Sukari imepanda Bei. Hapo ulipo bei ipoje?

Sukari imepanda Bei. Hapo ulipo bei ipoje?

Jana asubuhi nilimtuma mtoto na shillingi 8,400 kununua sukari kilo tatu nikifahamu mteja wangu huwa ananiuzia sukari Tshs. 2,800 kwa kilo.

Mtoto alirudi mikono mitupu akanieleza kuwa sukari imepanda bei na sasa kilo moja ni Tsh. 3,500. Nilishtuka sana na mpaka sasa sijaamini.

Nina maswali yafuatayo kwa Serikali:

1. Ongezeko hili limesababishwa na nini?

2. Je, kama Serikali mlitoa taarifa kwa wananchi kuhusu ongezeko hili?

3. Je, mnajua wananchi wengi hawataimudu bei hii?

4. Je, Serikali haijui kuwa Wananchi tunakosa imani na Serikali yetu?

Ninaomba majibu ya maswali yangu.
Jana nmenunua 4000 ile ya bwana sukari. Nlikuwa nikiinunua kwa 3000
 
Nimesoka ktk ukurasa wa twitter wa waziri wa kilimo akionyesha mapungufu ya uzalishaji sukari ktk viwanda vyetu.

Lakini hajaeleza mikakati gani inafanywa na serikali kufidia huo upungufu kwani hali ya upatikanaji na bei ya sukari ni mbaya sana. Sehemu nyingi za nchi sukari ikipatikana bei yake ni kati ya tsh.3800/= mpaka 4000/= kwa kilo 1.

Ushauri kwa serikali ni kuagiza sukari kutoka nje ya nchi ili kukabili huo upungufu kwani wananchi wanateseka sana.

Sent from my sm-a145r using jamiiforums mobile app
 
Wafanyabiashara washaona wasipopiga hela kwenye huu utawala hawatapiga tena
 
Uzalishaji wa Sukari inayotumiwa Nyumbani katika Viwanda vya Ndani umeripotiwa kushuka na kusababisha Serikali kutoa Vibali vya uagizwaji Tani 100,000 za Sukari kutoka nje ya Nchi ili kukidhi mahitaji.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Kilimo Tanzania, sababu ya kushuka kwa uzalishaji ni kutokana na Mvua kubwa zilizosababisha Mashamba ya Miwa kujaa maji na hivyo Miwa kuoza na mingine kupungua kiwango cha Sukari (Molasses) inayotakiwa.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema sababu nyingine mi Viwanda viwili vya TPC Limited na Bagamoyo Sugar vilivyosimamisha uzalishaji kwaajili ya matengenezo na hivyo kuongeza uhaba wa Sukari Nchini.
 
Chadema watasema wanataka kunadamana Kwa sababu bei ya sukari ni kubwa hivyo wakiandamana itashuka 😁😁

Next time Serikali iwe inanunua sukari ya dharura na kutunza kwenye maghala Ili ikotokea upungufu wanaiachia sokoni.

Asali inaweza kuwa mbadala
 
Waziri hii sio kweli haiwezekani Zimbabwe,Malawi,Uganda,Zambia na Eswatin wao kila mwaka wanazidisha kiwango cha uzalishaji na ndio hao hao Ilovo na huku mnakuja na hadith ile ile tuu...

Tanzania hamjawahi kuzalisha kwa kuzidi kiwango kila mwaka mnapanga watu wa kuwapa vibali ili waleta Sukari kutoka Nje Sukari sio Big ishu sema mmeweka password ndio maana inaoneka Big ishu..
 
Waziri hii sio kweli haiwezekani Zimbabwe,Malawi,Uganda,Zambia na Eswatin wao kila mwaka wanazidisha kiwango cha uzalishaji na ndio hao hao Ilovo na huku mnakuja na hadith ile ile tuu...Tanzania hamjawahi kuzalisha kwa kuzidi kiwango kila mwaka mnapanga watu wa kuwapa vibali ili waleta Sukari kutoka Nje Sukari sio Big ishu sema mmeweka password ndio maana inaoneka Big ishu..
Som haya maelezo harafu useme kwamba Waziri kakosea wapi.

Mwaka huu ndio ilikuwa tufikie viwango rasmi vya mahitaji ila ndio mambo yameingiliana.

Hizo Nchi unazotaja Zina Mapebari wa miaka Mingi sie ni recently ndio tumepata walau viwanda vipya 2

View: https://www.instagram.com/p/C2UMkX0I_2O/?igsh=MXRlaWZ3emxzN3h1ag==
 
Mkuu fanya kazi tuu hii biashara haramu ukiweza fatilia kidogo upate nyama nyama zake watu wanauana kwenye vibali hivyo..Sukari sio Big ishu na haijawahi kuwa Big ishu ni vile Tanzania wahuni wanatengeneza mazingira ya kupata fedha kupitia Sukari kila mwaka uliza mipakani kwa Nchi nilizotaja upate bei ya sukari kwa nusu bei ya ilipo Tanzania kwa sasa wao kila mwaka sukari ipo kidogo wanatoa vibali hawajawahi kuwa na bidhaa inayozidi...
 
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema hali ya uzalishaji wa sukari katika viwanda saba nchini imeshuka hadi kufikia tani 1,000 kwa siku kutokana na mvua za El-nino zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.

Akitoa kauli ya serikali leo Jumamosi kuhusu hali ya sukari nchini, Bashe amesema katika kukabiliana na uhaba wa sukari ambao sasa umefikia tani 30,000, serikali imetoa kibali kwa wenye viwanda kuagiza sukari tani 100,000 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini tarehe 23 - 24 Januari mwaka huu.

“Uzalishaji wa sukari katika taifa kwa kipindi cha miaka mitatu uliendelea kuongezeka kiasi kwamba sugar gap kwa mwaka jana ilishuka mpaka kufika wastani wa tani 30,000 na mwaka huu tulitarajia kumaliza kabisa gap ya sukari katika Taifa letu.

Hata hivyo amesema kutokana na hatua zilizochukuliwa anaamini ifikapo katikati ya Februari hali ya upatikanaji wa sukari itaanza kurejea katika hali ya kawaida na kutokuwa na madhara yoyote.

Source - EATV
 
Habari Tanzania!

Nipende kukiri kuwa sukari inatumika katika jamii na inatumika katika bidhaa nyingi hasa za viwanda. Ukweli katika kuelimishana; Isipokuwa kupanda kwa sukari hakuna matokeo hasi yoyote yale kwa jamii zaidi ya kuwa na matokeo chanya juu ya jamii katika afya na uchumi wao.

Afya na uchumi wa Afrika unaharibiwa sana na bidhaa za sukari hasa katika kustawi na kukua kwa maendeleo ya nchi (Kijamii na Uchumi).

Sukari sio sababu ya wewe kulalamika kama una macho ya kuona mbali kuhusu jamii na uchumi.

Asante.
 
Walioficha sukari anzeni kuuza sasa kwani ulanguzi hautakuwa na faida tena.
 
Mpk February mtakuwa mshajipigia fedha za kutosha kutoka kwa mambugilaaa

Ova
 
Back
Top Bottom