Sukuma gang ni itikadi siyo kabila

Sukuma gang ni itikadi siyo kabila

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Sukuma gang ni itikadi liyoasisiwa na Magufuli inayoamini katika ukatili unaohusisha matusi, utekaji, uporaji, mauaji na uonevu.

Kwahiyo itikadi hii isihusishwe na kabila la Wasukuma. Mfano, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, ndugu Sabaya yeye ni Sukuma gang lakini siyo Msukuma. Wengine ni Polepole, Ndugai, Bashiru, Mnyeti, Happi, Kabudi, n.k.

Lakini wapo Wasukuma ambao pia ni wafuasi watiifu wa itikadi hii ya sukuma gang. Sina haja ya kuwataja.

Nimeandika haya ili kuondoa dhana inayotaka kujengwa na baadhi ya watu ama kwa upotoshaji wa makusudi au kwa bahati mbaya kuwa kuwachukia wafuasi wa Sukuma gang ni kuchukia Wasukuma. Hili siyo jambo zuri na kufanya hivyo ni kupanda mbegu ya ukabila.

Mm Sexless mwandishi wa uzi huu nawachukia Sukuma gang na muasisi wao ingawa nami ni Msukuma.
 
Ni kweli lakini usimwagie maji hoja ya kuoanisha usukuma na Sukuma Gang.

Nami ni mnantuzu chotara(msukuma wa Bariadi) lakini siungi mkono Sukuma Gang.

Tukubali tusikubali, wakati wz Awamu ya Tano, kuna wakati Cabinet ilikuwa na wasukuma wengi kiasi cha kuongea kisukuma kujadili hoja.

Na teuzi nyingine zote zilitoka Lake region.

Hilo halina ubishi.
 
Dhambi mnayofanya wachaga wa Chadema kuwabagua na kuwadhalilisha wasukuma ipo siku itawatafuna.
Wasukuma watawashikisha ukuta chadema na uchaga wao mwakani na 2025.

Kwa kua sasa chama cha kichaga kimegundua hakina nafasi zaidi ya kukubaliana na CCM ili angalau 2025 wakikosa chochote Samia aendelee kuwakumbuka.

Chadema na wachaga ndio wamepanda huu ukabila. Cha ajabu, Mbowe maandamano, mikutano ya siasa na kampeni anazindulia Usukumani hadi sasa sijasikia mkutano wa kisiasa Kilimanjaro ama Arusha ila kila siku Mwanza, Shinyanga, Kahama, Geita, Simiyu, Tabora nk.

Mikutano ya msingi kama ya wanawake ndio anapeleka Moshi, mikutano ya fujo, uharibifu anapeleka Usukumani wakati huo huo anawatukana wasukuma.
 
Ni ujinga wa aina fulani kufungamanisha kabila fulani na jina la kundi fulani, halafu ukasema eti jina la kundi hilo ni falsafa na haihusiani na kabila tajwa...
Wasukuma wapi wewe, sis wasukuma tupo na hilo genge la sukuma gang tunalijua ni kundi la waimba mapambio ya magufuli kama kina kabudi,

Ndugai, Sabaya na wapumbavu wengine wakiwemo wasukuma wenzetu ndio maana sis wasukuma hilo genge tulishalipuuza na kama hamjui huku kanda ya ziwa chadema ndio kila kitu na mikutano mmeiona ilivyofurika wasukuma huku ccm mmeshindwa hata kuitisha mikutano huku maana mtaambulia aibu.
 
Wasukuma watawashinda chadema na uchaga wao mwakani na 2025.

Kwa kua sasa chama cha kichaga kimegundua hakina nafasi zaidi ya kukubaliana na CCM ili angalau 2025 wakikosa chochote Samia aendelee kuwakumbuka...
wasukuma wapi njoo maeneo ya simiyu eg maswa, meatu, bariadi,shinyanga,kahama, malya, sumve, ngudu, nyamagana, ilemela na maeneo mengine utafute CCM kama inasapoti yoyote kutoka kwa wasukuma uone matokeo yake ndio maana wabunge wa mchongo huku kwa wasukuma hawawez hata kuitisha mikutano wakapata watu.
 
Dhambi mnayofanya wachaga wa Chadema kuwabagua na kuwadhalilisha wasukuma ipo siku itawatafuna.
hio kete itawazika ccm kama hamjui na kwa taarifa yenu sukuma gang huku kanda ya ziwa tunawajua na hamuwez kutuhadaa wasukuma.
 
wasukuma wapi wewe, sis wasukuma tupo na hilo genge la sukuma gang tunalijua ni kundi la waimba mapambio ya magufuli kama kina kabudi,ndugai,sabaya na wapumbavu wengine wakiwemo wasukuma wenzetu ndio maana sis wasukuma hilo genge tulishalipuuza na kama hamjui huku kanda ya ziwa chadema ndio kila kitu na mikutano mmeiona ilivyofurika wasukuma huku ccm mmeshindwa hata kuitisha mikutano huku maana mtaambulia aibu.
Wewe sio msukuma! Kwa nini msiite Magufuligang? Jinga kabisa achana na wasukuma mpuuzi wewe!
Kama ni msukuma ni jinga kabisa na haujiamini!
 
Sukuma gang ni itikadi liyoasisiwa na jiwe inayoamini ktk ukatili unaohusisha matusi, utekaji, uporaji, mauaji na uonevu.

Kwahiyo itikadi hii isihusishwe na kabila la wasukuma. Mfano, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, ndugu Sabaya yeye ni sukuma gang lkn siyo msukuma. Wengine ni Polepole, Ndugai, Bashiru, Mnyeti, Happi, Kabudi, n.k

Lakini wapo wasukuma ambao pia ni wafuasi watiifu wa itikadi hii ya sukuma gang. Sina haja ya kuwataja.

Nimeandika haya ili kuondoa dhana inayotaka kujengwa na baadhi ya watu ama kwa upotoshaji wa makusudi au kwa bahati mbaya kuwa kuwachukia wafuasi wa sukuma gang ni kuchukia wasukuma. Hili siyo jambo Zuri na kufanya hivyo ni kupanda mbegu ya ukabila.

Mm Sexless mwandishi wa uzi huu nawachukia sukuma gang na muasisi wao ingawa nami ni msukuma.
Mnaanza kuwaogopa eee
 
Sukuma gang ni itikadi liyoasisiwa na Magufuli inayoamini katika ukatili unaohusisha matusi, utekaji, uporaji, mauaji na uonevu.
Mkuu Sexless , kwanza nikupongeze kuileta hoja hii, pili naomba kuitumia hoja yako hii kama mbegu ya kuonyeshea bandiko langu fulani, na tatu japo ni kweli neno Sukuma Gang ni itikadi tuu, lakini si kweli kuwa iliasisiwa na Magufuli!. Tumwacheni Magufuli apumzike kwa amani!. Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

The Sukuma Gang ni a fictitious Group that doesn't exist in reality lililobiniwa na yule Kigogo wa Twitter na watu wajinga wajinga wenye akili fupi wakaamini hili kundi ni kweli lipo!. Kiukweli kabisa Sukuma Gang sio kundi la kweli, halipo popote and don't exist anywhere in reality except ndani ya vichwa vya watu waliofilisika kisiasa!.
Kwahiyo itikadi hii isihusishwe na kabila la Wasukuma. Mfano, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, ndugu Sabaya yeye ni Sukuma gang lakini siyo Msukuma. Wengine ni Polepole, Ndugai, Bashiru, Mnyeti, Happi, Kabudi, n.k.
Pia sii kweli!, bali baada ya Kigogo wa Twitter kuliasisi kundi hili fictitious, akatumia nguvu kubwa kulifanyia indoctrination kuwa hili kundi does real exist, hivyo wale watu wa Magufuli na watu wote wanaomsupport Magufuli wakawa pointed kuwa ni members wa Sukuma Gang, hata mimi ni Msukuma, na namsupport Magufuli na sio Sukuma Gang!.
Lakini wapo Wasukuma ambao pia ni wafuasi watiifu wa itikadi hii ya sukuma gang. Sina haja ya kuwataja.
Hakuna kitu kama hiki, ila kwa vile indoctrination ya existence ya uwepo wa kundi hili imefanyika na watu wenye akili fupi waliofilisika kisiasa wakaamini', kama na wewe unaamini kuwa kundi la Sukuma Gang kweli lipo and does exist in reality, ujijue ni akili fupi and muflis kisiasa kama wale muflis wengine wote wanaoamini ujinga huu!
Nimeandika haya ili kuondoa dhana inayotaka kujengwa na baadhi ya watu ama kwa upotoshaji wa makusudi au kwa bahati mbaya kuwa kuwachukia wafuasi wa Sukuma gang ni kuchukia Wasukuma. Hili siyo jambo zuri na kufanya hivyo ni kupanda mbegu ya ukabila.
Hapa nakuunga mkono!.
Mm Sexless mwandishi wa uzi huu nawachukia Sukuma gang na muasisi wao ingawa nami ni Msukuma.
Kumchukia mtu yoyote kwasababu yoyote sio jambo jema!. Dini zinatufunza hata adui mpende!. Hivyo it's not right kumchukia mtu yoyote!.

Japo hii shana ya the existence of the Sukuma Gang ni dhana tuu, na the Sukuma Gang ni just a fictitious Group that doesn't exist in reality, lakini kufuatia indoctrination iliyofanywa na yule Kigogo wa Twitter, watu wenye akili ndogo, akili fupi na waliofilisika ki fikra, wakaamini, hivyo chuki dhidi ya Wasukuma is real!. Hili sio jambo jema!.

Kufuatia kabila la Wasukuma kuwa ndilo kabila kubwa Tanzania kuliko makabila yote, zikitokea nafasi zozote za uongozi, na watu wote wako huru kugombea, obviously Wasukuma pia lazima watakuwepo.

Kulitokea nafasi fulani za uongozi ndani chama fulani, wakajitokeza wagombea 186 kugombea nafasi 8 aa uongozi. Miongoni mwa waliojitokeza walikuwepo Wasukuma wengi tuu ila mimi nawajua kulikuwa na Wasukuma wawili ambao kama wangepitishwa wangetupatia wawakilishi wazuri the best of the best.

Ikasemekana kuwa mmoja kati ya hao Wasukuma wawili ni member wa the Sukuma Gang!. Then kwenye mchujo ikaelezwa kuwa wamepewa maelekezo hatua ya kwanza kabisa ni kuwakata Wasukuma wote waliojitokeza!. Na kweli Wasukuma woote tukakatwa eti ni Sukuma Gang!. This is not fair at all!. Taifa linakosa uwakilishi wa watu wazuri kwa ubaguzi wa kijinga kabisa!.

Na katika hili naomba na mimi nijiunge kwenye kukemea hii sumu ya ubaguzi mbaya kabisa ya kuwabagua Wasukuma kwa kisingizio cha Sukuma Gang, na naomba kutamka kama kuna Msukuma yoyote popote ameadhibiwa au kubaguliwa kwa kisingizio ni member wa the Sukuma Gang, then dhambi hiyo ya ubaguzi, itawatafuna wabaguzi hao kupitia kitu kinachoitwa karma!. Karma haina mswalie Mtume wala haijali nani ni nani!.

P
 
Back
Top Bottom