Suala la Salim Kikeke kuhamia EFM na akili za watanzania

Huyo Kikeke kama kweli kaenda EFM itabidi apimwe akili. Mtu unaondokaje BBC na kujinga EFM kama kweli akili zako zimetimia? Hii mi sawa na kutoka chuo kikuu ukahamia chekechea. Ni aibu kubwa sana kwake.
 
Kwa hatua aliyopiga ilibidi aanzishe Televisheni yake atoe platform kwa vijana wadogo waandishi
Hatua ipi ?kwa mfano Kwako unaweza kuona jero ni ela ya kupiga hatua ya kuanzisha biashara mwenzako jero ni ela ya ndogo anahitaji buku mbili maisha ni kuhusu mtazamo nyie mnachowaza mwenzenu haja kiona
 
Huyo Kikeke kama kweli kaenda EFM itabidi apimwe akili. Mtu unaondokaje BBC na kujinga EFM kama kweli akili zako zimetimia? Hii mi sawa na kutoka chuo kikuu ukahamia chekechea. Ni aibu kubwa sana kwake

Unajua situation yake hadi kufikia maamuzi hayo? Au una conclude wewe tu unavyowaza
 
Wewe unaongea kama nani? Kwa nini umpangie maisha mtu ambaye hata hakufahamu? Ni nani aliwahi kutoka BBC akaanzisha hata blog tu?
Hatujui mshahara wa Kikeke alipokuwa BBC, lakini naamini haukuwa mkubwa.

Kwa wale waliowahi kukaa London wanajua gharama za bidhaa na huduma zilivyo juu.

Si ajabu asilimia 80 ya pesa yote ya mshahara kutumika kila mwezi kwa mahitaji ya lazima. Hapo bado una ndugu na wazazi huku bongo wakikutegemea.

Kama EFM wamempa pesa anayoihitaji, sioni shida kwa yeye kukubali kupiga kazi.

Isitoshe: mtembea bure siyo sawa na mkaa bure.
 
Unayajua maisha yake binafsi? Unauhakika na investment zake mpaka useme ameshuka? you can't conclude without enough evidence je kama hiyo kazi ya EFM haimbani kwenye mishe zake binafsi anazofanya ? Achague kazi halali ili awaimpress watu dizain yako. Watu kama wewe ni type ya bongo movie or bongo fleva mnaishi fake life kwa ajili ya kuwaimpress watu
 
Samahani kiongozi kahama kutokea RADIO gani kwenda E-FM?. Mm najua alistaff BBC.
Asante
Hakustaff bhanaa..! Wanadai BBC swahili iko chini ya Kenya now so ishu ya ajira na mkataba imekuwa kipengele kwa wabongo sema Kwa charlea hilari alistaff na yule mwana mama wakalamba shavu Serikalini.. Kikeke nae ni suala la muda tuu yani kama Godin Ligondwe alilamba shavuuu huyu nae atalamba shavu
 
Ukiangalia kwa upande mwingine, watz wanamuona ana talanta zaidi! Anastahili kuwa na cheo ki kubwa kama msemaji wa ikulu! CEO wa TBC!, au, Al Jazeera, sio kwenda kuajiliwa kwenye kampuni ndogo kama EFM,harafu ulipwe mshahara kama wa Kitenge au Zembwela!
Yaani Salim wa BBC aende EFM harafu awe anajibishana na watu vilaza kama Zembwela, Kitenge?!!
Tunaona anastahili ki kubwa!
Juzi,kwenye mkutano wa chakula kule Dar, MC wa, shughuri alikuwa mtangazaji wa CNN raia wa Kenya, Larry madowo! Kenge kama Zembwela, au Hando na kitenge, hata kama waliona lile tangazo, walipita pembeni! Maana shule Yao ndogo! Pale sio pa porojo za yanga na Simba!
 
Huyu jamaa na sikia kwamba alivyo rudi akajikita kwenye issues binafsi za uMC (huku kuna hela mno).

Mimi naona angekomaa na uMC unalipa ,kwa mtu kama Kikeke ana exposure, lugha ya Kingereza anaijua,sauti nzuri anayo sizani angekosa shughuli hata tano kwa mwezi,kwani nimemuona kwenye event nyingi za kiserikali kama MC,tena kama akicharge 3M mara tano hakosi 15M.

Ila sijui yy mwenye kaona nini ila Kikeke sio wa kufanya kazi kwenye hizi media za Wasafi, EFM,Clouds nk naona kama ataenda kutangaza kwa style ya kikatuni katuni.
,kama wafanyavyo watangazaji wa hivi vituo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…