Sukari madukani hamna, tatizo ni nini wakati tayari kuna bei elekezi toka Serikalini?

Sukari imekuwa bidhaa adimu jijini Dar es salaam.

Maduka yote makubwa ya jumla haipatikani.

Kabla ya kupotea ilikuwa inauzwa 127 000/50kg. Bei hii ni 2540, wakati bei elekezi iliyotangazwa na serikali kwa DSM ni 2600.

Kwa maana hii serikali inawapangia wafanyabiashara wapate sh 60 tuu kwa kilo bila kujali gharama zingine.

Serikali ichukue hatua nzuri kwenye hili swala la sukari.

Mara zote serikali ndio inatibua bei ya sukari.
 
Waziri alisema sukari iko bandarini!
 
Kwa sisi WANYONGE hata ikifika 10,000/ kwa kg hakuna shida,tutanunua tu,anaeona sukari inauzwa bei kubwa,akalime miwa!
Niko Msolwa huku, kwenye shamba langu la muwa.
 
WAnaleta siasa kwenye biashara.
Watuuzie sasa hiyo siasa ili tuweke kwenye chai.
 
Hizi ndio bei elekezi kwa Mikoa yote,chunguzeni kwa makini bei za mkoa wa Dar es salaam mtapata majibu sahihi kwa nini sukari hamna madukani,maana haiwezekani kwa mtu wa dsm auze sukari kilo 50 na kupata faida ya tsh 3000,wakati mikoa mingine wanapata zaidi ya 13000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…