A
Anonymous
Guest
Mimi na wenzangu kadhaa tunaosomea Shahada ya Uzamili (Master of Public Health - MPH) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tuna changamoto moja kubwa ambayo imekuwa kero kwa muda mrefu na kuendelea kuifumbia macho itakuwa ni sawa na kuendelea kufuga mtatatizo.
Tatizo letu kubwa ni kuhusu utendaji unaofanywa na Wasimamizi wa Kazi za Utafiti za Wanafunzi (Supervisors wa Research), hawa watu wa muda mrefu wamekuwa ni tatizo na kama hali hii haitekemewa au kuchukuliwa hatua watakuwa ni kati ya sababu zitakazokimbiza Wanachuo kusoma UDSM.
Kabla ya kuanza kusoma Masters hapo UDSM baadhi yetu tuliambiwa na waliosoma kuwa bora tutafute chuo cha binafsi kuliko kusoma hapo, tulipouliza tukaambiwa ni jambo gumu sana kuhitimu Masters na ukifanikiwa mara nyingi lazima uwe nje ya muda hata kama unasoma vipi na kujituma.
Utaratibu uliokuwepo siku za nyuma ilikuwa unapofika muda wa kukamilisha kazi yao na ukazidisha ilitakiwa mhusika alipe Tsh. 50,000 kwa kila mwezi, lakini sasa hivi utaratibu ulivyo ukichelewa kukamilisha Reasearch yako unatakiwa kulipa hela ya Semister nzima ambayo ni Tsh. Milioni 2.5
Uongozi wa UDSM unafanya hivyo kwa kuwa hauambiwi ukweli kuwa asilimia kubwa wanaosababisha Wanafunzi wanashindwa kukamilisha tafiti zao ndani ya muda ni Supervisors.
Supervisors wanajiona kama Miungu watu, kwanza unapopewa akusimamie picha linaanza kuja kumpata ni unatakiwa kuacha kazi upate kazi ya kumtafuta yeye.
Ukifanikiwa kumpata anaweza kukupa maelekezo ya kazi au ukamkabidhi kazi yako ili aipitie lakini akachukua zaidi ya miezi miwili kuipitia au kuja kumuona tena.
Tuna wenzetu ambao tulianza nao Masters pamoja, wao wapo katika vyuo vya binafsi kama ilivyo Chuo cha SAUT, sasa hivi wanaelekea kuhitimu, sisi ndio kwanza tunaendelea kuimba mapambio ya kuwatafuta Supervisors.
Mfano darasa letu tulikuwa Wanafunzi kati ya 25 hadi 30 lakini hivi tunavyoandika hapa wanaotarajia kuhitimu ni wawili tena ambao nao wamechelewa.
Supervisors ni shida, hawapatikani kirahisi na baadhi yao ukiwapata hawakupi majibu mazuri.
Ukisema uende ukashtaki au kuwasilisha malalamiko yako juu ya Supervisors, huwezi kupata msaada kwa kuwa unaenda kushtaki kwa wenzao.
Pili, suala la kutakiwa kulipa ada ya Semister nzima kwa uzembe unaofanywa na Mtumishi wa Chuo ni maumivu makubwa kwetu tunaosoma.
Kozi ya Miezi 18 unajikuta umeisoma Miaka mitatu, hapo unalipa ada ya Tsh. Milioni 7+ kisha uambiwe tena ulipe Tsh. Milioni 2.5 ni mateso yasiyo na maelezo hasa kwa kuw wengi wetu tunaosoma chuo hicho ni Wafanyakazi na wengine tuna familia.
Tunakuwa hatueleweki, kutumia muda mwingi kusoma, hela ya familia pia tunaipeleka
Uongozi unapewa taarifa tofauti
Tumefuatilia na kugundua kuwa Uongozi haufikishiwi taarifa sahihi, wanajulishwa Wanafunzi ndio wenye shida lakini uhalisia ni tofauti.
Hii ikiendelea UDSM itaendelea kukimbiwa kwa kuwa hakuna anayeweza kuvumilia usumbufu huo na kupoteza hela bila sababu za msingi.