?
 
Kwanini walimshadadia akazikwe kule kama yeye alitamani kuzikwa bara? Nini mzizi wa yote?
Kwani wapi Mwinyi alisema alitamani azikwe bara?

Nje ya maneno ya kuungaunga ya watu baki ambayo hayana hata ushahidi, wapi Mwinyi mwenyewe kasema alitamani azikwe bara?
 
Amesika muombolezaji mmoja.. Laiti Uncle Magufuli angekuwa hai..
Mzee angezikwa Mkulanga tuu.. Kama ilivyo kuwa Mzee Mkapa..
 
MBONA UBUNGE ALIGOMBEA MKURANGA KWANI HAKUGOMBEA ALIKOKULIA na KUOA?
 
...Ila umewahi kuipangia familia ya viongozi wa kitaifa na serikali kujua wapi walipolazwa viongozi wa nchi.

Huu ndio msimamo wako naufahamu, nina kumbukumbu nao, sio mjinga kuandika nisichokijua kukuhusu, kazi ya kutafuta thread huku ifanye mwenyewe majibu yako utayapata.

Kuujua msimamo wa mtu kwenye jambo fulani sio ajabu, usitake kuletewa ushahidi hapa ili kupotezeana muda, prove me wrong if you can.

Tena uje na ushahidi wako toka kwenye ule uzi wa ugonjwa wa Makamu wa Rais alipoenda kutibiwa hivi karibuni, nimeshakupa na point of reference kazi kwako.

Unasumbuliwa na egoism, matokeo yake umegeuka kama popo, jambo moja unataka upewe ushahidi wa kifamilia ili kulijadili, jambo lingine unakimbilia kutaka kujua kulikoni bila ushahidi wa ugonjwa!

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Amesika muombolezaji mmoja.. Laiti Uncle Magufuli angekuwa hai..
Mzee angezikwa Mkulanga tuu.. Kama ilivyo kuwa Mzee Mkapa..
Watanzania wengi ni watu wasiojua ku question the premise.

Yani ni watu fulani hivi, ukishawaambia "Chagua bluu au nyekundu", wengi hawawezi kuuliza "kwa nini nichague bluu au nyekundu tu, hakuna nyingine?". Au hawawezi kuuliza "kwa nini wewe ndiye unaniambia mimi nichague, na mimi nisikupange wewe uchague?".

Mawazo haya ni ya unyonge mkubwa wa kifikra. Umasikini wa fikra hata kabla hujafika kwenye mali zinazoonekana.

Watu wenye mawazo haya, ni rahisi sana kuwapandikizia hadithi za uongo zionekane kama kweli.

Unachotakiwa kufanya ni kutunga uongo tu. Sema tu "Mwinyi alitaka kuzikwa bara, ila familia yake imelazimisha azikwe Zanzibar kwa sababu za kisiasa".

Hawakuulizi kasema lini, wapi, ushahidi uko wapi, tutajuaje kweli alisema hivyo, na wewe si muongo unayetaka kutumia msiba huu kwa faida zako za kisiasa.

Watu wanapenda umbea na conspiracy theory wanaunganisha tu stories bila hata kuhakiki.

Ndiyo mazungumzo mengi kwenye hoja hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…