Subaru mnatufilisi, Gari zinakunywa mafuta kama zinameza!

Subaru mnatufilisi, Gari zinakunywa mafuta kama zinameza!

Wapi naweza pata mtu wa kuifanyia diagnosis hii gari kwa computer maana ulaji huu ni sawa na 1ltr kwa 5km ni sawa kweli?msaada pse

Mkuu uko wapi? Maana ulaji huo sio wa kawaida nimetumia hizo gari hazili hivyo !
 
Mkuu hiyo gari ina high perfomance engine 2000cc.Watu wengi wana iconfuse na kufikiri ni sawa na Corolla!Hii gari ni kiboko, ina perfomance bora kuliko Chaser au gari inayolingana na Chaser.Ukitaka kuijua Subaru piga long trip kama Mbeya au Arusha ndo uyaiheshimu.Its a leader in its class.
2000 cc inakunywa utafikir 4500 cc!!! Ina high perfomance lakini fuel consumption ni mbayaaaaa....1 litre =5 km, too much kwa 2000cc, engineering yao sio nzuri, mana inakunywa kama Supercars (Lambos, Ferraris, Aston Martin, maseratti....) tena these cars zina high CC kuliko subaru.... Na still subaru inakunywa kama hizo! If so they suck!
 
Ukianza kuifumuafumua ndio itakuja kukupa uchizi...kama unaipenda ipaki uwe unatembea nayo pochi ikiwa vizuri...lacvyo kaa kando na member ''Shark'' mwenye ''tatizo la kununiwa'' muongee biashara ukachukue anotha...do your research next time.
 
Mkuu ni kweli kuna siku jamaa mmoja alinitesa sana Mbwewe mpaka Manga njia ya Tanga wakati mimi nilikuwa na gari yenye engine ya 1G,nilimuiliza jamaa yangu performance za Subaru akaniambia achana nazo kwa gari hizi za kawaida,ilibidi nitafute nikapata Legacy touring lakini mbona kwenye mafuta sio kama anavyolalamika huyu bwana au kuna kasoro kwa sababu haina tofauti kubwa sana na gari ya cc 2000.
Kweli mkuu, ulaji wa mafuta wa Subaru si mbaya kama invyodhaniwa. Ila ukii-compare na starlet au Vitz hapo suala lingine.
 
Nakushauri uwe unachakachua kwa kuchanganya na maji kidogo labda itakupa unafuu
 
Mkuu uko wapi? Maana ulaji huo sio wa kawaida nimetumia hizo gari hazili hivyo !

Niko Dar man khaaa siielewi hii gari nimeambiwa sababu ya turbo sielewi kwani turbo inakulaje mafuta wkt inafunguka ikifika speed 100!na dar speed hiyo kwa mwezi unahesabu
 
Nineweka full tank lita 65 ajabu nimetembea km 350 mafuta kwishney leo nimejaza tena

Weka fuel extreme...... aU Changanya na mafuta ya Transfoma kitu hakiishi,Waulize wakaanga chips watakwambia wese linakaa mwezi mzima.
 
Mkuu hiyo gari ina high perfomance engine 2000cc.
Watu wengi wana iconfuse na kufikiri ni sawa na Corolla!

Hii gari ni kiboko, ina perfomance bora kuliko Chaser au gari inayolingana na Chaser.

Ukitaka kuijua Subaru piga long trip kama Mbeya au Arusha ndo uyaiheshimu.
Its a leader in its class.
Mkuu hapo umedanganya, labda utueleze ni chaser ipi, ulaji mafuta wa chaser gx100 engine beams 2000 vvti, huwezi kuulinganisha na subaru aidha mjini au safarini, subaru inakunywa mafuta sana kulinganisha na hii chaser.
Subaru ina full time 4WD au AWD hivyo ni lazima ile mafuta zaidi na pia ni nzito kuliko chaser na ina 4 inline cylinders engine.
chaser gx100 ni compact na ina six inline cylinders vvti ngine with rear drive only na ni nyepesi kuliko subaru. hivyo chaser ni far more economic than subaru. chaser ikiwa nzima inakwenda hadi 12km/liter in town na hadi 17 km/liter safarini.
 
Mkuu ushatembea safari ndefu na VW Golf? Subaru itasubiri sana pale by the way subaru kwa gari za Mjapani heshima
 
Niko Dar man khaaa siielewi hii gari nimeambiwa sababu ya turbo sielewi kwani turbo inakulaje mafuta wkt inafunguka ikifika speed 100!na dar speed hiyo kwa mwezi unahesabu

kaka kinachokutesa wewe ni foleni, mi natumia forester na nina average ya 8 hadi 10 ninapoamua kukimbizana na wadau! na kwangu AC is always ON.
 
Niko Dar man khaaa siielewi hii gari nimeambiwa sababu ya turbo sielewi kwani turbo inakulaje mafuta wkt inafunguka ikifika speed 100!na dar speed hiyo kwa mwezi unahesabu

Kuna mafundi pale magomeni shule ya Mzimuni ni wataalamu wa wire unaweza kuwapitia wakaingalia!
 
Mkuu hapo umedanganya, labda utueleze ni chaser ipi, ulaji mafuta wa chaser gx100 engine beams 2000 vvti, huwezi kuulinganisha na subaru aidha mjini au safarini, subaru inakunywa mafuta sana kulinganisha na hii chaser.
Subaru ina full time 4WD au AWD hivyo ni lazima ile mafuta zaidi na pia ni nzito kuliko chaser na ina 4 inline cylinders engine.
chaser gx100 ni compact na ina six inline cylinders vvti ngine with rear drive only na ni nyepesi kuliko subaru. hivyo chaser ni far more economic than subaru. chaser ikiwa nzima inakwenda hadi 12km/liter in town na hadi 17 km/liter safarini.
Mkuu pengine sikueleweka na neno "performance".
Maana yangu ni mikiki ya hii gari, acceleration ni explosive na kwa vile ni turbo-charged gari chache zina weza kuperform vitimbwi vyake.
Pengine katika kula mafuta Chaser inaweza kuwa ina ubora kidogo maana ni gari niliitumia 10 years ago, lakini kwa speed, maneuverability, stability at high speed , I would go for Subaru.
 
Mkuu hiyo gari ina high perfomance engine 2000cc.
Watu wengi wana iconfuse na kufikiri ni sawa na Corolla!

Hii gari ni kiboko, ina perfomance bora kuliko Chaser au gari inayolingana na Chaser.

Ukitaka kuijua Subaru piga long trip kama Mbeya au Arusha ndo uyaiheshimu.
Its a leader in its class.

Mkuu ni kweli ni leader kwenye league lakini ni GAS GUZZULER vile vile, inafaa katika mashindano ya magari au mtu mwenye pesa za kumwaga. Akiona vipi basi aibadirishe/modify iwe inatumia GAS badala ya mafuta, lakini performance yake itakuwa degraded kidogo.
 
Mkuu ushatembea safari ndefu na VW Golf? Subaru itasubiri sana pale by the way subaru kwa gari za Mjapani heshima

Mkuu, heshima mbele kwa gari yoyote ya mjerumani.
Gari za mjapani kwa kawaida gearbox iko syncronised kwa speed ya hadi 180km/hr kulingana na sheria zao.
Lakini mjerumani kwenye outobahn zao gari zao ziko sync hadi 240-280km/hr!!!
Hata hivyo hal hla , ni sehemu chache sana nchini za "kupaa" hata kwa hiyo 180km/hr!!!
 
Mkuu pengine sikueleweka na neno "performance".
Maana yangu ni mikiki ya hii gari, acceleration ni explosive na kwa vile ni turbo-charged gari chache zina weza kuperform vitimbwi vyake.
Pengine katika kula mafuta Chaser inaweza kuwa ina ubora kidogo maana ni gari niliitumia 10 years ago, lakini kwa speed, maneuverability, stability at high speed , I would go for Subaru.

Nimekuelewa mkuu kwa ulichomaanisha
 
Wenzio tunawekamo engine za corolla. Engine hiyo tupia mbwa wale.

Hahahaha....umenikumbusha mbali aisee...mimi nakumbuka nilinunua BMW kwenye mnada ilikua imekufa engine ila body ikawa iko powa, nililnunua kwa milioni mbili na nusu...nikaenda kariakoo nikanunua engine ya mark II laki sita unusu nikawa nimemaliza kazi...barabarani watu wananitolea mcho kumbe gari hata milioni 4 haijafika.... mjini bwana.
 
2000 cc inakunywa utafikir 4500 cc!!! Ina high perfomance lakini fuel consumption ni mbayaaaaa....1 litre =5 km, too much kwa 2000cc, engineering yao sio nzuri, mana inakunywa kama Supercars (Lambos, Ferraris, Aston Martin, maseratti....) tena these cars zina high CC kuliko subaru.... Na still subaru inakunywa kama hizo! If so they suck!

Hivi Electronic Fuel Injection yake niya single point au multi point? Yasije yakawa ni magari yanayo tumia carburator mbili badala ya E.F.I lakini sidhani, niliwahi kununua gari la TOYOTA CAMRY kutoka Uingereza lenye European Specs, CC zake ni 2000 E.F.I ni Multipoint lakini ulaji wa mafuta ni close na pikipiki ya 850CC, sasa ya kwako tatizo linatokana na nini?

Lakini looking back, kama Engine yenyewe sio natural aspiring i.e inatumia turbo charger basi fuel to AIR ratio itakuwa kubwa SANA inachanganya mafuta mengi sana na hewa ku-boost performance, ukubwa wa injini unaweza kuwa ni CC 2000 lakini kutokana na kuwa-turbo charged performance yake italingana ya injini ya CC3500, najaribu ku-analyse kisayansi - ndio maana inakula mafuta kama mchwa.

Kama gari yako bado unaipenda kabadirishe Engine weka ambayo inatumia mfumo wa natural aspiration na siyo Engine yenye turbo charger, chukua ya CC 2000 yenye E.F.I ya multipoint - utakuja kuniambia. Good luck.
 
Hivi mkuu mi najiuliza hiyo subaru mnasema inakimbia sana,kwa hiyo mkitoka na hizi gx 100 vvt-i haiwezi kufata ?maana hizi mia nazo si mchezo !!
 
Back
Top Bottom