Subaru mnatufilisi, Gari zinakunywa mafuta kama zinameza!

Ulitaka iwe inakunywa mchemsho? Sio sahizi yako hy gari
 
Nineweka full tank lita 65 ajabu nimetembea km 350 mafuta kwishney leo nimejaza tena

Watu tunatumia jeep 3700cc yani 3.7L Petrol na hatuwazi wewe na hio 2.0L yako unalia lia tu
 
Abadili gari achukue BMW ulaji wake wa mafuta ni nzuri sana hasa ukipata diesel version

Kati ya Subaru Forester na BMW X3 ipi ni nzuri kwenye performance, speed na durability?
 
Nimewahi kuwa na magari ka 5 hivi. Lakini sasa ukininyang'anya FORESTER yangu hii tutakosana. Mnaosema inakunywa mafuta, ni PM ka utafikia bei niinunue niweke ndani.
SUBARU is the best of all. Sina kipato kikubwa lakini nafurahiiii nikikalia usukani wake. Ka si vijitochi vyao, hii ndo gari ya masafa. Ni ndege ya chini. Miye nalilia fine zao tuu. Nadhani ningeshanunua nyingine
 
Nani kasema gari zenye tubro inakula sana mafuta?hv unajua kazi ya turbo kwenye gari?
 
Hiyo gari ulinunuliwa na sugar mami nini? Kama ulinunua kwa akili yako timamu basi na wewe ikomalie tu kwa kuinyima mafuta.

Daaa nimecheka sana...... watu wanamaneno humu
 
Nani kasema gari zenye tubro inakula sana mafuta?hv unajua kazi ya turbo kwenye gari?

unajua wengine tunabisha bila kujua. Turbo inaongeza ufanisi wa engine kwa hiyo si rahisi kuongeza comsuption ya mafuta.
 
Mkuu hebu funguka zaidi ni oil gani nzuri kwa subaru legacy twin turbo? pia labda tujuze madhara ya kuweka filter ya kichina.
 
Huyu jamaa si mkweli forester zote zina 60L labda hio 5 pamoja na reserve ila forester I na forester II average fuel consumption ni kuanzia 7.3-8.1 km kwa 1L ambayo ukiizidisha na either 60L au 65L full tank hapo unapata zaidi ya 430km na kuendelea sasa unless awe anaendesha kwenye msongamano mkubwa sana ndo inawezekana kutembea km 350 tu na ku refill na scenario ingine ni hilo gari ni bovu...
 
Au pia yawezekana Gari bovu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…